HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 15
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "Season 15

ILIPOISHIA JANA
Nilianza kupekuwa katika masanduku na kila kona kujaribu kuikumbuka namba hii bila ya mafanikio na wazo la pili likawa ni kujaribu kila namba inayoishia na hivyo ili kujua nini kimo ndani hizo.
Moja kati ya namba hizo nilizojaribu ilipokelewa na ..............................
ENDELEA
MOJA kati ya namba hizo nilizozijaribu ilipokelewa na kampuni moja binafsi ya ulinzi kitengo cha zimamoto na wakaniuliza kama kuna taarifa nilitaka kutoa muda huo. Kidogo niombe msaada wa kuja kulizima tatizo langu lakini niliishia kusema ni wrong number na kuendelea mambo yangu.
Niliduwaa paloe sebuleni kwa muda nikiwa na glas yangu ya maji ili kushusha presha na kisha nikajivuta chumbani ili nipumzike kwa ajili ya siku ya pili. Usiku haukuwa mfupi kwani nilikuwa nikihisi mauzauza ya kila aina yakiniandama.
Asubuhi yake niliamka mapema na kujiandaa kwenda kazini wakati niko njiani maeneo ya Mafiati nilisimamishwa na trafiki ambaye aliniuliza ni kwa nini gari langu linayumba sana? Na kwa muonekano ni kama nimelewa vile?
Jinsi nilivyozidi kuongea nae aligundua nina usingizi mzito sana na kuniamuru nilipaki gari na kunipiga fine huku nikiamriwa kumwita dereva mwingine aje pale kunichukua na kunirudisha nyumbani.
Nikiwa ndani ya tax na gari langu nikiwa nimeliegesha bar moja pale maeneo ya Mafiati kwa ahadi ya kuja kulifuata mida ya jioni na ofisni nikiwa nimewapigia simu kuwa sitoweza kufika huko,mara kuna kitu cha ajabu kilijitokeza.
Mara hii niliiona namba ile ile ya 200802 ikiwa na kodi za mtandao fulani wa simu hapa nchini na ikiwa kwenye ukurasa mmoja wa gazeti moja la udaku tena chini ya tangazo la mganga mmoja wa jadi aishie mbozi.
Usingizi wote ulinitoka na safari ya nyumbani ilisitishwa baada ya kuipigia namba ile na kuongea na bibi mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mganga wa kienyeji aitwaye GUSA UNATE.
Mbaya zaidi ni kwamba hata kabla sijamaliza kumwabia kisa changu alianza kuniambia matatizo yangu kuwa nimetupiwa jini aitwaye KWANGUA VOCHA na kuwa huyu jini ni hatari sana anapatikana kwenye simu hasa za kuperuzi hivyo niende mara moja.
Dereva alilikimbiza lile gari zaidi ya mbio za magari ya mwenge mpaka tulipoliona bango la mganga lililoandikwa Gusa Unate Clinic na hii ikaashiria kuwa tulikuwa tumewasili eneo husika.
Nilishuka na kuingia kwa mganga ambaye alinipokea kwa kunizaba vibao kama sita mfululizo na msaidizi wake alinishika na kunitoa pale mapaka sehemu ya pumzikia ambapo dakika mbili baadae bibi gusa unate alikuja akiwa ameshika chungu kikubwa cheusi kikifuka moshi mkubwa na kuniambia. "SOGEA HAPA, Tena ulikuwa na dakika 25 tu za kuishi"
Nilianza kutokwa na machozi ambayo yalitokana na hofu ya kifo pamoja na kumbukumbu ya vibao vya bibi yule ambaye alikuwa akinizaba kama vile kanikuta na mjukuu wake.
Aliuinamisha uso wangu kwenye kile chungu kinachotoka moshi na ni mara hii nikagundua hata macho kutoa machozi yalisababishwa na moshi huo wenye pilipili.
Nikaona kama FFU walikuwa maeno hayo na bomu la machozi limeachiwa, alinizaba kofi moja la kisogo na kumbukumbu zangu zikanirejea tena na safari hii akaniambia kuwa nikae na kumsikiliza kwa makini zaidi.
" Kijana umetupiwa jini aitwaye Kwangua Vocha ambaye hukaa kwenye simu kama yako... Umenunua bei gani simu hiyo?"
Nikamjibu laki saba na nusu tu.
"Pumbafu sana wewe mjukuu, unanunua simu za bei kubwa hifi? Unaona sasa jini huyu hupenda sana kukaa kwenye simu za aina hiyo hasa kama hii yako ya kuperuzi peruzi hebu weka hapa chini, toa laini, dumbukiza kwenye chungu hiyo laini"
Wakati nafanya hivyo hali yangu haikuwa njema kabisa kwani nilibanwa na tumbo la kuhara lililoambatana na hofu na kwa mikwara ile kwamwe hata kama ungekuwa wewe usingethubutu kuongea neno.
" eenh tena nimekumbuka, jini huyu huwa anakuwa na mtoto wake je umekumbuka kuja naye?" Bibi aliniuliza ingawa sikuweza kuelewa kwa mara moja nini maana yake mpaka pale aliponiambia kuwa mtoto huyo ni chaja ya simu hiyo.
Akanitaka nirudi haraka mjini kuifuata chaja yake jambo lililonifanya niamke haraka na kuanza kuondoka na dereva yule ambaye muda wote huo alikuwa akikohoa kutokana na moshi wa pilipili nilioingia nao.
Hatukufika mbali kabla ya kukumbuka kuwa ile chaja nilikuwa nayo kwenye mkoba wangu na nafikiri ni ile mikwara iliyonifanya nishindwe kukumbuka kisha nikarudi mpaka kwa bibi ambaye aliichukua na kunipa laini yangu.
Baada ya hapo akanipa dawa ya kunywa nikiwa nyumbani na kusema niache hiyo simu na baada ya wiki nirudi pale nikiwa na ng'ombe, mchele, kuni, mafuta, ndizi, pilipili, na maji katoni moja ili anifanyie tambiko.
Tuliondoka na dereva wa tax mpaka mjini na baada ya kumlipa na kuniacha kwenye gari langu, nikalichukua gari na kwenda nalo Hangover Bar ili nipate moja ya kujipongeza na kuukaribisha uhuru wa nafsi maana jini Kwangua Vocha alinitesa na kuniondolea uhuru wangu na ni hatari kwa afya....
Wakati nashuka kwenye gari kuingia pale bar kuna rafiki yangu mmoja alinifuata na kuniambia kuwa aliniona maeneo ya mbozi nikiingia barabara ya kwenda kwa mganga gusa unate na kwa kuwa alikuwa na haraka hakuweza kusimama kunisabahi na kuuliza kwa nini nilikuwa naenda kule?
Nilimjibu "kaka wewe acha tuu" tena kwa ushujaa mkubwa sana na ujasiri na kumwona kama ni mpumbavu ambaye hajawahi kukutana na jini kwangua vocha na hajui namna ya kumtoa huyo jini hasa akikuingia mwilini kupitia simu hizi za laki saba.
Kwanza nikamuuliza, "kwani kaka wewe watumia simu gani?" Jamaa akajibu mimi natumia simu ya tochi simu ya kawaida. Nilicheka sana tena kwa dharau na kumwambia ndio maanna wewe jini kwangua vocha hawezi kukupata wewe.
Jamaa akaniuliza, " Duuh kuna jini kwangua vocha ambaye anakaa kwenye simu?????????"
Alinishangaa na hakuamini kuwa pamoja na elimu yangu ningeweza kuwa na imani na vitu vya kipumbavu kama hivyo na kama haitoshi akaongeza kuniambia kuwa ndio maana baadhi ya watu wanadai nina kicha siku hizi.
Maneno yale yalinipa hasira na kumuuliza wewe unajua nini kuhusu huyu jini kwangua vocha ambaye tena ana mtoto wake na wewe hujui lolote... ???
Jamaa alicheka tena na safari hii alicheka zaidi ya ile mara ya kwanza hadi akakaa chini kisha akasema na kama ulienda kwa yule bibi tapeli na mwehu anayejiita gusa unate kweli umegusa na umenaswa.
Kwanza hebu niambie hilo jini kalitoaje? aliniuliza
Nami kwa mkwara mzito nikawambia., " BWana mdogo!!!!! Huwezi kuwa dalali kama hujui mitaa, pale kanipa vibao vichache, moshi wa pilipili na kumchuua huyo jini aliyekuwa kwenye simu yangu na mtoto wake na kawafungia kwenye chungu na kunipa laini yangu ikiwa huru.
Na hapa natakiwa kwenda wiki iajayo nikiwa na ng'ombe, mchele, kuni, mafuta, ndizi, pilipili, na maji katoni moja ili anifanyie tambiko na niwe huru kama zamani.
Jamaa safari hii naye alinipa kibao na kudai nizinduke kwani anahisi malaria inazidi na kuniambia yule bibi ni mwizi na mji mzima wanamjua.
" kwanza hayo aliyokufanyia pamoja na unayoambiwa ukapeleke huoni kama unampelekea chakual? aliongeza jamaa
Kwanza simu na chaja kazichukua yeye na nafikiri atakuwa naye kashajiunga whastapp muda huu. yule bibi ni mtoto wa mjini na ukienda club za usiku humkosi na wanamwita fundi vimeo... ha ha ha ha ha ha wewe fala kweli tena naondoka na sitaki kukaa nawe tena. Alimalizia rafiki yangu na kisha akaondoka
Akaondoka na kuniacha nikiwa na hofu na akili ya haraka ikanijia na kwenda dukani kununua simu na baada ya kuichaji nikaweka laini yangu...
Simu inawaka tuu, nikapigiwa simu na wakati huu yule mpigaji alianza tena kuongea kwa ukali zaidi na kuniambia.....................................
Je wakati huu mpigaji alitaka nini?
Usikose kisa hiki JUMATATU jioni
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu kwa udhamini wa Gracious HOUSE of CAKES watengenezaji maarufu na waliobobea wa keki za aina mbalimbali kwa hafla mbalimbali waliopo jijini Mbeya na wanapatikana kwa namba 0767218014
Nawe waweza kukisoma kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp kwa kuwasiliana na namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo
share, like na comment
0 comments: