Kuku wa miguu mitatu naye ana mambo
Fuledi alikuwa akiendesha gari lake kutoka mji mmoja kwenda mji mwingine, njiani akagundua kwa kuna kuku alikuwa akimfuta huku anakimbia sana.Jamaa akashangaa kuona bado yule kuku anamkimbiza ikambidi aongeze spidi ya gari kutoka 50 MPH mpaka 75 MPH lakini kuku akawa nazidi kuja kwa spidi.
Fuledi akaona isiwe nongwa akaongeza mwendo lakini yule kuku akaja spidi na kumpita fuledi na gari lake.
Wakati anampita fuledi akashangaa kuona kuwa kumbe yule kuku ana miguu mitatu, ikabidi aendelee kumfukuzia na kuona yule kuku anaenda wapi.
Kuku akaingia kwenye shamba moja na baadae kutokezea kwenye jumba ambalo alishangaa kuona kuna kuku wengi wa aina hiyo.
Fuledi akamuona mzee na kumuuliza mbona hawa kuku wana miguu mitatu?
Mzee kajibu, " Niliwapandikiza na ndege wa porini wakatokea hivi nafikir labda watu watawapenda"
Fuledi akauliza tena je umeshawahi kuwaonja na kujua wananogaje?
Mzee kasema hapana nami sijawahi kumshika hata mmoja wala kumlenga kwa manati tangu nianze kuwaweka hapa na hawali hapa pia na mbio zao sio za kawaida.
Fuledi akaondoka akiwa haamini alichokiona na majibu ya yule mzee anayefuga vitu ambavyo hajui thamani wala utamu wake
******************************
Dereva alikuwa akishindana na kitu asichokijua na kuahirisha safari yake ili tu aende kuhakikisha
Mfugaji kazalisha vitu ambavyo hajawahi pata matunda yake na hatafaidi kamwe
******************************
Funzo
Jitahidi kutumia muda mwingi kutengenza vitu ambavyo hata wewe utavifaidi na usiwe kama huyu mzeee
Fuledi ni mfano wa watu ambao huacha mambo yao na kuanza kufuatilia mambo yasiyowahusu au kwa kuwa walidharau nguvu za wapinzani wao
Ukiwa katika ushindani haijalishi umbo la mpinzani wako kila mara amini kuna watu wanafikiri na wana uwezo zaidi yako hivyo jizatiti
Miguu mtatu ya kuku ni sawa na nguvu au uwezo wa ziada ambao kamwe huwezi kuutambua na huwa siri ya watu katika kufanikisha mambo yao
Fuatilia mambo muhimu katika maisha yako
0 comments: