Laptop yaniponza tena........ Mke hajaongea kwa siku kadhaa ..... wadau mliokomaa nipeni ushauri

09:32:00 Unknown 0 Comments



Kiukweli facebook imenikaa akilini sana na mara zote imekuwa njia muhimu kwa mimi kupata warembo na sina cha zaidi hata hizo habari mie sifuatilii kabisa.

Wiki moja iliyopita nilikuwa na safari ya kikazi kwenda kukagua kazi ambazo kampuni yetu husimamia katika miji mwingine nje ya mbeya.

Nikamuaga wife na safari hii sikuweza kutembea na laptop wala simu yangu ambayo naitumia kwa facebook kwa sababu iliharibika na kwenda na laptop niliona ni mzigo na huko tuendako ilikuwa ni kazi na muda wa kuchati ningekosa.

Idadi kubwa ya marafiki zangu wengi wakike ninao wa-add huwa napenda wawe wametoka hapa mbeya ili iwe rahisi kuwabana na hatimaye kufanya mishe mishe zangu.

Mke wangu nikiwa safarini wakati huu aliongeza mapenzi na kuwa ya dhati sana na akawa ananiambia kuwa anatamani nikirudi aandae chakula cha usiku yaani table for two nje ya nyumbani ili tuweze zungumza masuala mbali mbali ya maisha.

Kweli nimerudi akanipokea na tukaenda home na baada ya hapo akaniomba twende out.

Ile naingia hotelini ambako tumekubaliana kwenda nikaanza kuhisi machale yananicheza, maana gari ya mama yangu ikawa pale nje sikupata taabu sana kwani mama hupendelea kupata wine mara nyingi mwishoni mwa juma akijumuika na marafiki zake.

wife akaniambia twende sehemu ya faragha na kukaa wenyewe, kufika hiyo sehemu nashangaa kumwona mama akiwa na mabinti watano ambao watatu nimeshawapitia na tulifahamiana nao fb na wengine nilishawapanga na nikawa najua nikirudi nawamega.

Mara nyingi nilikuwa na sababu za wivu kwa mke wangu na kumzingua sana ili asifuatilie mambo zangu na mama katukalisha mara nyingi na kunionya kuwa napenda vibinti nami nikawa nagoma.

Mama aliponiona naingia akanikaribisha na wale mabinti wakanisalimia nami nikajifanya kutowajua.Mama akaniuliza Fuledi unawapata hawa? Nikajibu hapana.

Wakanipa karatasi zote za chati zangu na wao nikajifanya labda akaunti yangu ya fesibuku wadau walihaki, binti wale watatu wakasimama na kusema na wewe walikuhaki mpaka ukatufuata na tukaenda hoteli na tukafanya yale mambo?????

Jasho likaanza kunitoka na nikaanza kujifanya nimepandisha BP na kisha wakanipeleka hospt.Dokta akadai huyu haumwi wala nini, nikamchukia sana yule dokata wa kike.

Leo ni siku ya pili wife hajaongea neno lolote na sijui nini cha kufanya.

Nimemtafuta rafiki yangu akaniambia wife alimpigia na kumpa mkanda kuwa aliichukua laptop yangu na kuanza kuchati na marafiki zangu wa kike na hata kujionea nini nimekuwa nawasilina nao na kisha kuandaa mapango wa siri ili nidakwe.

Wanawake wanatuzidi akili siku hizi.......


Hii ni story feki tu

You Might Also Like

0 comments: