HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 14

16:43:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Season 14
ILIPOISHIA JANA

Nikiwa katika hali ya kujiweka sawa kwa mapambano na wakati huu ujasiri ukianza kunijia kwa mbali mara simu ya mezani iliita. 

Nilitulia kama sekunde kadhaa nikihofia juu ya simu hiyo kama ni yangu au la na kisha nikaifuata na kuipokea..Kwa kweli simu hii ilibadilisha kabisa mawazo yangu kwani maneno yaliyoongelewa................................................................

ENDELEA
Kwa kweli simu hii ilibadilisha kabisa mawazo yangu kwani maneno yaliyoongelewa yalisisababisha nisimame haraka na kutoka nje huku simu yangu ya mkononi nikiiacha kitandani kwani nilitakiwa na mhudumu nishuke chini akidai kuna mgeni wangu pale mapokezi.

Swali kuu kichwani mwangu lilikuwa ni vipi kuwe na mgeni wangu tena wakati mimi nilitakiwa kuwa mgeni pale??

 Hakika nikaanza kuona kama kuna dalili za mchezo mbaya unaota kunitokea pale hoteli.
Nilifika pale mapokezi na kukutana uso kwa uso na shemeji yangu dada wa mke wangu mama amigo ambaye yeye alikuja pale kwa ajili ya semina na baada ya kuniona nikingia chumbani na anajua fika mdogo wake yuko kijijini akaona ni vyema aokoe jahazi.

Maskini ya Mungu!!, nilimwangalia shemeji usoni na kidogo machozi yanitoke na kuona jinsi baadhi ya kina mama walivyo na upendo wa dhati wa kuokoa ndoa za wenzao wakati sisi wanaume tukizidi kuharibu furaha za ndoa zetu. 

Nilimshika bega na kumwambia, 

"hapana usijali, hapa nimekuja kikazi kuna research naikamilisha hivyo usiwaze shemeji"
Lakini nilijua fika kuwa jibu lile halikumtosheleza wala kuwa na vigezo.Hivi ni utafiti wa aina gani ukafanyika hotelini tena nje ya mji na ni chumbani? Nilijiuliza swali hili kwa upole na unyenyekevu kabisa.

Lakini nikasema moyoni kuwa labda kaniwahi na yeye, maana semina gani iendelee wakati muda huo ni saa moja kasoro? Hapo bwana shemeji kuna jambo.Nilijisemesha huku moyoni tukiachana.

Tuliachana nami nikarudi chumbani na nilipokuwa naingia simu yangu ndio ilikuwa inaishia kuita na kuangalia kulikuwa na missed calls saba wakati naendelea kuitazama ile namba meseji ikaingia.

Meseji ile ilisema, " Mwanaume hutulii wewe, huyo ndio aliyekuita hapa?Nitakasirika na utalipia chumba na kulala hapa mwezi mzima ... pumbavu sana haya hebu ondoka ushanikera mimi"

Daaah !!! Nilishukuru ila nikajifanya kiburi na kuondoka pole pole ila nilipokaribia mapokezi simu ikaanza kuita. 

Sikuangalia nyuma wala kuiangalia simu nilikimbia kuelekea nilikolipaki gari langu na kuondoka spidi bila hata ya kuongea neno mpaka mbalizi kisha nikapaki gari pembeni kwa uoga na kutaka kukojoa mkojo ambao hakubahatika kutoka zaidi ya shuzi  za uoga ilizoambatana na tumbo kuunguruma ule muungurumo wa mtu aliyemeza magneziamu .

Nikaichukua simu na kuiangalia lakini missed call ilikuwa ni ya baba pachu, nikashikwa na hasira na nikakumbuka kuwa huyu ndio chanzo cha haya yote. 

Wakati natafakari nimpigie au lah,  mara meseji ikaingia kutoka kwa baba pachu akiniuliza nipo wapi wakati huo kwani kaja nyumbani na kunikosa na nyumba kaiona iko iko kama watu wamehama.

Sikujibu na kwahasira nikaifuta ile text maana nilihisi ingeweza kugeuka na kuwa janga tena kwani baba pachu namwogopa zaidi ya degue au ebola. Nikarudi kwenye gari na kuendelea na safari mpaka naingia nyumbani.

Kufika nyumbani pale getini alikuja kijana wa nyumba ya jirani na kuniambia kuwa ana barua yangu ambayo kuna dada mmoja aliileta na kumwambia anipe mimi tu asione mtu mwingine.

Nikajifanya kutabasamu kinafiki huku nikimwambia kijana asante na kutoa shilingi elfu mbili na kumkabidhi kama asante kisha nikaingia ndani. 

Nilipofika ndani nikakimbilia kila chumba kuhakikisha hakuna mtu na wala huyo binti hayupo ndani maana nilianza kuona sio binadamu wa kawaida.Na iweje aanze kunitumia vinoti na je nani kamwambia kuwa nakaa hapa na ofisi niifanyiayo kazi????

Nikamkumbuka baba pachu na kidogo nimpigie simu kwani hili janga sasa linaanza kuwa na kimkoa likikimbilia kuwa la kitaifa lakini kwa kiburi nikaona nitulie na kuifungua kile kinoti.

Nilifungua kile kinoti na kuona kuna namba zimeandikwa " 200802" wakati nikiendelea kutafakari kuwa hawa ni freemason au boko haramu mara sms ikaingia kutoka kwa mke wangu mama amigo ikiwa na namba 200802 akaniambia baba amigo mbona umenitumia namba hizo, je  ni pasiwedi za nini au namba za simu?

Niliruka na kukumbuka kuwa kwa bahati mbaya tachi skrini yangu ilikuwa imelowana na jasho na kujigusagusa jambo lililosababisha kuifoward ile meseji kwa bahati mbaya kwenda katika namba ya mama amigo.

 Nikampigia na kumwelekeza kuwa ni namba yangu ya tiketi ya bahati na sibu anitunzie lakini kichwani inikaanza kufikiri ni namba gani ya nini tena hii kwangu..

Nilianza kupekuwa katika masanduku na kila kona kujaribu kuikumbuka namba hii bila ya mafanikio na wazo la pili likawa ni kujaribu kila namba inayoishia na hivyo ili kujua nini kimo ndani hizo.

Moja kati ya namba hizo nilizojaribu ilipokelewa na ..........................................

Je namba hiyo ilipokelewa na nani na je ni nini mwanzo wa namba hii?

Usikose kisa hiki kesho jioni


Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu kwa udhamini wa Gracious HOUSE of CAKES watengenezaji maarufu na waliobobea wa keki za aina mbalimbali kwa hafla mbalimbali waliopo jijini Mbeya na wanapatikana kwa namba 0767218014

Nawe waweza kuwa kusoma  kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 

share, like na comment

You Might Also Like

0 comments: