Mme wangu alikufa na kufufuka baada ya siku ya tano ndani mwetu kisa utajiri
Harusi yetu ilisumbua mji ule na huwezi amini baada ya harusi nilifurahi sana na kujiona kama kila kitu kimekamilika katika maisha yangu na sikuwa na taabu tena, nasema yaani tena yaani umasikini kwishney.Mauza uza yalianza miezi miwili baadae mme wangu alipo niambia nimfungie kwenye moja wapo ya vyumba mle ndani na asiingie mtu yoyote hata mie kwa muda wa siku tano kisha niende kumfungulia muda kama niliomfungia.
Mie nikadhani utakuwa utani lakini alinisisitiza na kusema hatakiwi hata mtu ajue nipo, hivyo simu zikazimwa na kila aliyenipigia nikamwambia mme kasafiri kaenda nje ya TZ kufunga mzigo.
Sitaki kusema siku tano zile mle ndani niliishinde kwa wasiwasi na nikijiuliza maswali mengi kuwa ni nini kinaendelea mpaka pale nilipoenda kumfungulia baada ya siku ya tano na kukuta yupo na mifuko ya mahela ya kufa mtu.
Aisee unajua mtu nikaanza kupanic na kuhaha huku na kule nijue whats going on, si wajua tena maisha haya usije kujikuta mtu unafanywa ndodndocha bure.
Ni rafiki yangu mmoja ndiye aliyenizibua masikio na kuniambia kuwa jamaa anatumia utajiri wa mkataba hivyo zile siku tano mle chumbani hufa na akifufuka hurudi na noti za kufa mtu ndio siri kuu ya jamaa.
Na akasisitiza mke wake wa kwanza alikufa baada ya kutovumilia na kuamua kuingia aone kunani na baada ya kuona mauza uza kaanza kuumwa kichwa na baadae akafariki kabisa.
Jasho likaanza kunitoka na nikaona naanza kutompenda mme wangu, sikutaka kukurupuka ikanibidi nianze kufanya mishe za kwenda kusoma na baade nikajikuta nimebahatika kupata nafasi ya kuja hapa nje ya nchi kusoma na sasa nasoma Masters yangu ya masuala ya biashara.
Ila kurudi Bongo haipo maana nisije kuwa msukule bure na huku najua hawezi nifuta wanasema UCHAWI hauvuki bahari.
Usiiamini habari hii nilijichokea tu hapa nikaona niwatungie he he he ila mimi fuledi mjinga sana nawaza ujinga tuu
0 comments: