Mwanamke mjanja aliyewazidi kete wanaume wanne

10:00:00 Unknown 0 Comments

Marafiki wanne walikutana miaka 30 baada ya kumaliza chuo. Mmoja akaingia uani kujisaidia na kuwaacha wenzake wakijadiliana jinsi watoto wao walivyofanikiwa katika kazi zao.

Rafiki wa kwanza akaanza kwa kusema;"Mtoto wangu amesomea uchumi, na sasa anafanya kazi za kibenki na kampa rafiki yake wa kike gari aina ya ferrari kama zawadi ya birthday"

Rafiki wapili akadakia na kusema;" Kijana wangu yeye ni mfanya biashara na ni tajiri sana, wiki iliyopita kampa mpenzi wake nyumba ya kupangisha wafanyabiashara na pia kampa mtaji wa milioni 100 aanze biashra pia"

Rafiki watatu akasema,"Mtoto wangu ni injinia, na ana kampuni binafsi ya ujenzi, na juzi kampa zawadi mpenzi wake ya nyumba na gari jipya katika birthday yake."

Rafiki wa nne akawa anatoka uani na kuona kuna mjadala mzito akauliza, "mnajadili nini?"

Wakajibu tunajadili kuhusu mafanikio ya watoto waliyoyapata katika kazi zao, vipi wewe mwanao kafanikiwaje?

Akajibu,"Mtoto wangu ni changudoa na anajiuza ili apate fedha!"

marafiki wale watatu wakajibu,"Aibu gani hiiii!!! haujisikii vibaya kwa kuwa hajafanikiwa?!"

Akajibu,"Sina aibu yoyote kabisa yaani, anafanya vyema na mipango yake. kwani wiki iliyopita wakati wa birth day yake kanunuliwa gari aina ya ferrari, nyumba ya kupangisha wafanyabiashara, mtaji wa milioni 100 aanze biashara na pia kapewa nyumba na gari."

You Might Also Like

0 comments: