Nililazimiswa kuoa mchepuko na kumkosa mpenzi wangu

05:52:00 Unknown 0 Comments



Saa tisa ya mchana nikawa natoka natoka airport kuelekea nyumbani baada ya kuhakikisha kuwa Mariam kashapanda ndege akielekea ubelgiji ambako alikuwa anaenda kuanza masomo yake.

Nikawa katika dimwi zito la mawazo nikianza kujihisi jinsi nitakavyuokuwa mpweke baada ya mpenzi wangu mariam kuondoka nami nikiwaza namna ya maisha mapya.

Sio siri kwa mwaka mmoja ambao nimekuwa na mahusiano na mariam nimekuwa na amani na furaha na sasa nikawa na shauku ya kusubiri mwaka mmoja na nusu uishe aje tufunge ndoa tuu na tukae pamoja.

Pamoja na kuwa kila mtu alikaa kwake ila sikufua wala kupika wala kufanya lolote zaidi ya kudekezwa na hata nikiwa na maswahibu yangu yeye alikuwa karibu yangu kama mshauri mkuu.

Wanawema hata uwe mgumu vipi ila kuna siku utalainika ukimpata umendanye nami sikuwa na ubabe tena kwa mariam wangu.... Mungu amjalie masomo mema mke mtarajiwa.. nikajisemesha na kuwasha radio na kuanza kupata mziki laini.

Niliburudika na nyimbo zile alizoniachia mariam mpaka pale niliposimama mitaa ya Nyambono Resort bar ili niweze kupata bia moja ya kuimalizia wiki na kunipa kampani hasa baada ya mariam kuniacha.

Nilikutana na rafiki yangu na swahiba wa muda Suphiani na kuanza kupata bia kabla ya kundi la warembo fulani waliomfuta suphiani kuingia pale na kujumuika nasi.

Kuna binti mmoja katika wale warembo alinifanya nipoteze kumbukumbu na kuhamishia mawazo yangu yote kwake kwa jinsi alivyokuwa akinitazama na lile umbo lake kwa muda ule likaanza kunifanya nihisi kama vile pombe zinaanza kunichukua kwani kamwe nisingeweza fanya lolote kumsaliti mariam wangu.

Nikafikiria na kuona niachane na mawazo hayo na kuwa busy kumsoma fuledi huku nikichangia baadhi ya story za hapa na pale huvu vinywaji vikishuka. Kuna story moja ya fuledi eti alinunua vocha na kisha kutupa chini ganda la vocha na kuuondoka kisha siku ya pili akaja kuchukuliwa na polisi eti anahusika na mauji pale alipotupa vocha kuna mtu aliuawa jana yake.

Story ile ilinifanya niwe busy kuisoma na kupoteza usikuvu wa nini kilikuwa kinaendelea pale ndani huku nikianza kumwone huruma kijana wa kwenye story kabla ya kuja kugundua kumbe fuledi alikuwa akitusimulia ndoto  aliyokuwa akiota muda huo kanisani wakati ibada inaendelea.

Nilicheka kicheko ambacho kila mtu alishangaa pale na kisha wakajataka kujua na niipowasimulia wakawa nawafurahi lakini yule binti ambaye kwa muda huo nilisikia jina lake akiitwa Monica akasogea kwangu ili aione na kuisoma mwenyewe kwanianaifuatilia sana page hiyo.''

Tukaendelea na story na baada ya kukaa pale kwa muda tukaamua tungie mjini kwenda kuonana na baadhi ya marafiki kabla ya kuamka siku ya pili na kushangaa kuona Monica kalala upande wa pili na huku kukiwa na kila dalili ya kuwa tulichepuka usiku kwani tulikuwa pombe sana.

Nikaumia sana kwa kitendo kile na kuamua kutulia kwani nikajua nisingerudia tena na kusema kukosa mara moja sio mbaya. Tukajiandaa na kuondoka zetu nikamptisha kwake na kisha mimi kuendelea na mizunguko yangu ya hapa na pale.

Jioni akanipigia simu na kudai kuwa atakuja mara moja kuna mkoba wake aliusahau nikawa sina neno na lipokuja akaanza hadithi za hapa na pale na tukajikuta tunaamua kutoka kwenda kula na tukarudi wote.

mahusiano yakaendelea na mara kwa mara akawa analala kwangu au kuja kunisaidia kazi za pale nyumbani.Wakati huo mariam na mimi tukawa tunaendelea na mawasilino kama kawaida.

Mwaka mmoja na nusu uliisha nikiwa sasa nina mahusiano mazito na Monica na wakati huu nikaanza kuumia nitafanyaje maana Mariam naye ilibidi arudi kwani muda wake ulikuwa ukingoni na sikuwahi kumwambia Monica kuwa nina mchumba aliyeko masomoni nje ya nchi.

Nikiwa katika mawazo hayo nikapokea email kutoka kwa Mariam kuwa amepata kazi ya kufanya pale chuoni kwa meiezi saba kisha atarudi nami nianze maandalizi ya kwenda kujitambulisha kwao na kisha taratibu zote zianze mara arudipo.

Nikapumua kidogo na kuona sasa nitumie mwanya huo kumwambia monica kisha tuachane na mambo yangu na Mariam zianze kuchukua usukani. Nikamshirikisha Monica naye aliniuliza swali moja tu, "je kwa nini hukunishirikisha tangu mwanzo jambo hili?" Nikawa sina jinsi zaidi ya kukaa kimya.

Wiki tatu baadae nikaitwa nyumbani kwetu baba na mama wakaniambia kuwa tulipokea ujumbe wako kuwa unataka kwenda kutoa posa kwa kina Monica... Sasa ulifkiri iwe lini? Nikawa na shangaa habari hizo zimefikaje?

Kumbe monica aliandika barua na kujifanya mimi na mbaya zaidi hata wazazi wake alishawaambia, nikawa sina cha kufanya nikaondoka mpaka mjini. Kufika kule nina hasira nataka kumpiga Monica naona ananipa karatasi kumbe ana mimba ya miezi miwili kasoro.

Hasira zikaniisha kwani sasa nikaona nimechanganya mambo na ndio ndoa yangu ikapata mwanya huo na ile ndoto ya kuwa na mariam ikaishia. Mariam aliporudi na kusimuliwa hali yake ilitetereka kiasi na kurudi kuwa safi na kuendelea na maisha yake.

Mbaya zaidi ni kuwa ameapa kuwa lazima atanifanyia kitu mbaya... na kutokana na hofu hiyo nimejikuta muda wote nashinda nyumbani zaidi kuhofia kufanyiwa hiyo kitu mbaya.

Kila msaliti hukutana na mjanja wake... 




,

You Might Also Like

0 comments: