Sababu za wanaume kuwa na michepuko

05:50:00 Unknown 0 Comments




Ingawa wanaume karibia wote wanajua kwamba kuchepuka  ni makosa lakini wengi wamekuwa wakiendelea kuwa navimichepuko vingi bila kujali ni mchepuko wa vumbi au lami.

Mojawapo ya sababu ambazo wanaume wengi hutokea kutembea nje ya ndoa au kuchepuka kabisa pembeni kwa mujibu wa wanoko wa mapenzi duniani ni kama zifuatazo:

1: Mboga Mpya: Wanaume wengi huchoka kula nyama kila siku usiku badala yake hutaka kujaribu mboga mboga nazo zinakuwaje, hii ndio sababu wanaume huwa hawajali mwanamke wanayetembea nae nje ya ndoa hata kama akiwa hana mvuto hata kidogo.

2.Sio Kama zamani: Kama mwanaume ataona mpenzi wake hayuko kama zamani kwa mfano hajijali tena, amenenepa sana siku hizi, hapendi tena mambo ya mapenzi n.k sababu kama hii hupelekea wanaume wengi kutengeneza kibanda nje.

3: Mapenzi: Kama mwanaume anaona mwanamke wake anashindwa tena kumtosheleza kimapenzi au anashindwa kujaribu mambo mapya katika mapenzi, basi mwanaume huyo hutoka nje ya ndoa kujaribu kutafuta mambo mapya katika mapenzi mapya ambayo mke wake hawezi kumfanyia.

4: Kisasi: Mwanaume wakati mwingine huamua kutoka nje ya ndoa kama njia ya kupunguza machungu ya hisia zake baada ya kugundua mke au mpenzi wake anatoka nje ya ndoa.

5.Nafasi: Kwakuwa ni mara chache sana wanaume kutamkiwa mambo ya mapenzi na wanawake, wanaume wengi huwa ni vigumu kuiachia nafasi pale mwanamke mwingine anapoonyesha mapenzi na kuwa tayari kwaajili yake. "Bahati imejileta yenyewe kwanini kuilazia damu".

6.Mabishano: Kama kwenye nyumba migogoro haiishi kila siku, wanaume wengi hutafuta nyumba ndogo pembeni ili kupata sehemu ya kujilawaza na kuondoa stress zao.

7. Mapenzi kupungua: Wakati mwingine wanaume huona mapenzi katika ndoa yamepungua na huamua kubakia kwenye ndoa kwasababu ya watoto au sababu za kiuchumi, kwa maana hiyo huamua kutafuta mapenzi zaidi nje.

8. Msamaha: Kama mwanamke atamkamata ugoni mwanaume wake mara nyingi sana na mara zote akamsamehe, basi kuna uwezekano mkubwa wa mwanaume kuendelea kutoka nje kwa kuwa atajua msamaha utakuwepo tu.

You Might Also Like

0 comments: