Siku mwanaharakati wa wanyama alipozimia

10:47:00 Unknown 0 Comments




Jamaa alikuwa anafuga nguruwe, siku moja akatembelewa na wanaharakati wa Haki za wanyama;

MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
MFUGAJI: Nawalisha mabaki ya chakula toka migahawa mbalimbali
MWANAHARAKATI: Hayo ni makosa unawatesa wanyama kwa kuwalisha chakula kichafu. Akapigwa faini... Baada ya siku chache wakaja wanaharakati toka Umoja wa Mataifa
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?

MFUGAJI: Huwa nawaanzia siku na uji wa ulezi, halafu mikate, mchana ugali kwa kabeji na usiku viazi

MWANAHARAKATI: Loh watu wanakufa kwa njaa wewe unalisha nguruwe, akapigwa faini....siku chache baadae wakaja wanaharakati wa Mazingira

MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?

MFUGAJI: (Kwanza akasita kidogo) Hawa huwa nawapa shilingi alfu tano kila mmoja kila siku halafu wao wenyewe wanaenda kununua chakula wanachokitaka

You Might Also Like

0 comments: