Siku wachumba zangu walipoandamana na kulipa kisasi.....

20:05:00 Unknown 0 Comments

Nilijiinamia huku nikifikiria kwa zaidi ya dakika kumi bila kupata jibu sahihi.

Nikajisemesha, " yaani pamoja na ujanja wangu leo hii mwanamke mmoja tuu ananizidi nguvu na kunifanya niwe mtumwa wa nyumba yangu???"

Kwangu ilikuwa ni zaidi ya dharau na kama haitoshi nikaanza kuona picha ya jinsi habari ya mimi kutandikwa na binti yule ambavyo ingeenea zaidi ya kawaida.

Nikiwa na endelea kuwaza hilo alipita dada mmoja ambaye ni jirani yetu mtaa wa pili. Kuniona tu akaanza kuachia kicheko na kusema, "

kazi unayo dan, salome kawaita na wale mabinti wenzake wamekaa pale kwako na wanadai hawataondoka labda ukimbie au kujiua."

Nilianza kumchukia yule dada lakini baada ya kuniambia hayo nikaona sasa kuna jambo linaenda kitendeka tena kubwa.

Nikaingiza mikono mfukoni na kugundua kuwa simu moja niliisahau nyumbani kutokana na purukushani na kuichukua moja ambayo haina majina ya kutosha.

Lengo lilikuwa nipige simu nyumbani na kupata yanayojiri huko na kujua nini cha kufanya.

Sikuwa na jinsi nikamwomba yule dada aende pale nyumbani na kupeleleza nini kinaendelea ili aje anipe habari za nyumbani.

Haikupita dakika chache akaja yule dada na kuniambia kuwa pale nyumbani kuna wadada wanne wamekaaa kwa shari wakinisubiri na wanaongea kuwa hawaondoki na simu ameona dada mmoja kaishika.

Sikutaka hata kuuliza zaidi nikaanza kukimbia kuelekea mjini kwa jamaa yangu ili niweze tafuta msaada, wakati naanza kuondoka simu ikaita ma rafiki yangu aitwaje jim akaniambia kuwa kafika home ameona hapafai niko wapi..... Nikamwambia nilipo na akaja.

Alipofika pale akaniambia kuwa hali ni tete mabinti wametoa kila kitu changu nje wameweka juu ya gari langu na wanataka kuchoma.

Hapo sasa nikajikuta nasema kwa sauti " NOOO NOOOO" kwani nikaona sasa gari langu litaishia hapo na halijamaliza hata mwaka tuu yangu niliagize.

Jimi akasema, " ila Dan nilikuambia mtindo wa kucheza na hisia za mabinti na kuwatupa baada ya mahaba ya mbwembwe yenye ahadi kemkem za maisha vitakutokea puani.......... Nadhani umeona sana"

Hebu angalia jinsi Mayasa alivyokuharibu kichwa chako kwa kipande cha tofali na kama haitoshi pale nyumbani yupo mayasa, mary, liz na adela na wakati naondoka nimesikia wanaongea na mtu kwenye simu yako pia nafikiri kuna binti mwingine anaitwa.. Aliongeza jim na kunifanya nianze kutokwa na machozi.

Kabla ya kuanza chuo nilikuwa na mpenzi aitwaye mary mbaye tulikubaliana kuja kuoana na nilazaa nae na kimfanya yeye achelewe mwaka mmoja kwenda chuo.

Nikiwa chuo mwaka wa kwanza nilikuwa na mayasa na kuwa na mahusiano yaliyodumu kwa muda wote wa chuo na akajifungua mtoto tukiwa mwaka wa mwisho.

Wakati huo nilikutana kwa bahati mbaya na liz aliyekuwa akisoma chuo jirani na siku moja tukiwa club pombe zikatuzidia na kulala nae na wiki chache baadae akawa mjamzito na kugoma kutoa mimba.

Adela yeye nilifahamiana nae kupitia facebook na tumekuwa na mahusiano naye kwa kitambo sasa na wiki chache zilizopita nilienda kujitambulisha kwao kwani huyu nilitaka kufunga naye harusi na wote wanajua na nimjamzito.

Mayasa baada ya kugundua tena siku moja baada ya kuja kwa kushtukiza mkoa ambao nilipelekwa kikazi akafuma kwenye simu yangu picha za watoto na mama zao na kwa bahati mbaya akamtamba adela na tumbo lake kumbe wao ni ndugu.

Wakatafutana wote na kuanza sasa kupanga jinsi ya kunijeruhi kwa siri bila ya mimi kutambua nini kitatokea.

Leo nikiwa home nikapokea sms kuwa nisiondoke anataka kuniona ila nikiwa nimekaa chumbani nikawaona wakiwa wanakuja na wazo la haraka likanijia nikimbie.

Wakati najaribu kukimbi adela pamoja na tumbo lake akanisukuma nikaanguala na kukutana na vibao kama vinne vya mayasa na wakati nataka kusimama ili niweze kijizatiti walinishambulia na kufanikiwa kuwakimbia ingawa nikasindikizwa na kipande cha tofali.

Kelele zikanigutusha katika mawazo haya na jim "akaniita twende kaka si wasikia kelele hizo na moshi ule?"

Mbele ya gari kuchomwa wakati huu hata sikuhofia tofali nilikimbia kuelekea usawa wa nyumbani na kushuhudia wakichoma nguo zangu na vitu vyangu vya thami wamevichukua pamoja na kadi ya gari kuwa wanaenda kuviuza ili wapate fedha za matunzo ya watoto.

Nikaingia chumbani kuona jinsi walivyoharibu na kuchukua vitu mpaka kadi ya benki nikaishiwa nguvu na maumivi ya kichwa kutokan na kile kipande cha tofali yakazidi na nikaanguka chini kabla ya kugundua muda huu kuwa na hii ni ndoto ya asubuhi hii.

Mmmh mayasa jeuri

Kama umeelewa wewe share na comment

You Might Also Like

0 comments: