Ukiona dalili hizi huhitaji kupigiwa kengele,jua umri umeenda.
Ukiona dalili hizi huhitaji kupigiwa kengele,jua umri umeenda.----------------------------------------------------------------------
1. Huna muda wa kushinda na mpenzi wako kutwa nzima mkipiga stori za mapenzi
2. Ukihitaji kufanya mapenzi mahali unakokufikiria ni kitandani
3. Unaanza kujaza friji lako kwa vyakula zaidi kuliko pombe
4. Muziki unaoupenda unausikia ukiwa kwenye lifti ama kwenye gari lako ukienda na kutoka kazini
5. Saa 11 alfajiri ndiyo muda unaoamka, na siyo muda tena unaorudi kulala
6. Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa
7. Rafiki zako wanakualika zaidi kwenye vikao vya harusi kuliko mtoko wa kwenda Maisha Club
8. Ukienda dukani kununua kitu unakuwa na juhudi sana ya kuomba upunguziwe bei
9. Idadi ya tisheti na jinsi inapungua kwa kasi kwenye kabati lako la nguo
10.Wewe ndiyo unayekumbuka kuwapigia simu polisi endapo mtaani kwenu kuna vijana wavuta bangi wanaowasumbua
11. Hukumbuki tena Azam Ice Cream na Samaki Samaki wanafunga saa ngapi
12. Ukiwa nyumbani unaanza kutumia muda wako wa ziada kulima lima bustani ya maua ama mbogamboga badala ya kuzikomoa movie na kuzurura
13. Kila kitu kikinunuliwa nyumbani jambo la kwanza unalouliza, "Umenunua sh' ngapi?"
14. Unakwenda duka la madawa kununua Ibuprofen na Antacid, siyo kondomu tena wala kipima mimba
15. Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi, The Express, Citizen na Nipashe badala ya Uwazi, Ijumaa, Kiu na Amani
16. Asilimia 90 ya muda unaoutumia kwenye kompyuta yako unautumia kufanya kazi badala ya kuchat
17. Ukimwona rafiki yako yu mjamzito unampongeza sana badala ya kumwuliza, "imekuwaje tena?"
18. Ukienda kutembea mahali huishi kuulizia bei za viwanja
Loooool...shtuka!!
0 comments: