Njia kuu tatu za kugundua kuwa unayechati naye ni mwongo
1. Anapicha sio zaidi ya mbili au moja za kushare kwenye profile au timeline yake
Pamoja
na kuwa sio vizuri sana kila mtu kuweka picha zake hapa mtandaoni
lakini watu waongo wao huwa na picha chache au hata kutokuwa nazo kabisa
ili kuzuia kuonekena au kufahamika na hata ukijaribu kumwomba bado
ataonyesha kusitasita na wengine hukupa picha zisizo zao.
Ni
vizuri sana kama ukajaribu kumwomba akutumie picha laiyopiga kashika
karatasi lililoandikwa jina lako angalau kufahamu ni nani unachati naye.
2.Kutokana na maelezo yake atakuambia anakaa jirani sana na wewe ila atakwepa sana kukuona
Siku
hizi hakuna mtu anayefanya kazi masaa 24 kwa siku 7 mfululizo bila kuwa
na muda wa kupumzika hivyo ukigundua analeta sababu za ubize mara kwa
mara basi wewe jua hapo kuna jambo.
3. Ana maongezi mazuri yanayotaka kuendana na ukweli
Kila
mtu ambaye ameumizwa na watu wa hapa online wengi wao huonyesha
walikuwa wakichati na watu waliokuwa wazuri sana kwao na familia zao
hivyo ni vyema kuwa waangalifu mapema.
0 comments: