Umasikini sio sababu ya kuwa mchafu wala utajiri Sio kuwa na kila kitu hata kama hukihitaji
Umasikini sio sababu ya kuwa mchafu wala utajiri Sio kuwa na kila kitu hata kama hukihitaji. Hebu angalia hapo nyumbani kwako!
Vitu msivyovihitaji Leo wala kesho
mmeweka vya nini? Umenunua makochi
mapya Yale ya zamani mmegawana vyumbani
mnaishia kurundika minguo hapo na kufuga
mipanya, godoro umenunua jipya la zamani
umeviringisha juu ya kabati, kabatini kwako
kuna nguo ulivaa ukiwaona secondary mpk
Leo unazo eti ukumbusho au utazivaa
ukipungua, jikoni ndo shida iliposhika
hatamu !!
Mivyombo ya plastiki imepaukiana
imeyayuka na moto ipo tu eti vyombo vya
watoto,mahotpot yamekata roho imebaki kuwa
sufuria we unalo tuu, ndoo hata hazitumiki
zipozipo tu hata maua hazifai kupandia we
unazogo tu huchomi,hutupi wala huzihitaji,
vyombo vya udongo fina mapengo na magego
km vinang'atwaga na kila kimoja na dizaini
yake havifanani coz set imeshavunjikavunjika
hivo ndo vimebaki,Dressingtable imejaa
mikopo na mibox haina Kazi,perfume ya
mwaka 2000 unayo hapo kisa ukumbusho wa
zawadi,stoo yenu wenyewe ila mwaiogopa
kuingia coz imejaa vitu visivyohitajika imekuwa
ghetto la panya badala Ukiweka mnavyohitaji,
nje ya nyumba kuna gari la urithi la babu
lipogo tu hapo linafuga ndege,kutupa vitu
visivyohitajika hamtupi eti Dhambi na kugawa
hamgani coz mmeviharibu hadi mwisho
mtampa nani?
Kutwa mnapishana
mahospiitalini mnaumwa flu na vifua kila
siku,kimoja Kwann msiumwe na mnakaa
dampo ?
Hivi mnajua km huu ni ugonjwa?
Unaitwa hoarder disorder. Tena
mnawaambukiza wanenu as wanajua kwao
hata kikopo cha icecream hakitupwagi
kinaoshwa kinawekwa hapo. Halafu bado
unaendelea kumuomba Mungu akupe, akupe
uweke wapi na kwako pameshajaa?
Credit: Joseph Mwaisango
0 comments: