Akaa na mke kwa miaka saba bila kujaliwa mtoto na hajachepuka

04:05:00 Unknown 0 Comments

Salome alibahatika kuzaliwa katika familia ya watoto wanne ambao kati ya hao watoto wanne kulikuwa na kijana mmoja tu wakiume aliatwaye Dan.

Watoto wote watatu wakike waliolewa na kwenda kuishi na waume zao wakimwacha dan akiwa anaishi na mama yao kwani bado alikuwa akiendelea na masomo yao.

Mama yao aliwakuza watoto hao baada ya baba yao kufariki wakiwa na umri mdogo na kwa kuwa baba alikuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa basi maisha hayakuwa magumu kwao.

Maisha ya familia hii yaliendelea kuwa mazuri hata baada ya watoto wa kike kuolewa na familia zinazojiweza na kuishi kwa kufuata ndoto zao.

Mambo yakaanza kuwa magumu kwa binti wa wa pili ambaye alikuwa kakaa katika ndoa yake kwa miaka miwili bila dalili za kuleta matumaini kuwa angepata ujauzito.

Kutokana na hali hiyo kukawa hakuna amani tena katika familia yake hali ambayo ikawa inabadilila kila siku kutoka hatua moja nafuu kwenda mbaya zaidi.

Akiwa ameripoti hali hiyo ya huzuni kwa mama yake na ni zaidi ya mwaka mmoja sasa umepita nakufanya kuwa miaka mitatu bila ufumbuzi dada yake akafungiwa virago na mme wake kurudishwa kwa mama kwani naye alikaa miaka mitano bila kupata mtoto.

Ni dada yao mkubwa tu ambaye mme wake aliendelea kumpenda na kumvumilia pamoja na kukaa miaka saba ya ndoa bila ya kuwa na dalili za kupata mtoto.

Wakati huu mdogo wao yule wa kiume aitwaye dan akawa kila akitaka kuchumbia pale kijijini kwao mabinti wanakataa katakata na kusema familia yao haizalishi na kila baba na mama kuwaonya watoto wao wa kike kuolewa na dan.

Familia hii ya mama salome ikawa katika wakati mgumu na kila mmoja kwa imani yake wakaanza kutafuta suluhu na kote walikoenda wakaambiwa kuwa mama yao anaijua siri ya hali zao.

Mama yeye akawa hajui chochote zaidi ya kulia usiku kucha akimwomba Mungu aisaidie familia yake kurejesha furaha yao watoto wake wa kike warudi kwenye ndoa zao na wapate watoto na dan apate mchumba pia.

Siku moja baaada ya maombi salome alioteshwa kuwa yeye na mama yake walifanya kosa na kosa hilo litaiandama familia yao na kamwe haitopata furaha na amani.

Akamsimulia mama yake na kwa pamoja hawakuweza kukumbuka na ikawabidi wawashirikishe wenzao bila ya kupata ufumbuzi pia.

Familia nzima ikaanza kufunga kwa maombi huku wakiomba kugundua nini kimeikumba familia yao na mfungo ule wa siku saba ulivyoisha kila mmoja alikuwa ameoteshwa ndoto.

Jambo la kushangaza ni kwamba wote waliota ndoto iliyomhusisha mtu moja katika matukio tofauti sana.
Dada wa kwanza yeye aliota kuwa alikutana na dada mmoja mfanyakazi wa ndani wa nyumba moja ambayo alihisi kuifahamu akiwa nje ya nyumba analia na kila alipomsogelea amsaidie dada yule alipotea.

Dada wa pili yeye aliota kuwa alimwona dada mmoja ambaye alionyesha kuwa ni mfanyakazi wa jumba moja la kifahari akiwa anasafisha vyombo ila kila akitakatisha vionyesha kupakwa damu.

Salome yeye akaota  kuwa alikuwa anakimbizwa na dada mmoja ambaye alikuwa kashika panga na anajaribu kumkata bila mafanikio.

Dan yeye akaota kuwa alikuwa amekaa sehemu na kuna dada akawa analia akiomba msaada na kila alipojaribu kumsaidia dada yule kuna mama alitokea na kukataza dan na dan akaishia kushindwa kutoa msaada.

Mama yeye aliota aliluwa gizani kazungukwa na nyoka wa nne wakubwa  waliokuwa wakinyemelea kuwauma watoto wanne aliokuwa nao na kuna dada mmoja akawa kashika silaha kubwa ila akiangalia tu bila kutoa msaada na kuishia kulia.

Ni wakati huu mama akaanza kulia kwa sauti kubwa kwani kutokana na ndoto hizo akakumbuka kuwa wakati watoto wale wakiwa wadogo aliwahi kuwa na msichana wa kazi.

Siku moja binti yule alikuwa akifanya usafi bafuni na mama hakupendezewa na usafi ule akamchapa binti wa kazi na kuchukua sabuni ya kufanyia usafi chooni na kumywesha yule dada.

Dada akaanza kuumwa siku ya pili na kwa uoga akashindwa kumwambia mama na badala yake baada ya kuzidiwa akakimbia na siku nne baadae alikutwa kafia katika kichaka kimoja huku baadhi ya sehemu zake za mwili zikiwa zimeliwa na mbwa.

Binti yule ambaye alikuwa ni wapekee katika familia moja maskini sana alililiwa sana na mama yake ambaye naye alifariki wiki moja baadae kwa shinikizo la damu.

Baada ya kisa hiki familia nzima waliishia kulia huku wakimwomba Mungu awasamehe kwa madhambi ya mama yao na miaka minne baadae watoto wa kike walifanikiwa kupata watoto na dan kuoa ingawa mama yao alifariki mwaka mmoja baadae.

Mungu atupe hekima na busara kwa kita tukifanyacho sasa ili tusije jutia kesho.AMEN

You Might Also Like

0 comments: