WIVU USIGEUKE KUWA SHUTUMA!!

06:51:00 Unknown 0 Comments



Hutokea kwa jinsia zote mbili ya mke na mume pale mmoja anapoona mwenza wake ametenda kilichomtiya ndani ya wivu mmoja basi panapo mapenzi ya kweli lazima kufumbua midomo yake na kuuliza pa kuuliza au kukanya pa kukanya.
Mwenzangu mbona umemtizama yule kwa JICHO la kunitazama mimi!?
Mwenzangu mbona ile WELCOME au AHSANTE haikuwa katika hali ya kupewa yule!?
Mwenzangu mbona picha hii haikustahiki kuonekana na mwengine zaidi yangu!?

Maswali kama hayo hapo juu na mfano wake ni sehemu ya wivu kwa mwenye kupenda kweli na si vyema kwa mmoja kuyageuza kuwa shutuma ndani yenu. Na huleta athari kubwa sana iwapo yatazoeleka mapenzini. Athari kubwa ya hili ataigundua mwenye kuyabeza kati yenu na akawa mwenye kumjibu mwenza wake kinyume na matarajio yake. Kwani kila ninamtazama ndio namtaka mie alaa!??
Acha upuuzi wako wewe nikimwambia AHSANTE au KARIBU wewe ushafika mbali acha zako mwanamke wewe!!
Unapenda kunifikiria mabaya mie tu kila siku.. kwani kuweka picha hapo ndio maana najiuza au malaya mie??

Tujiulize kuna ubaya gani utapomjibu mwenza wako jibu la kujiona umethamini kukuonea wivu kwake ( mfano.. Honey hii picha ni kwa ajili yako tu na sikua na maana zaidi ya kuona wafurahi mpenzi wangu) ambayo ni sehemu ya mapenzi na sio kuichukuwa kama shutuma toka kwake!!
Na utakuja kumlaumu nani utapofika pahala akaogopa kukionesha kilichomtia wivu na kusababisha wewe kuhisi hana wivu kwako na ukaamini mapenzi pia hayapo!?

Tuzingatie saana tunapopokea yaliowapa wivu wapenzi wetu na katu tusiyachukulie kama SHUTUMA, kwani kuyajenga kama shutuma yatakuja kutuathiri wenyewe tunaodhani twashutumiwa kumbe mapenzi ya kweli ndani ya vitendo.

You Might Also Like

0 comments: