Hii ndiyo tofauti ya mvulana na msichana kwenye mahusiano ya kimapenzi
Kila kunakokucha watu wanalalama kuwa siku hizi mapenzi hayan maana but ni kwa sababu wameshau kuwa kati ya mwanaume ( mvulana ) na mwanamke ( msichana) wanatofauti kubwa kati yao, tofauti hizo ni kama zifuatavyo
1. Mvulana anapomwona msichana kwa mara ya kwanza anamtamani na kumtathmini kama kweli anaweza kumfaa kwa matamanio yake mfano je ni mrembo, akitoka naye out atauza, je anamajivuno ama yupo kawaida, WAKATI msichana anapomuona mvulana kwa mara ya kwanza anamjaji kwa muonekano wake, mfano je huyu ana pesa, ana usafiri ama anafanya kazi ya maana au ndo hivyo tena SASA mara nyingi wengi hukosea hapo na kuwawekea aidha positive ama negative attitude kisa alivyo vaa.
2. Mvulana akiona msichana amemtamani kwa kiwango cha juu basi kinachofuata atamweleza kile anachohitaji wakati Msichana yeye atasikiliza kile mvulana atakachozungumza kwa kuzingatia vigezo alivyoviona aidha handsome ama tajiri anazitaka hela zake.
3. kwa kuwa wavulana huona kwa macho na kupeleka akilini ( ANA ANGALI, ANAMTAMANI, THEN ANAFIKIRIA ITAMCOST KIASI GANI KUMPATA YULE MREMBO) maana yake hilo jambo haliendi moja kwa moja moyoni bali ni kichwani WAKATI msichana yeye atasikia kile anachoambiwa then maneno kama ni matamu basi yataenda moja kwa moja moyoni bila kufikiria kwa umakini kwanini huyu mtu kaniambia ananipenda, ndo hapo atakapoanza kufikiria atakuwa too late
4. mvulana inamchukua muda mrefu kumpenda msichana ki ukweli ukweli wakati msichana inamchukua muda mfupi kumwamini mvulana kulinana na mwonekano wake.
5. Mvulana anapoumizwa huwa ni baada ya kukaa muda mrefu na msichana na kumwamini lakini anapoinvest love for Real anajikuta yupo kwenye dimbwi la tapeli wa mapenzi ila Msichana humchukua muda mfupi kuumizwa kwa sababu hakumchunguza sana mpenzi wake na alimwamini kwa kusikia kile anachosema mdomoni bila kujua kilichomo moyoni mwake, na anapogundua ndipo matatizo yanpoaanzia hapo.
ALL IN ALL TUNAPASWA KUHESHIMU MAHUSIANO YETU
0 comments: