Kina dada someni hapa

12:59:00 Unknown 0 Comments



* Kamwe usiutumie ujana wako kwa kujichora picha itakayokuja kukudhalilisha maishani mwako..... Jaribu kuwa na tabia njema ya mavazi na jinsi ulivyo kwani hiyo ndio itakupa mme unayeendana nae na familia yako kitaakisi jinsi wewe ulivyoishi ujana wako.

* Kutembea nusu uchi sio ndoano ya kuwapata wanaume. Utachezewa na mwisho wa siku kila mwanaume anamtaka mwanamke mwenye tabia njema ya mwili, roho na moyo wake..


* Kila ukifanyacho hapa mtandaoni sasa kumbuka hakitafutika miaka nenda rudi na itafikia kipindi wanao watajionea jinsi mama yao alivyokuwa akiishi miaka hiyo.


Kumbuka

Mwanaume atakayekupenda ukiwa nusu uchi jua anakutamani na hana lolote jipya zaidi ya kukutumia na kukuacha hivyo badilika

Mwanaume akikusisitiza kuvaa mavazi ya chumbani mkiwa mbele za watu jua hana mapenzi ya dhati.... hebu jaribu kumwambia yeye atembee na boxer uone kama utasalimika.

Jiheshimu na kuuthamini mwili wako kwani ndio baraka uliyopewa na Mungu kwani hata chocolate ikifunguliwa na kukaa wazi kwa muda mrefu upoteza ladha na kuwa haifai tena.

You Might Also Like

0 comments: