Maswali ambayo utayasikia tena na tena maishani
•Mdada anaingia kwenye daladala na viatu vimechongoka anakukanyaga, halafu anakuuliza ‘Samahani umeumia?’•Kwenye msiba utakuta watu wanalia,’Kwanini kafa yeye? Jamani kwanini kafa yeye?
•Mtu anaingia kwenye mgahawa halafu anamuuliza weita,’Biriani yenu nzuri?’
•Shangazi yako ambaye hamjaonana siku nyingi lazima atatoa, ‘He jamani umekuwa mkubwa’
•Binti akiwaeleza ndugu zake kapata mchumba wa kumuoa lazima ndugu moja atauliza,’Mtu mwenyewe mzuri?
•Ukipigiwa simu saa 7 ya usiku tegemea swali,’Vipi nimekuamsha?’
•Madaktari wa meno wakati wanakuchokonoa meno na vyuma vyao utasikia,’Nambie kama unaumia’
•Umekaa unaburudika na sigara yako anatokea fala anakuuliza,’Kwa hiyo siku hizi unavuta?
0 comments: