Ukimjulia mwanamke hawezi kukutesa, kukuliza, kukusumbua...
Baadhi ya wanaume wanashindwa kuelewana
na wanawake zao kwa sababu tu hawajawajua
walivyo. Rafiki zangu, wanawake
wanatofautiana, lakini si kwa kiasi kikubwa;
tabia zao nyingi zinafanana.
Kikubwa ni kuwajua walivyo, basi hapo kazi
inakuwa imeisha. Wengine wanaachana na
wapenzi wao huku wanawapenda, baadaye
wanakuja kujutia, kisa hawakuwajulia. Kwa nini
mwanamke akutese? Akulize? Akusumbue
kichwa hadi kipasuke? Hakuna sababu.
Sasa hapa katika All About Love, nitaanza kwa
kukupa siri za ambazo huzijui kuhusu
wanawake. Ukweli ni kwamba, katika uhusiano,
kuna mambo ambayo wanawake huyafanya siri
au huogopa kuyasema, lakini yakawa
yanawaumiza kwa kiwango kikubwa na huenda
baadaye yakaharibu uhusiano wenu.
Hebu twende katika hizo sindano tuweze
kung’amua pumba na nafaka.
KUHUSU UAMINIFU
Katika Saikolojia ya uhusiano suala la uaminifu
ndiyo nguzo ya muhimu. Mwanamke anapenda
uwe mwaminifu kwake katika kiwango cha
mwisho, hataki kuwa na mashaka na wewe
katika kila unachokifanya. Anatamani kuwa
salama hata utakapokuwa mbali naye kwa
sababu za kikazi au mambo mengine.
Ili uaminifu huu ambao mwanamke anauhitaji
kwako uwepo, lazima uwe na penzi la dhati
kwake, uwe huna mwanamke mwingine nje.
Kwa maana hiyo, wakati mwingine mpenzi wako
atakuwa huru na simu yako.
Wengine wanakuwa wakali sana na simu zao.
Kuna nini cha siri kimefichwa kwenye simu?
Kama ni kweli unampenda na upo huru kwake,
huwezi kumzuia kuishika simu yako. Kumbuka
wanawake wengi ni dhaifu, huwa hawapo tayari
kumpoteza mwanaume wake kwa vitu vidogo
lakini ukweli ni kwamba hubaki na siri ya
maumivu moyoni mwake, lakini si ajabu akawa
anawaza kupata mwanaume mwingine ambaye
atamponya madonda ya moyo wake.
‘KILA KITU SAWA’
Wanawake walio wengi, linapokuja suala la
kukosea jambo fulani, huwa hawapendi kuwa
wasemaji sana. Wakati mwingine atakuwa
tayari kutumia lugha za ishara ili uelewe
anachokitaka, usipong’amua ananyamza!
Anaweza kujifanya anaridhika na kila kitu,
kumbe ndani ananung’unika. Mbaya zaidi, hata
mnapokuwa faragha, inawezekana hukufika
anapotaka, lakini hawezi kukuambia, lugha ya
ishara itatumika, ukishindwa kuelewa
atakuacha, lakini moyoni ana maumivu.
Pamoja na kwamba anakupenda, atalazimika
kutafuta mwanaume mwingine ambaye
anaweza kumpa raha! Hapo utabaki na
maumivu. Fumbuka rafiki yangu, msome
mwanamke wako ujue anachokitaka.
HATAKI SIRI
Mwanamke anapenda uhuru, anapenda
kujisikia wazi mahali popote. Hujisikia vibaya
anapokuwa hana uhuru hata wa kumshika
mkono mpenzi wako wanapokuwa barabarani.
Anapenda penzi la uwazi!
Maana mwingine utakuta akikutana na rafiki
yake, badala ya kumtambulisha vizuri kama
mpenzi wake, anaanza kupatwa na kigugumizi.
Ataishia kusema ni rafiki yake
sana...amemaliza! Hayo si mapenzi. Kwa nini
unaficha?
Hukosa amani kabisa akifanyiwa hivi, lakini
hatasema, atabaki na maumivu akiendelea
kufikiria utatuzi, ambao kwa hakika huwa ni
kutafuta mwanaume mwingine. Vipi hapo, si
utabaki na maumivu mzee?!
UNAJALI?
Rafiki yangu, mwanamke anapenda awe pekee
kwako, umsikilize, umjali na umpe kipaumbele
katika kila unalolifanya. Wanawake wengi
wanapenda kudekezwa, lakini hawapendi
kuweka hilo wazi kwa mwanaume.
Wakati mwingine anaweza kukupa mitihani ili
kupima kiwango cha penzi lako. Anaweza
kukuambia anaumwa au anauguliwa na mtu
wake wa karibu, lengo ni kuangalia ni jinsi gani
unakuwa makini anapokuwa na matatizo. Vile
utakavyochukulia tatizo lake kwa ukaribu,
uchungu na kuona kama lako, ndivyo
utakavyomfanya aone thamani la penzi lako
kwake, ikiwa vingenevyo basi humuacha na
machungu moyoni, huku akijutia kuwa na
mpenzi wa aina yako.
KATAA MAUMIVU
Siku zote, unatakiwa kuwa mshindi kwa
mwanamke wako. Jifunze kusoma hisia zake,
kabla ya kufanya kitu, fikiria mara mbili, lakini
baada ya kufanya, msome kupitia uso wake.
Analifurahia au umemchukiza?
Ni vizuri kugundua hilo ili uweze kufunga hisia
za kumfanya aanze kufikiria kukusaliti. Hata
mnapokuwa faragha ni vizuri kuwa makini na
kila unachokifanya! Chunguza kama anafurahia
penzi lako na manjonjo yote unayomfanyia.
Kumbuka kwamba ni vigumu sana mwanamke
kukueleza moja kwa moja kwamba
hujamfurahisha au kuna kitu umekikosea, hii
husababishwa na hofu ya kuogopa kukufanya
ujisikie vibaya.
0 comments: