Binti aokolewa akitaka kujirusha kutoka ghorofani kisa usaliti wa mapenzi
"Kaka umependeza sana na naomba Mungu akutangulie katika tukio hili na hakika maisha yako yawe ya furaha kubwa"
Haya yalikuwa ni maneno ya mwisho yenye nguvu kutoka kwa rafiki aliyekuwa akunisifia pale salon kuwa nimependeza wakati wa maandalizi ya harusi.
Dakika chache baadae alikuja sasha rafiki wa mke wangu mtarajiwa na kunivuta nje nilihofia zaidi kwa kuwa uso wake ulionesha dalili zote za hofu.
"Shem mpaka sasa nashindwa sijui nianzie wapi kwani tangu jana vivian hataki kabisa kutoka nje na leo kagoma kabisa kwenda salon wala kujiandaa na muda huu hayupo nyumbani.
Baada ya kumtafuta na kumsubiri nikaona nije kwako nyumbani labda atakuwepo lakini hakuwepo nikaambiwa upo hapa hivyo nimeona nije kukushirikisha"sasha alimaliza kuongea
Niliishiwa nguvu na kurudi ndani pale saloon na kuanza kumpigia simu vivian ingawa haikuwa hewani.
Hofu ikanijaa na nikaanza kufanya kila liwezekanalo nimtafute bila mafanikio na kuona ni vyema niwashirikishe wazazi na wasimamizi ambao nao juhudi zao hazikuzaa matunda.
Wakati huo watu walishaanza kujaa kanisani na ikawa ni kitendawili kingine kuwaambia watu wale kuwa harusi imevunjika.
Hakukuwa na jinsi zaidi ya kuwaambia watu wale ambao wengi walishtushwa na wakitaka kujua nini tatizo na niwakati huu nikaanza kuhisi maumivu na kutokwa na machozi baada ya kumwona mama yangu na mama yake vivian wakitokwa na machozi.
Nilirudi nyumbani na kujifungia chumbani na kuanza kuwaza ni kitu gani kimetokea na kumfanya vivian asionekane wala kutoa taarifa juu ya aliko.
Tulitoa taarifa kituo cha polisi na kuendelea kumsaka kila kona huku siku nazo zikizidi kuyoyoma nami kujikuta mtu mweye majonzi kila kukicha.
Ilikuwa ni ngumu sana kuamini kama vivian angeweza kuchukua uamuzi wa kunitoroka na nikajiuliza hata kama angefanya hayo kwa nini sikuona dalili za yeye kuwa na mahusiano na mtu?
Niliumia sana ingawa baada ya miezi michache nikajikuta naanza kuizoea hali ile na hatimaye kuanza maisha mapya nikiwa sina hamu ya kuwa na binti yoyte kwani vivian aliuharibu moyo wangu.
Hebu fikiri umetimiza taratibu zote na siku ya harusi ukiwa unajiandaa kwenda kwenye kiapo mara unaambiwa mpenzi wako katoweka katika mazingira hatarishi na hakuna taarifa za wapi aliko.
Niliyasahau hao na wiki mbili baadae nikaomba kuhamishwa kikazi kutoka dar na kuhamia mbeya nikijua kuwa nitapata muda wa kusahau na hatimaye kuanza maisha mapya jambo ambalo hata ndugu zangu walinikubalia.
Miezi mitatu baadae nilikuwa nimeshaanza kuufahamu mji wa mbeya pamoja na baadhi ya mitaa yake. Kazi yangu ya udaktari pia ilinipa nafasi ya kufahamina na watu wapya kila siku na hatimaye kusahau kila dhoruba iliyonikuta na kuwa mtu mpya ingawa kuna nyakati tukio klile lilinirudia akilini lakini nilijitahidi kuwa na msimamo wa kuamini kuwa kuna siku furaha itanirudi.
Kuwakimbia wanawake ni shida hata kama wawe wamekutenda kiasi gani, yaani miezi kama sita baadae nikajikuta nikiwa ndani ya penzi la mtoto Sonia ambaye pia alikuwa daktari mwenzangu pale Hodari Family Hopsital na hakika alikuwa fundi wa kunifanya nisahau yote ya liyopita na kuniahidi kuwa atakuwa furaha yangu hasa baada ya kujua kisa kilichonikuta,.
Siku moja jumapili kama ya leo nilipigiwa simu kuombwa niende kazini na kuwambiwa kuwa kuna watu watatu wamepatwa na ajali mbaya sana na walihitaji kupewa msaada wa kidaktari haraka sana.
Nilikuwa zangu mitaa ya iyunga na rafiki yangu Fred tukipata zetu bia weekend hiyo na nikaenda haraka sana kazini na kuonana na wangonjwa hao.
"Mama yanguuuuuuuuu" ilikuwa sauti ya chini chini ambayo niliitoa na kila mmoja wa watu waliokuwa pale walijua nimeshtuswa na jinsi watu hao walivyoumia katika ajali hiyo lakini ilikuwa ni mshangao wa kuona uso wa vivian ukiwa umeharibika sana.
Haraka nilienda mpaka ofisini kwangu na kubadilisha nguo haraka na kuwaandaa wagonjwa wale maana walivunjika na kutokwa na damu nyingi na nikajisemesha kuwa " Nilazima nihakikishe wanapona"
Walikaa pale hospitali kwa nzaidi ya siku saba bila ya kufumbua macho wakiwa katika hali ya mahututi na siku ya nane vivian alifumbua macho na siku tano baadae alikuwa mzima kabisa.
Sikutaka kuonesha kushtushwa na kuonana naye ila yeye aliishiwa nguvu na hakuamini kuwa kamwe tungeonana na nikajua kuwa alikimbia na kuja tunduma kuishi na kijana mmoja ambaye alikuwa kapata naye ajali na ni mmoja kati ya vijana ambao wanafedha nyingi na walifahamiana siku mbili kabla ya ile siku ya harusi waliyokimbia na ilikuwa ni tamaa ya fedha.
Vivian kila siku akiwa pale hospital alionesha kuwa mtu mwenye mawazo sana na siku moja usiku siku moja kabla ya siku ya pili yake kuruhusiwa nikiwa nataka kufunga ofisi yangu kurudi nyumbani mara niliona mtu akipita haraka na kuelekea usawa wa dirisha akitaka kujitupa kutoka ghorofa la tano.
Kumwangalia vizuri alikuwa ni vivian nilikimbia na kupiga kelele za msaaada mamaaaa weeeeeee saidieni kabla ya kushtushwa na dogo mida hii akiniamsha baba baba chakula tayari kumbe ilikuwa ni ndoto...
Ndoto za mchana ni shida sana
0 comments: