Niliishi kwa kufungwa kishirikina miaka 15
Nilikuwa katikati ya msitu mnene sana nikitafuta upenyo wa kuniongoza nitoke humo na mkononi mwangu kuna kitu nilikuwa nimekishika bila kukitambua.
Nilikaa kwa muda bila kuona dalili zozote za kujikwamua na muda mfupi baadae nilianza kuona dalili za mwanga na kuanza kuufuata.
Niliufuata ule mwanga na hatimaye jikajikuta nipo nje ya nyumba yangu.
Cha kushangaza kuna mtu alikuwa katika bustani yangu pembeni ya mti mmoja mkubwa akitoa misumari iliyopigiliwa.
Hakuishia hapo ghafla akaanza kunyofoa baadhi ya mashina ya mboga ya ajabu iliyokuwa imestawi pale bustanini na nikashangaa kwani sikuwahi kuona hizo mboga.
Wakati akafanya hayo yote hakuniona na nilipochungulia nadani mwangu nikaona kila aliyekuwemo ndani akiwa busy na mambo yake na hakuna anyejua kuwa kuna mtu pale nje sikuweza kumwamsha mke wangu kwani kila nikijaribu kutoa sauti haikufika mbali wala kumshtua hata huyo mtu.
Nikajikuta machozi yakianza kunitoka huku mtu huyo akija mpaka mbele ya nyumba yangu bila kuniona tena na kufukua fedha zikiwa zimechimbiwa upenuni mwa nyumba kiasi kidogo.
Pia mtu huyu alipofika mbele ya mlango mkuu wa kutokea nje alifunua kitambaa kirefu kama sanda na nilishtuka kwa kupiga kelele baada ya kuona nyoka mkubwa alifukiwa pale jamii ya chatu na sikuwahi kugundua na mbaya zaidi kelele hizo hazikufanya lolote na nikawa hata nikijitahidi kumfuta nashindwa kutoka kwani miguu ilikuwa kama imeshikwa na nguvu fulani..
Ndoto hiyo ilinifanya nishtuke na kwenda mpaka chumba cha mke wangu kwani muda huo tulikuwa tumetengana vyumba kutokana na mambo kadha wa kadha ya mahusiano yetu na tulikuwa njiani kupeana talaka.
Ilikiwa ni ngumu kwake kuamini kama usiku huo ningemwita lakini alinielewa na tukarudi mpaka sebuleni na kumsimulia ndoto hiyo ya ajabu.
Kwa mara ya kwanza mimi na mke wangu tukajikuta tukianza tena kukubaliana na kuamua asubuhi twende kwa mchungaji.
Saa mbili asubuhi nikiwa nje sina kumbukumbua nilikuwa nikifanya nini lakini mke wangu alikuja na bila hata kujua chanzo ni nini tukaanza ugomvi na mwishowe kila kitu kikaishia hapo.
Maajabu ni kwamba usiku wake tukajikuta tukiongea pamojatukiwa sebuleni kwetu, wakati huu sijui ni Mungu gani nilikuwa naye kwani nilimpigia simu mchungaji ambaye alikuja na nikamsimulia mkasa mzima juu ya ndoto na hali yangu ya kimaisha.
Miaka 15 iliyopita nilifanikiwa kufunga ndoa na mke wangu na kubahatika kuwa na maisha ya mazuri nikiwa na utajiri wa kiasi na kwa kuwa niliamini baraka hizo ni za mimi na jamii yangu hivyo nikaanza kusaidia kila ndugu aliyehitaji msaada katika maisha yake.
Hakika mkono utoao ndio unaobarikiwa hivyo kila siku nikawa najikuta nazidi kupata mafanikio na kuongeza utajiri wangu na familia.
Wakati huo nikawa nimerudi kijijini na kuongea na mama pamoja na ndugu kuwa nilihitaji kujenga nyumba kubwa ya mimi na familia na niliyokuwa nikiikaa itumiwe na ndugu pamoja na wadogo zetu wa familia zetu waliopo na wanaokuja mjini kwa masomo na kazo binafsi ili kuanzia maisha.
Walifurahi sana na kunipa baraka zote na baba yangu mdogo yeye alifurahi zaidi kwani watoto wake wawili nilikuwa namsaidia kuwasomesha akafurahi sana na kuja kunisaidia kutoa ushauri wa ujenzi mara kwa mara kwani alikuwa na taaluma hiyo.
Nyumba ilijengwa haraka na mwaka mmoja baadae nilihamia tena kwa tafrija kubwa huku kila ndugu akifurahi na kuniombea nizidi kuwa na mafanikio.
Tangu siku ya kwanza kuhamia kwenye hiyo nyumba ndio ilikuwa siku ya kwanza na ya mwisho kwa mimi kuwa na furaha, amani na mafanikio yakaanza kubadilika na kuwa huzuni na umaskini kwangu.
Mke wangu hakubahatika kushika mimba na akakaa nayo zaidi ya miezi mitatu bila kutoka, kila siku ni ugomvi na mbaya zaidi kila siku biashara zilififia mpaka ikafika hatua ya mimi kufanya kazi kama dereva tax wa gari letu la mwisho pekee.
Niliokoka tu kuuza nyumba lakini kila kitu kilipotea kwa muda mfupi kama vile nilikuwa na mikosi au kuna upepo mbaya uliokuwa ukiniandama.
Baada ya kumsimulia yule mchungaji mkasa huo pamoja na kuwa alihuzunika sana lakini mwisho wa siku alitushauri jambo moja ambalo lilikuwa gumu kwa kawaida lakini hatukuwa na ujanja zaidi ya kukubaliana naye.
Sikutakiwa kutoka nje mimi na mke wangu ndani ya siku saba tukikaa ndani bila hata ya kutoka nje ya geti tukifunga na kuomba bila kukatisha na kuwa yeye angejumuika nasi kila siku jioni na siku ya saba tungeshuhudia miujiza ya kustaabisha.
Tulianza kazi hiyo wakati huu kila mtu akiwa makini zaidi kati ya mimi na mke wangu na mchungaji akiwa anakuja kila siku, na nikaanza kushangaa kuwa tukiwa ndani bila kutoka tunakuwa na maelewano zaidi..
Siku ya saba nilishangaa mlango kugongwa na mama, dada zangu wawili, baba mdogo na shangazi zangu walikuja pale na wanao jambo ambalo halikuwa kawaida tangu ile tafrija ya kuhamia katika nyumba hiyo.
Mchungaji alianza sala pale na huwezi amini mara baba mdogo akaanza kiweweseka na kutoka nje huku mchungaji akisema tumfuate.
Tulishangaa kuona akitoa misumari mitano aliyoipigilia kwenye mti pale bustanini na kushuhudia kuwa jinsi mti huoambavyo ungezidi kukua na misumari hiyo basi mimi, mke wangu, mama, na dada zangu wawili tusingekuwa na maelewano kabisa.
Alipanda mbegu za chuki na kuondoa kabisa amani kwangu na mke wangu na kunifanya kuwa na tabia zitakazoota mizizi ya kudumu na mbegu hizo alizifukua pia..
Alifukia fedha nilizowahi kumpa ili kamwe nisipate upepo wa mafanikio wala kuwa na maendeleo zaidi ya kudumaa na kila nitakachokipata kiishe bila ya kuzaa maendeleo yoyote.
Alifukia hirizi mlangoni ili kila asububi mimi na mke wangu hata kama tutakuwa na ujasiri wa kutafuta suluhu tusahau na kila mke akiruka pale mtoto aliyeko tumboni atoke na tusiwe na familia kabisa..
Nililia kwa uchungu zaidi nikimwangalia mke wangu, mama na wadogo zangu na nikashikwa na hasira zaidi nilipomwona baba mdogo akijifanya kulia kuonesha kujutia, nilijikuta namrukia huku nikipiga kelele nitakumalizaaaaaaaa kabla ya kushtuka muda huu na kujikuta ni ndoto tu ya mchana nikiwa nimeshika biblia yangu baada ya kutoka kanisani.
Swali langu je kuna watu kama hawa duniani?
Kama wapo na washindwe katika jina la YESU amen ruksa kushare
0 comments: