Msome binti aliyewahi kunipa tumbo joto baada ya kumtangazia kibuti
Nilikuwa uwanjani nikicheza mpira wa kikapu na baadhi ya marafiki na dakika tatu baadae alikuja fetty binti ambaye nilikuwa nimempiga kibuti.
" kaka fetty anaomba kuongea na wewe"
" achana naye fala huyo hana maana yoyote D"
Niliongea maneno hayo huku nikiukimbilia mpira na kuendelea kicheza kwa furaha.
Fetty aliendea kukaa pale kwa zaidi ya robo saa akinitolea macho na sikuweza kufanya lolote zaidi ya kumwona kama alikuwa akipoteza muda wake.
Alisimama na moja kwa moja akaja mpaka katikati ya uwanja na kunishika mkono jambo lililomfanya kila mchezaji kusimama na kusogea pale kuona nini kingetokea.
" umeniacha mimi na kunipa maneno machafu kisa huyo binti mpya uliyempata? Hebu kumbuka ni mangapi tumefanya pamoja na ni miaka mingapi imepita ukiwa nami na ukiapa kuwa lazima unioe?"
" acha hizo, unajua unatukatisha stimu ya zoezi?"
"Ok naondoka ila nawe una siku chache za kuishi kama mimi" aliongea maneno hayo fetty huku akifuta machozi na kuondoka eneo hilo.
Sikujali kitu na kuendelea na zoezi ingawa ile sentensi ya "Ok naondola ila nawe una siku chache za kuishi kama mimi" ilinikaa sana kichwani na baada ya muda mfupi nikaomba nipumzike na aingie mwingine kuicheza nafasi yangu.
"Ok naondola ila nawe una siku chache za kuishi kama mimi" mmmmmh fetty ana maana gani kuongea yale maneno? Au nakaribia kufa??? Mmmh ila kweli kama kakonda vile au inaweza kuwa kaniambukiza virusi?? Noooo au labda anataka kuniua au kualika watu waniue? Ila hapana
Nilijiuliza maswali hayo na kujipa majibu ya kujiridhisha na hatimaye muda wa kurudi nyumbani ukafika.
Ikuwa ni mara yangu ya kwanza kuona umuhimu wa kusoma simulizi ya simu ya ajabu ya bwana fuledi ili nijifunze mbinu za kuwakwepa watu wa dizaini kama hii, yaani kama nilivyosimuliwa na rafiki yangu hodari ambaye yeye alisoma.
Ok baada ya kusoma nikagundua kuwa natakiwa kuwa makini kwani fetty angeweza kutumia badhi ya mbinu kunidhuru na hivyo nikajizatiti.
" mwanangu mbona siku zinavyozidi kwenda unakonda sana usije ukawa una-ukimwi?"
Maneno hayo aliongea mama huku akitaka kujua kwa nini siku za karibuni nimekuwa mdhaifu na ninakonda sana.
Sikumjibu kitu nikainuka na kwenda nyumbani kwa fetty na kumwomba aniambie ni nini alitaka kunifanyia au alikuwa na ukimwi na kaniambukiza hivyo anajua nitakufa?
" usijali wewe ni kidume wa kuharibu ndoto za wenzako subiri tuu utausoma mchezo mzima"
Majibu haya ya fetty yakanifanya nianze kulia moyoni na kundoka eneo hilo nikijua tayari ninao ukimwi.
" dalili moja wapo ya kujua kama wewe ni mwathirika ni vitu kutembea mwilini na kifua kuwa kizito na ulimi kuwa na utandu"
Nilirukwa na akali baada ya kusoma jarida moja na kuona wakiainisha baadhi ya dalili za ngoma na nikaanza kuona kuwa dalili zote zanihusu kwani kasi yangu pale uwanjani imeshuka na pia vitu hunitembea mwilini ingawa ulimini ilikuwa taabu kujua nini kilikuwepo mwanzo ili nilinganishe.
Akili ya haraka ikawa ni kumfuata fetty na kumwomba anisamehe ili aniambie ukweli juu ya hali yake na kunikubali pamoja na kuniambia hana ukimwi wala nini mimi nikajua ananifariji tuu kuendea kuumia.
" niende kupima au nifanyeje?
Swali hili lilinitawala bila hata ya majibu na nikaona nisubiri muda muafaka nione nini kingetokea.
Ndani ya muda mchache nilianza kuona nikibadikika na kumchukia hata binti ambaye alinifanya niachane na fetty.
Kila kitu kilibadilika na kuanza kuona nilikuwa ni mfu nitembeaye.maisha yalibadilika na nikawa mtu wa hasira nisiyetaka kitu chochote zaidi ya kujifungia ndani.
Nilikaa siku moja na baba yangu na akawa akinifundisha maisha na kunipa faraja na ujasiri wa kuwa nitakuja kuwa mwanakikapu hodari sana.
Tatizo langu likawa nahisi kama anajua nina ukimwi na ananikebehi kwani wakati huo hali yangu ilidorora sana.
Siku moja majira ya asubuhi akikuja shangazi yangu ambaye yeye ni daktari na aliponiona alishtuka sana na kuniuliza "una nini mbona umetokwa mpaka na vidonda mwili umepauka na umekuwa dhaifu sana kama mwenye ukimwi?"
Sikutaka kabisa kuamini kama sasa kila mtu anajua kuwa nimeathirika na wakati naanza kurudiwa na akili za kawaida nikaanza kuona mambo mengi ambayo nilisoma kwenye vitabu.
mambo hayo yalikuwa ni pamoja na watu kuanza kunitenga kuanzia darasani mpaka nyumbani na kuna siku nilimshuhudia binti wa kazi akikiweka alama ndogo kikombe nilichonywea chai ili asije jisahau akakitumia.
Nilizidi kulia na kuona kila mara nikiwa na mawazo na siku moja kuna rafiki alinifuata na kuniambia ni bora niende kupima kwani naweza kuwa najipa presha bure mbona fetty yeye ana nawiri tu kila kukicha?
Wazo lilinikaa na wakati huu kwa kuwa njilishakata tamaa ya maisha nikafikiri kufanya hivyo ingawa kila nilipofikiri namna majibu yatakavyotoka nikaona nazidi kuwa mnyonge na kusahau kabisa kwenda.
Nikawa kila nikiwaona rafiki zangu wakiwa na furaha huku wakijadili nini watafanya baada ya masomo kiukweli nikawa nazidi kukata tamaa sana ya maisha.
Asubuhi moja niliondoka mpaka kituo kimoja cha ushauri nasaha na kupanga foleni. Kiukweli kuliwa na watu wengi na siku hiyo baadhi walikuwa wakija kuchukua dozi zao wengine wakija kucheki nafya zao.
Na kila mtu aliyetoka chumba cha daktari alikuwa nya nyuso yenye kutoa taarifa fulani, kuna waliofurahi wakiwa na wapenzi wao kuna waliokuwa wakitokwa na machozi na kila ilipofikia nafasi yangu nikasimama na kurudi kukaa mwishoni.
Hata baada ya kupimwa ule muda wa majibu tumbo langu lilikuwa la moto na nakumbuka kuna binti mmoja alikuwa akiniangalia huku akinionea huruma kwa jinsi uso wake ulivyoonesha.
Nilirudia mchezo ule ule wa kurudi nafasi ya mwisho kila nilipojikuta natakiwa kuingia kuchukua majibu mpaka pale nilipojikuta sina jinsi kwani nilibaki peke yangu.
Sikuamini kuambiwa sina ukimwi nilikurupuka kutoka chumba kile nikicheka na kurudi nyumbani ambako sasa mwili ulianz kurudi vizuri na kila siku nikajikuta narudia hali yangu ya zamani hata kama kuna baadhi ya watu walishaanza kutangaza kuwa natumia dozi lakini nilijikuta nawapotezea huku nikiapa kutokuwa nna mahusiano kwa muda huo au hata nikija kuwa nayo nisifanye kama nilichomfanyia fetty.
Miezi minne baadae fetty alinifuata na kuniambia nafikiri umekoma na kwa muda tulisaidiana kuyakabili maumivu ya kibuti..... nilitaka nimpe ngumi ila nikaogopa asije kuja na kisanga kingine
0 comments: