“…Njia 5 za kuzifuata baada ya kuachwa na mwenza wako …”

21:18:00 Unknown 0 Comments

1. KUBALI.
Mambo yanavyokuwa yameisitishwa kati yako na X wako, kitu cha kwanza kukifanya ni kukubali kuwa sasa wewe na X wako mmeachana na kuwa mahusiano yameisha.
Najua ni jambo gumu kukubali ila kwa kufanya hivyo itakupa nguvu zaidi za kujifikiria wewe zaidi na mambo yako kuliko kukaa na kumfikiria zaidi X wako jambo litakayokuumiza zaidi na kukukosesha ujasiri.
2. ACHA MAWASLIANO.
Hii ni njia muhimu ya kumsahau X wako kabisa, kutokuwa na mawasiliano nae inakuonesha na kukupa nguvu kuwa sasa unaendelea kusonga mbele na huangalii nyuma tena.
Kumtumia x text, kumpigia au hata kumtafuta mara kwa mara kumwomba msamaha inampa nguvu za kuendelea kukuumiza huku ikionesha jinsi gani ulivyoumizwa na ambavyo hujitambui hivyo usimpe mwanya huo na kujiumiza zaidi.
3. JIPE MATARAJIO CHANYA
Katika kipindi hiki ni vizuri uanze kuangalia nini ni bora zaidi kwako, fikiria ni nani anaweza kukupa furaha, kukufanya uwe na furaha, fikiria vitu chanya na usikaribishe mawazo hasi kyakutawale.
Kwa kutokaribisha mawazo hasi yakutawale kichwani mwako naamini utamsahau X wako na kuwa na furaha zaidi.
4. PATA FURAHA
Unafahamu hobbies zako kama unapenda kuogelea, kuangalia filamu, kusoma hadithi za fuledi, kutoka na marafiki zako basi huu ni muda muafaka wa wewe kufanya haya yote.
Kufurahi na marafiki kutakufanya usahau mahusiano yako na X wako na kufungua ukurasa mpya wa furaha
5. TUMIA MUDA KUJIFAHAMU WEWE NA UMUHIMU WAKO
Kuna wakati tunasahau furaha zetu na kuanza kuangalia furaha za wenzetu, hebu jifikirie wewe na umuhimu wako na acha kutaka watu wakuumize na kukupotezea furaha yako.
Waachie waje kwako wale watakaokupa furaha na achana na wale wanaotaka kuchezea maisha yako na furaha yako./

You Might Also Like

0 comments: