Usimtegemee sana mwanadamu katika maisha yako, kwanza ni dhambi!!........ kama huamini soma kisa hiki
Katika kijiji cha Matare wilaya ya Mugumu Serengeti, bwana Wambura alikamatwa kwa kesi ya kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu.
Huku nyuma akiacha mke na watoto wanne waliokuwa wanasoma. Hukumu
hiyo ilimtesa sana kichwa chake, alitamani kila mtu anayemhisi kuwa ana makosa aingie katika moyo wake na kuupata ukweli.
hiyo ilimtesa sana kichwa chake, alitamani kila mtu anayemhisi kuwa ana makosa aingie katika moyo wake na kuupata ukweli.
Alilia na umaskini wake, labda angepata wakili mzuri angeweza kumtetea, kumkosa wakili kukahalalisha kifungo hicho!! Alikwenda gerezani huku akiumia sana rohoni. Aliyaanza maisha mapya kwa shida sana, akawamnyonge
kila mara na mwili ukapoteza afya kiujumla.
kila mara na mwili ukapoteza afya kiujumla.
Huko gerezani alifanikiwa kupata rafiki aliyekuwa na cheo ama jukumu la uzikaji wa wafungwa hasahasa ambao hawakuwa na ndugu ama ambao ndugu zao huwa hawajitokezi pale gerezani.
Mzikaji alijaribu sana kumtia moyo Wambura na kumwaminisha kuwa hiyo ilikuwa hatua tu ya maisha anapaswa kuizoea na siku moja ukweli
utajulikana tu! Bwana Wambura maneno ya mzikaji hayakumuingia kabisa.. alizidi kunyong’onyea. “Siwezi kuvumilia kukaa gerezani miaka mitatu…..kama unajali kilio changu nisaidie nitoroke kwa namna yoyote ile ndugu yangu!!” Wambura alimsihi mzikaji.

SIKU MOJA mzikaji akamwambia Wambura kuwa msaada umepatikana. Lakini yataka moyo!!
Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu nitoke humu!!” alijibu kwa msisitizo huku akimtegea sikio mzikaji. “Msaada pekee wa kukutorosha humu ndani ni kwa njia ya jeneza… yaani mfungwa akifa mimi nakuunganisha naye kwenye jenerza…..” akashusha pumzi kisha akaendelea “Wewe ukisikia kengele ya msiba, njoo mara moja kwenye chumba cha maiti, utakuta tayari sanduku liko katikati ya chumba linakuwa halijafungwa, funua mfuniko ingia ndani yake ulale pembeni ya maiti kwani sanduku huwa kubwa la kutosha kila aina ya
maiti na hata miili miwili inaingia.
maiti na hata miili miwili inaingia.
Kisha nitakuja na kulipigilia misumari. Baada ya muda tutalipakia kwenye gari na kutoka kwenda nje ya gereza makaburini nikiongozana na baadhi ya wafungwa na maaskari magereza.
Tutakuzika huko lakini baada ya dakika 20 hadi 30 nitarudi kukufukua. Hautaweza kushindwa kupumua kwa dakika hizo, utatoka ukiwa huru.”
JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini lilimtisha sana Wambura. Hata hivyo akaona afadhali afanye hivyo kuliko kukaa gerezani miaka mitatu bila kosa.
JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini lilimtisha sana Wambura. Hata hivyo akaona afadhali afanye hivyo kuliko kukaa gerezani miaka mitatu bila kosa.
Siku moja akasikia kengele ya msiba. Akafanya kama alivyoelekezwa na mzikaji. Akaenda na kuingia chumba cha maiti. Kweli akalikuta sanduku, akiwa na hofu kuu akaingia na kulala pembeni ya maiti iliyokuwepo. Mara akasikia mtu ameingia na kulipigilia msumari sanduku. Muda mfupi baadaye sanduku likainuliwa na kuwekwa kwenye gari.
Gari likatoka nje ya gereza hadi makaburini. Sanduku likashushwan na kuwekwa kaburini na kuanza kufukiwa. Wambura alijitahidi sana kuvumilia japo hofu ilizidi kutanda. Alimtegemea sana mzikaji na alianza kumuona mkombozi wa maisha yake.
Kama alivyoambiwa, akasubiri dakika kumi, ishirini.. zikapita kimya!! Dakika
thelathini kimya. Joto nalo likazidi kuongezeka.
thelathini kimya. Joto nalo likazidi kuongezeka.
“Nitavumilia hadi afike…” alijisemea kisha akajiongezea kauli ya ujasiri.
“Kama nilitakiwa kuishit gerezani miaka mitatu kivipi dakika kadhaa za hapa kaburini zinishinde” KWA kuwa alishakaa gerezani kwa muda kiasi akatamani kujua aliyekufa ni nani… ni kweli aliogopa kuitazama maiti lakini aliona
kama inatisha zaidi ikiwa imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi.

Akaifunua upande wa usoni… Kwa kuwa kulikuwa na giza nene alikodoa sana macho kuitazama. LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA NA SURA YA MZIKAJI!!! MZIKAJI ALIKUWA AMEKUFA NA AMEZIKWA NA AHADI ZAKE ZA UKOMBOZI!!
________________
________________
FUNZO::
Usimtegemee sana mwanadamu katika maisha yako, kwanza ni dhambi!! Pili mwanadamu anakumbana na vikwazo kama unavyo kumbana navyo wewe hadi kumwendea yeye.
Hivyo kumpatia maisha yako ni kuzidi kuyaweka hatarini zaidi!! Umeonewa umesingiziwa unanyanyaswa….. mwachie Mungu afanye maamuzi…
_______________
Haya mzikaji aliyetegemea atamfukua naye ni maiti…… tazama mateso atakayoyapata hadi kufa kwake…..Bila shaka atatamani kurudi
gerezani kwa miaka mingine kumi lakini haitawezekana tena!!!

share
0 comments: