KILA KITU KATIKA MAISHA KINA WAKATI WAKE!!!!!!!!!

21:39:00 Unknown 0 Comments


*Marafiki zako wote walihitimu chuo katika umri wa miaka 22 na 28. Lakini wewe bado unahangaika upate nafasi ya kujiunga na chuo....
kuwa mpole muda wako unakuja!
*Marafiki zako walipata kazi nzuri mara tu baada ya kuhitimu chuo, lakini wewe bado unasaka kazi bila mafanikio ingawa una degree yako.
Ndugu yangu kuwa mpole muda wako utafika!
*Marafiki zako wote wameoa/kuolewa na wanafurahia ndoa zao, lakini wewe unazidi kukutana na walaghai wa mapenzi na wanakuumiza kila kukicha.Pumzisha akili mambo mazuri yapo njiani yanasubiri muda wake!
*Wenzako wote wamepata watoto katika ndoa zao, lakini wewe ni mwaka wa kumi sasa unahangaika kupata mtoto bila mafanikio. Ndugu yangu usitetereke imani yako kwani Mungu anajua mpango wake kwako.......muda utafika
*Kila rafiki yako anapopata kitu na wewe unafikiri ni haki yako pia kupata, usitetereke, kuwa imara na mwenye uvumilivu ukiamini katika mafanikio.
SIKIA! Maisha sio mashindano kati yako na mtu yoyote yule.Kuwa wa kwanza KUONDOKA sio lazima awe wa kwanza KUWASILI sehemu aendako.
Maisha huhusu zaidi USALAMA wako,MAFANIKIO na FURAHA yako pia.
Kuwa MPOLE, mwenye BIDII,MWEREVU, mwenye KUJITAMBUA na Mungu atakubariki kwa MAFANIKIO na FURAHA.
Mungu ni mwema na hujua muda wake wa kukubariki, huja kwa wakati muafaka na kuufanya muda huo kuwa muda mzuri kwako.
KUMBUK! Mungu halali wala kupumzika akikuandalia MAFANIKIO na FURAHA.
Like na share kwa kila mtu aliyepoteza MATUMAINI

You Might Also Like

0 comments: