Je unafahamu aina za watu katika maisha yako?
WEWE NI MTU WA AINA GANI?
Mwakibubu alimuulliza baba pachu baada ya kumsimulia siri yake juu ya kuwa mwathirika na hata baada ya kumwambia juu ya madhaifu aliyomfanyia kama rafiki yake na baba pachu akachukulia sawa na kumpa ushauri na kuwa rafiki wa kweli katika simulizi ya SIMU YA AJABU
LOL. Lakini leo nimetamani mimi kubadili na kuliongea hili kama mimi FULEDI kwa wale ambao hawajawahi jiuliza hili katika maisha yao.
Huwa nina kuwa na mifano mitatu kila ninapofikiria watu waliopo katika maisha yangu, familia, marafiki, wasomaji wa simulizi zangu,wafanyakazi wenzangu na kila mtu ambaye nabahatika kukutana naye.... Na wote hao huwa nawaweka katika makundi matatu kama ifuatavyo
WATU MFANO WA JANI/MAJANI
Kuna watu wanakuja katika maisha yako kama majani katika mti. Wanakuja kwako wakiwa na kusudi maalaumu na huwezi kuwategemea kwa kuwa wao ni dhaifu na wasio na nguvu na wako hapo kwa ajili ya kukupa kivuli.
Wao wako kama majani ya mti, wako hapo kuchukua kile walichokusudia na mara upepo mkali, mvua kubwa, jua kali linavvyoyakumba maisha yako nao wataondoka na kupeperuka kama majani ya mti.
Hutakiwi kuwa na hasira nao kwani ndio jinsi walivyo na ndio maisha yao
WATU MFANO WA MATAWI YA MTI
Hawa ni watu ambao huja katika maisha yako na wanakuwa kama yalivyo matawi ya mti. Wako imara kuliko majani ya mti lakini unatakiwa kuwa nao makini sana.
Watakuwa karibu nawe kila msimu wa matatizo lakini kama utakumbwa na dhoruba moja kubwa au zaidi basi kuna uwezekano mkubwa kuwa watakuacha.
Muda mwingi matawi huvunjika wakati mambo yanakuwa magumu kuyahimili ingawa ni imara kuliko majani hivyo unatakiwa kuyajaribu kabla ya kuharakisha kuyaamini na kuyapa uzito mkubwa.
Kwa kawaida matawi huzidiwa pale uzito unavyoyazidia lakini pia hutakiwi kuwa na hasira kwani ndio jinsi yalivyo na ni maisha yao.
WATU MFANO WA MIZIZI YA MITI
Kama utafanikiwa kuyangalia maisha yako na ukagundua una watu wako katika maisha yako mfano wa mizizi, basi wewe umebahatika kupata kitu muhimu sana na unatakiwa kumshukuru MUNGU.
Kama ilivyo mizizi, ni shida kuiona kwani inajitahidi kujificha isionekane. Kazi yake ni kujificha huku ikikushikilia na kukupa nguvu na afya katika maisha yako na maendeleo yako.
Kama unastawi, basi mizizi inakuwa na furaha sana, inahakikisha inakuwa katika hali yoyote ile ili kukufanya ufikie mahali pazuri na hata kama una matatizo basi mizizi haitataka watu watambue na hata ukipata mafanikio mizizi haitaki watu wajue kuwa nayo imechangia.
Na hata ikifikia ukapatwa na dhoruba kali basi kazi yao itabakia kukushikilia, kukuboresha zaidi, kukulisha na kukupa maji ili usitetereke .
Kama ambavyo mti ulivyo na matawi mengi, majani mengi na mizizi michache hebu nawe angalia maisha yako.
Una matawi mangapi, Majani mangapi na je una mizizi?
Je wewe ukoje kwenye maisha ya watu?
Andika ASANTE MUNGU KWA MIZIZI ULIYONIPA! kama ungetamani kuwaita leo hii au kushare huu ujumbe ukiandika na maneno yako mazuri kwao
Nakutakia jumapili njema na kumbuka kitabu cha BOMA na SIMU YA AJABU kinapatikana toa oda yako kwa namba 0713317171
ONYO, usipoteze muda ku-share ujumbe huu au kutoa maneno mazuri kwa MAJANI kwani hawatakuelewa na hawatajali pia
0 comments: