BINTI ALIYENIBOA MWEZI HUU WA kwanza HUYU HAPA I HATE HER

16:14:00 Unknown 0 Comments


Mambo mengine bwana yaani shida tupu..... kuna binti mmoja jana kaniboa sana yaani.
Jana nilikuwa zangu town nanunua baadhi ya mahitaji yangu ya nyumbani, ebwana nikakutana na binti mmoja mzuri balaaaa.
Nikasema huyu lazima nimsimamishe niombe namba, ile namfuata akaingia kwenye duka moja la madawa baridi nami nikaingia kumbe ni duka lao na mama yake yupo pale ndani ikabidi nizuge ninunue panado za 500 na maji na kunywa pale panado mbili.
Nikatoka na kubana sehemu ili nimsubiri atoke, akapita jamaa yangu nikataka kujikausha akaniona ikabidi tuanze kuonge ana jamaa hamalizi story mara nikaona binti anatoka dukani ila jamaa kanibana pale..
Jamaaa kuniachia demu akawa kaingia kwenye daladalaa ya mbalizi ikabidi nami nipande ili atakaposhukia nami nishuke nimpe maneno.
Tumeenda akafika sehemu kashuka nami nikanyanyuka nakushuka kuangalia alishavuka barabara namsogelea kumbe nyumba ya kwanza ndio yao kaingia na nje pale baba yake yupo ikanibidi nikae kwa Shoe Shine na kubrash viatu na kupanda gari.
Mpaka sasa nafikiri nimefanikiwa kukudanganya wewe usomaye maana unavyopenda kusoma umbea na ulivyojiandaa kunishushua nadhani umesihiwa pozi

Karibu Mbeya shared a link.
Karibu katika duka letu la nguo za kike lililopo mwanjelwa-mbeya, Tunauza:- Top, skin jeans, magauni kwa bei ya jumla na rejareja.

You Might Also Like

0 comments: