HANGOVER MBAYA kweli

14:18:00 Unknown 0 Comments


Nilikurupuka toka kitandani na kujiandaa kisha kuanza kutimuka mbio lakini hatua kadhaa nikakumbuka sikuamuaga vizuri mke wangu na kuamua kurudi ndani mara moja.

Nilimwangalia pale kitandani alipokuwa amelala kwa zaidi ya dakika kadhaa hali ya uchungu ulioambatana na hisia kali za mapito machungu ambayo yanaendelea kuniandama vilinifanya nitokwe na machozi.

Niliinama na kuligusa tumbo lake likiambatana na busu moja na kuondoka huku taratibu huku nikiyafuta machozi na kuendelea na safari yangu.

Wakati huu mke wangu alikuwa na ujauzito ambao ulishafikia siku za mwisho kabisa na kwa maelezo ya daktari ilikuwa muda wowote ule angetakiwa kupelekwa hospitali.

Niliendelea kuwaza jinsi maisha yalivyobadilika na kuwa magumu na mpaka inafikia hatua ya kukosa fedha ya kula huku nikishuhudia kila mipango yangu ikigeuka na kuwa kama misumari ya moto miguuni kwangu.

Nikakumbuka jinsi mtoto wetu wa kwanza alivyokufa siku moja baada ya kuzaliwa na mke wangu kupatwa na ugonjwa wa ajabu na kuwa mtu wa kumalizia haja zote alipo huku mimi nikiwa msada wake wa pekee.

Nikamshukuru Mungu kwa kumponyesha na kuweza kumsimamia mpka akawa katika hali hii ya ujauzito tena Hata baada ya miaka zaidi ya sita ya yeye na mimi tukisali kuomba Mungu atende miujiza.

Ilifikia hatua hiyo kwani baada ya tatizo la kwanza na  hata baada ya madaktari kukiri kuwa ingekuwa ni bahati tu kwa yeye kushika mimba tena.Ni jambo hili ambalo lilomkosesha raha sana mke wangu na kumfanya ajione kama alikuwa mwenye nuksi.

Tangu tuoane ilishapita miaka 10 ambapo baada ya kuoana tumepita katika barabara yenye machungu makubwa na mpaka familia zetu zimetususa kila familia kwa shtuma zao tofauti juu yetu.

Familia zetu zilianza kututenga baada ya matatizo kuanza kutuandama mimi na mke wangu.Nyumba yangu na mke ambayo niliijenga na kuihamia siku mbili baada ya kutoka fungate iliwaka moto miezi minne baada ya kuingia na kuteketeza kila kilichokuwepo pamoja na magari mawili tuliyokuwa tumeyapaki wakati huo mimi na mke wangu tukiwa nje ya mji kwa mapumziko.

Maneno yakaongelewa na hata baada ya kuwafafanulia kuwa ni bahati mbaya hakuna aliyeamini. Wakati hilo likiwa halijapoa vibaka walivamia dukani kwetu na kuondoka na fedha na baadhi ya mali na kutokomea.

Taratibu dalili za umaskini zikaanza kuninyemelea na kila nilipojaribu kulitatua hili mara hili likazuka na kuwa lina machungu na maumuvu zaidi ya lililopita hasa ukizingatia ilinibidi nitumie fedha nyingi kulipia mizigo iliyoteketea na hata ile ibiwa.

Nilishikwa na kukaa rumande kwa miezi mitatu baada ya mali fulani kushikwa dukani kwangu nilizozinunua na muuzaji yule ambaye alikuwa akiniletea kwa muda mrefu kumbe nae aliuziwa bidhaa feki ambazo zikatupelekea kudakwa na vyombo vya sheria.

Huku nikiendelea na kuponyesha vidonda hivi na kuanza kutafakari namna mpya ya kujipanga kwa sasa kwani nilishapoteza kila kitu na nahitaji kusimama upya,  ndugu nao wakaanza sasa kumwandama mke wangu kwa kutozaa na kuwa alikuwa ni mkosi kwangu na upande wa kike wakidai mimi nilitumia biashara za kishirikina  na kuwa mke wangu hazai na mimba zake zaharibika kwa kuwa mimi ninazitumia kwa ushirikina ili biashara zangu zifanikiwe.

Kuna mambo yanaumiza sana na kumkatisha mtu tamaa ila hili lilinifanya nifikie kuamini kuwa wanaoweza kukufanya uione dunia mbaya au nzuri huwa ni watu wako wa karibu na nadiriki kusema ni ndugu zako.

Kwa uelewa wangu mke wangu alikuwa akipata msongo wa mawazo kutokana na maisha yetu yalivyokuwa yakizidi kudidimia na ndoto zetu kufifia siku baada ya siku jambo lililopelekea hali yake kuwa tata.

Na pia kuharibika kwa mipango sio sababu ya ndoa bali ni mapito tuu na ni kipindi kama hiki ambacho ndugu wanaojali huweza kuwa karibu nawe sio kwa kukupa fedha ila zaidi kukupa nguvu na ushauri wa kurejea na kuwa vyema zaidi.

Nikakaa na mke wangu na kushauriana na kisha tukufanikiwa kuondoka mji ule na kuja hapa ambako sasa nilianza maisha mapya tena nikiwa mweupe nisiye na kitu mfukoni .Huwezi amini sasa nilikuwa mtu wa kujishikiza hapa na pale ilimradi nipate kula mimi na mke wangu.
Nilifika pale kijiweni na kuona kukiwa na taharuki kubwa  muda huo kwani hakikuwa kijiwe rasmi bali tulikuwa tukikaa pale na kujadili deal za siku hiyo na kupeana miakkati yetu yakuifanya siku au wikun kuwa yenye heri.

Nikiwa sijui nini cha kimetoea wala nini knaendelea mara gari la polis lilisimama pale kwa kasi na tukadakwa watu tuliokuwepo pale na kutupiwa nyumba ya karandinga.

Kila mtualionekana kutokwa na machozi nikiwa nawashangaa mara nami nikaanza kujikuta nikitokwa na machozi bila hata ya kujua nini kinasababisha. Haikupita dakka akili ikanijia nqa kugundua kuwa pale palipigwa bomu la machozi.

Gari liliondoka kwa kasi na kutushushwa kituo cha kati ambapo nilishushwa na wenzangu na kuswekwa mahabusu. Pamoja na kuwa nilitamani kujua nini sababu ya sisi kuw apale lakini akili ilikuwa kwa mke wangu nyumbani kuwa nini kitamtokea ikiwa anajisikia uchungu na kutaka msada.

Tulikaa masaa sita pale kituoni na baadae nilifanikiwa kutolewa kwa mdhamana baada ya rafki yangu mmoja ambaye pia ni polisi pale kuniona na kunitafutia watu kuja kuniwekea mdhamana na kuniacha huru.

Baada ya kumshurukuru nilitimka mbio na kuelekea nyumbani ambapo nilishtushwa kuona michirizi ya damu na mke wangu akiwa hayupo pale nyumbani. 

Akili ya kwanza ilikuwa ni kukumbia kwenda kituo cha afya cha jirani ambako niliambiwa alichjukuliwa na gari la wagonjwa na kukimbizwa hospitali ya rufaa. Niliondoka kwa kasi mpaka pale na nilipofika pale walinisihi niwe mpole kwani alikuwa chumba cha uzazi.

Dakika mbili baadae daktari alikuja akiwa uso chini na kunifanya nianze kuogopa na uniambia kuwa kwa bahati mbaya mtoto amefariki kwa kucheleweshwa na mama amepungukiwa damu hivyo kawekwa drip la damu.

Hakika niliumia na kuona kama kila aina ya furaha ilikuwa ikinitoweka na kuanza kuonja jinsi maisha mapya yenye machungu zaidi yatakavyoanza kwa mimi hasa baada ya kumgoje ahuyu kiumbe bila ya mafanikio.

Saa moja baadae  nikiwa pale lilipita kundi la manesi wakiwa na mtu aliyefariki hata kabla sijauliza au kuhoji zaidi daktari alinifuata na kuniambia kuwa kwa bahati mbaya na mke wangu alituaga dunia.

Nililia kwa sauti kubwa ikifuatiwa na neno SITAKI SITAKI SITAKI kabla ya muda huu kunaswa kibao na bosi wangu hapa ofisini kumbe nilikuwa nimesinzia na kupitiwa na njozi hii ....... kweli  HANGOVER MBAYA 

You Might Also Like

0 comments: