Thamani yako hii hapa somaaaaaaa

14:08:00 Unknown 0 Comments



Leo nimefurahi sana baada ya kuambiwa mambo yako yanazidi kwenda sawa na biashara zako zinaendelea kwenda vyema.

Niliumia sana mara ya mwisho uliponiambia wewe sasa wajiona huna thamani na huoni tena haja ya kuwa mfanya biashara.

Rafiki, kuna siku moja nilipata bahati ya kuendesha mafunzo madogo ya wajasilia mali katika mji fulani.

Nilianza kwa kuwaonyesha bunda la hela ambazo thamani yake ilikuwa zaidi ya 1,000,000/- za kitanzania

Nakumbuka nilizinyanyua juu na kuwaambia kuwa bunda lile lina fedha zaidi ya 1,000,000/- za kitanzania na kuwa nani anazitaka zile fedha.

Watu wengi walinyoosha mikono juu kuashiria wanazitaka zile fedha, nikazichukua na kuzitupa chini na kuanza kuzichafua kwa miguu na viatu vyangu kisha nikazinyanyua tena na kuuliza nani bado anazitaka cha ajabu ni kuwa kila mtu alizitaka tena.

Nikaendelea kuzikanyaga na mwisho pamoja na uchafu wake ule kila mtu alizitaka zile hela kwa kuwa uchafu ule usingeweza kuzishusha thamani fedha zile.

Rafiki, ni mara ngapi katika maisha yetu ya kawaida tunakutana na hali zenye utata au kupitia katika nyakati ngumu, ukachafuka au kuchafuliwa, ukakatishwa tamaa na ukaona kama mwelekeo wako unaisha,lakini kwa kuwa wewe unaitambua thamani yako bado ukazidi kujipa faraja na baadae kuwa mshindi?

Mfano huu wa fedha zilizochafuka na bado zikawa na thamani naomba uzidi kuushika na kuamini siku zote kuwa wewe unathamani na wala hakuna atakayeweza kuzirudisha nyuma jitihada zako..na pia mtegemee mungu akufanye kuwa na thamani zaidi ya fedha kwa kuifanikisha mipango yako.

Wewe una thamani zaidi ya fedha kama utamshirikisha Mungu na naamini utazidi kufanikiwa zaidi.

Kutoka kwa rafiki

You Might Also Like

0 comments: