HAWA NDIO BINADAMU WA SASA.

16:04:00 Unknown 0 Comments



1.wakikukwepa usijali jua kuna siku watakutafuta
2.wakikusengenya nyamaza wenda watajifunza kupitia ukimya wako.
3.wakikununia omba mungu jua kuna siku watakuchekea.
4.wakikupongeza usiwaamini sana wenda wakawa wanakutania.
5.wakikutenga achana nao jua wao sio kila kitu katika hii dunia.
6.wakikudhulumu shukuru mungu ipo siku atakulipa.
7.wakikualika kuwa makini wenda kuna kitu wanakutegea.
8.wasipokupenda usijisumbue kujipendekeza
JUA MUNGU NDIO RAFIKI WA KWELI KATIKA DUNIA NA SI BINADAMU

11 people reached
Karibu Mbeya shared a link.
Posted by Fred Kihwele · 24 minutes ago
CHUO CHA DIGITAL MEDIA COLLEGE OF TANZANIA (DMCT) KINATANGAZA KOZI ZA COMPUTER (COMPUTER APPLICATIONS COURSE).
1. PROGRAMS UTAKAZOSOMA:-
1. Microsoft Word. 2. Microsoft Excel.
3. Microsoft Publisher. 4. Microsoft Power Point.
5. Microsoft A... See More
9 people reached
Like ·  · 
Facebook ilivyonikosesha raha 9

Ilikoishia jana

Au ana ajenda ya muhimu na maisha yangu na wenzangu? ndio hapa nilipo anza kufikiria kama kuna mtu nilishamkosea au kumfanya aumie na labda anataka kulipa kisasi.
... See More
Photo: Facebook ilivyonikosesha raha 9

Ilikoishia jana

Au ana ajenda ya muhimu na maisha yangu na wenzangu? ndio hapa nilipo anza kufikiria kama kuna mtu nilishamkosea au kumfanya aumie na labda anataka kulipa kisasi.

Nikiwa katika dimbwi hilo la mawazo nikapokea ujumbe ulionishtua zaidi kupitia namba yangu ya simu ukisema, "............................

Endelea

Nikiwa katika dimbwi hilo la mawazo nikapokea ujumbe ulionishtua zaidi kupitia namba yangu ya simu ukisema,

" Fred, sasa ni muda ambao unatakiwa kuujua ukweli kuhusu maisha yako na kutoka katika kifungo chako. Nenda nyumbani kwako na chini ya kitanda chako cha kulala utaona kitu"

Niliondoka eneo hilo haraka na kwenda mpaka nyumbani na niliingia moja kwa moja mpaka chumbani na kukutana na kitu cha ajabu sana chini ya godoro.

Huwezi amani niliiona sanda ambayo inaonesha kuwa ilitumika na kama haitoshi ilikuwa na maneno fulani yenye lugha iliyoandikwa kwa kiarabu.

Nilifunika haraka na kwa utaratibu ili mke wangu mama segito asigundue kitu na kiukweli nguvu ziliniisha na ni kwa mara ya kwanza nilijikuta nikichukua biblia na kusoma baadhi ya vifungu ingawa hofu ilinitanda zaidi na kuondoka mara moja.

" Pale nyumbani naishi mimi na mke wangu na mwanetu mmoja tuu, sasa ni nani anaweza kufanya mambo yale bila ya mimi kufahamu? au mke wangu kaanza kufanya mambo ya kishirikina?" Nilihoji wakati huo nikipiga kiroba cha nne bar moja maarufu jirani na nyumbani ambako niliamua kwenda kwa muda.

NIlirudi nyumbani kwangu nikiwa nimelewa sana na huwezi amini mke wangu alishangaa sana kwani ilishapita miaka kama miwili tangu niachane na kunywa kilevi cha aian yoyote ile.

Usiku wa siku hiyo haukuwa mfupi kwani kila nilipotaka kupata usingizi uliochanganyika na viloba bado nilishindwa nikikumbuka sanda na mauzauza niliyokutana nayo kwa siku kadhaa zilizopita.

Asubuhi niliamka na kumtegea mke akiwa bafuni na kuichukua sanda ile na kutokomea kwa ally ambaye alinitafsiria maneno yale ambayo yote kwa pamoja yalisomeka "UMASKINI, UMASKINI, UMASKINI"

Swali langu kuu likawa, je umaskini huo ni wa nini na kwa nani? ally akanijibu kwa kifupi tuu kuwa kaka hii kitu imenuiwa kwako hivyo unatakiwa kufanya mapema kuitoa au kuna kubwa lakujia.

Nitaanza kwa nani kuuliza juu ya hilo, na je nimuulizeje mama segito ili swali langu lisiweze kumfanya aumie na kusononeka kama yeye sio mhusika mkuu? nilijiuliza swali hili na kisha nikaondoka pale kwa ally na kurudi kwangu.

Nilimkuta mama segito akiwa kapika chakula na ananisubiri ili tule pamoja. kwa uchovu nikakaa kwenye kochi na kumwomba nisile muda huo jambo lililomshangaza sana mama segito.

Ulipita muda wote tukiwa kimya na kisha nikaona nivunje ukimya na kumwambia, " mama segito mke wangu, naomba nik..................................................

Nitaendelea kesho mida kama hiii, unaruhusiwa kutembelea www.karibumbeya.com kwani ndio mdhamini wangu

http://karibumbeya.com/ads/facebook-ilivyonikosesha-raha-sehemu-ya-9/
474 people reached
35 people reached
Like ·  · 

You Might Also Like

0 comments: