Jinsi nyumba ndogo tarajiwa ilivyonipa wakati mgumu
14:43:00
Unknown
0 Comments
14:43:00 Unknown 0 Comments
Nilimwacha mke wangu akiwa na ujauzito mdogo na kwenda zangu masomoni kwa muda wa miezi kadhaa nje ya nchi.
Lakini kabla ya kuondoka tulikubaliana tumtafute binti mmoja wa kazi ili wasaidiane pale nyumbani hasa ukizingatia hali yake kwa muda huo nikiwa sipo.
Akapiga simu kijijini kwa rafiki yake ambako mie sikutaka sana kufuatilia na tukabahatika kumpata dada mmoja aliyemaliza shule ya kata na kupata matokeo mabovu na kuona atusaidie kwa makubaliano ya kumwendeleza kimasomo.
Alikuwa binti mchafumchafu na wakawaida sana kiasi cha kuona hata kuwa na madhara yoyote kwangu wa kwa wadogo zangu pia wa kiume ambao wako chuoni na huja mara kwa mara.
Nikaondoka na kwenda masomoni na kwa bahati nzuri nikapewa offer ya kukaa mwaka mmoja na nusu.
Siku narudi mke wangu alikuwa kasafiri kwenda kijijini hivyo akaja mdogo wangu Salome akanibeba na kunipeleka nyumbani kisha akarudi zake hostel.
Nilionana na mgeni mmoja pale ndani ambaye akaanza kuumiza akili yangu, ikanibidi nimuulize kuwa yeye ni nani?
Mama yangu!!!, mama yangu!!! kumbe bwana ni yule mtoto namaanisha binti wa kazi kavaa pensi yake, kapita saloon , shape ile na usafi na mwili wake ukaanza kunipa maswali.
Nikajiuliza kuwa imekuaje kabadilila haraka vile? Lakini nikapiga moyo konde na kusema hebu niache ujinga na tamaa kwanza mke wangu mzuri zaidi.
Usiku ule nikawahi kulala na asubuhi nikawahi zangu pale posta kuna kampuni moja niliagizia mizigo yangu sasa nikataka kuichukua kisha kuipeleka nyumbani na baada ya hapo nilaelekea kupata moja baridi moja moto mida kama ya saa kumi za jioni.
Usiku baada ya kurudi nilimwangalia Mayasa (dada wa kazi) kwa ukaribu zaidi nikaona no way ngoja nimwage radhi na kumpa ukweli.
Binti akakataa na kusema mke wangu ni zaidi ya dada kwake na kamfanyia makubwa hivyo hatataka nifanye lolote zaidi ya kuniheshimu kama kaka.
Juhudi za kumbembeleza hazikuambulia chochote zaidi ya mimi kwenda kulala.
Siku ya pili sikutoka ndani na nikaanza kujilaumu kwa nini jana nilifikia uamuzi ule kabla ya kuamua kutoka nje na kwenda kutembea maana alipita pale sebuleni kavaa kanga moja na anaelekea chumbani akiwa katoka kuoga nikaona naweza pata kesi.
Jioni ya siku ile mashetani ya kikinga yakanipanda na kweli nikafanikiwa kutembea na mayasa ingawa alionekana kuhuzunishwa na uamuzi wangu ila akawa hana cha kufanya zaidi ya kusema kaka nakuambia kwa hili utajuta.
Mimi binafsi maneno yale hayakunitisha zaidi ya kujiona mimi ni mjanja wa wajanja mzee wa kutoshindwa.
Nikakaa kama siku nne hatuongei, kilichonifanya niongee nae ni baada ya nguo zangu za ndani nilizozianika bafuni kwangu kupotea na nilipomuuliza mwanzo hakujibu ila baada ya kukumbuka hatukuongea nae tangu siku ya lile tukio jasho likanianza.
Nikapekua chumbani mwake nakukuta nguo yangu moja ya ndani ipo kwenye begi lake kaifunga na kitambaa chekundu na kuna nywele ndani.
Nikaanza kuogopa kwani jana yake asubuhi nilifanya usafi wa maeneo yangu nyeti na sikusafisha bafu kwani nilikuwa nawahi apointimenti mjini.
Nikamwita pale ndani na akasema ni kweli alichukua yeye na zile nyingine, nikauliza kwa nini kaweka kwenye kitambaa chekundu na nywele katikati???????
Akadai babu yake alimkataza asifanye mapenzi na mtu yoyote mpaka awe amemlipia mahari na kufunga naye harusi au la sivyo moto utawaka.
Sasa ameweka wapi zile nyingine?????? Akadai kashazituma kwa babu yake huko kijijini kwao.
Nikaondoka pale haraka nusura nipande gari nikiwa na taulo kama yeye hakunikumbusha kwa kusema mbona wataka kuondoka na haujavaa suruali?
Baada ya kubadilisha nguo niliwasha gari mpaka bar moja na kupata bia na kisha kumuuliza mke wangu kuwa hausi geli huyu anatokea wapi vile? Akanijibu ni Sumbawanga....... Kwani vipi baba shamsa?????????
Nikasema kwa kufoka hawezi kuwa na uchawi toka huko kwao????? Maana analea mtoto wetu kumbuka?????
Akasema hakuna kitu, lile jina la sumbawanga tu likanifanya niiache ile pombe na kuanza kufikiria nini kitafanyika kuzichukua zile boxer zangu kwa babu yake.
Nikarudi nyumbani kiupole na kumwomba anisamehe akadai kuwa anamsubiri dada yake yaani mke wangu arudi na kisha ampe ukweli juu ya lile ili asilaumiwe kwa litakalonitokea.
Mwanaume nikaanza kuona kama ni biti basi limenikaa na sasa issue ya wife tena?????? Nikamwambia dada usitake nikufunge sasa hivi nipe vitu vyangu.
Kwa upole akasema nitaomba utufunge mimi na babu maana na wewe tayari uko kifungoni bila ya kujua ni sekunde tu uanze kuipata fresh yake......
Yale maneno yaliniingia na nikaanza kuona kama nimeshakuwa msukule nikaingia ndani na kupitiliza chooni ambako nilikaa dakika zaidi ya kumi hakuna kitokacho nikahisi babu kashaanza kazi yake.
Siku ya pili mke wangu akawa karudi na wote tukawa tumefurahia ujio wake na kwa kuwa hatukuwa tumeonana muda mrefu tukatoka out familia nzima.
Kila muda nilionekana kuwa mkimya na mwenye mawazo tofauti na nilovyo na kuna kipindi nilitamani kumwambia mke wangu aliki nikashindwa.
Siku ya pili dada akaniambia kuwa kaongea na babu yake kasema nimwambie nina mpango gani naye mayasa au aendelee na taratibu zake.
Sikuwa na jinsi nikampa laki tano baada ya wiki mayasa akanipa bahasha ikiwa na zile hela zangu na zimefungwa na hizi na maneno ndani kuwa hizo hela zinaweza kufanya nini kwa maisha ya sasa?
Nikatafuta sehemu na kumfungulia fremu na kumpa biaahara ya vipodozi na saluni ndio baada ya hapo akahamia huko kwa siri na mke wangu hakujua.
Baada ya kukaaza zaidi ya mwaka na miezi kadhaa sasa amani yangu na familia imerudi kwani sina vitisho tena.
Mbaya zaidi nimekuja kumgundua hakuwa na ushirikina wowote zaidi ya kunipa presha nimekoma na sitaki kuwasikia mabeki tatu tena.
Kweli nilimwona mchafumchafu kumbe kichwani zipo.....duh
Yes, You are in Mbeya!
KARIBUMBEYA.COM
Fuledi Mwagito
Nakushukuru kwa kunipa nafasi hii adimu sana ya kufurahi, kuelimika na kubadilishana mawazo. Nitafurahi sana kama utaniachia comment hapo chini ili nijue kama habari,ucheshi, simulizi na vioja vioja hivi vimekupa siku yako kuwa BOMBA. Kumbuka nawe waweza share nami chochote ulichonacho kwa kunicheki kupitia whatsapp kwa namba 0713317171 au kupitia comment. Asante.
0 comments: