Kamwe sitasahau siku nilipozifuma ARV kwenye mkoba wa mpenzi wangu......

16:27:00 Unknown 0 Comments



Mwaka wa kwanza pale chuoni sikuona umuhimu wa kuwa na binti na jitihada zangu zote zikawa darasani hasa ukizingatia bado nilikuwa na usongo wa kusoma na mawaidha ya wazazi bado yapo kichwani na ule usekondari haujanitoka.

Wenzangu wao walikuwa na mademu zao na wakawa wanaishi maisha ya mme na mke mie nikawa naona hiyo sio sahihi kwangu, muda mwingi niliutumia darasani, library, kanisani na uwanjani.

Mwaka wa pili nikajiona naanza kupunguza msimamo hasa baada ya kontena jipya kushuka na mabintiwa mwaka wa kwanza kuwa wazuri wa kupindukia.Nikajichagulia nimtakaye na kisha nikaanza kufukuzana nae.

Binti yule aliumbika kwani kila kitu utakachobahatika kukiona katika mwonekano wake basi lazima ungekubaliana na mimi kuwa alikuwa mzuri. Na nilimpenda zaidi ya yote jinsi alivyoonekana kuwa mpole na mwenye kujiheshimu.

Nilimfuatilia kwa zaidi ya miezi minne bila ya mafanikio na hakuwa na jipya zaidi ya kusema sitaweza kuwa na wewe kwani ninahitaji kuwa peke yangu na nina kitu kinachonifanya niwe na maamuzi hayo, wewe ni mzuri wa kuvutia ila nielewe.

Cha kushangaza hakuwa na mpenzi yoyote yule na alipenda sana kuwa na mimi hasa nyakati za weekend na kweli nikafurahia kuwa nae ingawa hakutaka uhusiano ule uwe zaidi ya hapo na kweli alikuwa na msimamo katika hilo.

Siku moja weekend nikamshawishi twende zetu sehemu moja ambako kuna hoteli nzuri ya kitalii ambayo pia ilikuwa ina bar yenye vinywaji aina mbalimbali na pia kila aina ya burudani.

Nikanunua wine na kumwomba naye anywe akagoma na baadae akainywabaada ya kuona kuwa niliumia kwa yeye kukataa.Maskini!!! kumbe hakuwa na uzoefu nazo, hivyo zikamchukua nami nikautumia mwanya huo kutimiza ndoto zangu na tukalala pale mpaka siku ya pili yake.

Asubuhi dada aliumizwa na kitendo kile na kusema sikufanya vyema na akauliza kama nilitumia condom nikasema hapana basi kuanzia pale tukawa sasa kama wapenzi baada ya kuomba msamaha na kukubalika.. ingawa kile kitendo kilionekana kumchukiza.

Tuliendelea kuwa wapenzi na kila mtu akalifahamu lile na kunionea wivu pale hostel na darasani pia.Nikawa pale chumbani kwake niko huru kama kwangu naweza kupekuwa chochote na kukitumia.

Siku moja baada ya kupita miezi mitatu nikawa nahitaji kitabu changu kimoja nilichompa na yeye wakati huo akawa yupo mjini. Nikaingia chumbani kwake na kuanza kupekua kabla ya kukutana na box dawa aina ya ARV.

Nilishtuka sana na kujipa matumaini kuwa labda sio zake lakini hapo hapo nikakumbuka kuna zaidi ya mara tatu nimeshawahi kumsindikiza kituo kimoja cha ushauri nasaha na akawa akiniacha hotel jirani na kwenda kule akidai kuna mjomba wake yuko pale sio vizuri anione.

Nikapanda gari mpaka pale nikaulizia nikaammbiwa kuwa pale ni kituo cha ushauri nasaha na pia  huwa wanenda wagonjwa wa ukimwi kila mwezi pale kupata dawa za kupunguza makali ya virusi. Sikuongeza neno nikaondoka mpaka nyumbani kwangu na kulala huku akili ikiwa imesizi kabisa.

Sikuweza kupata hata hamu ya kuhudhuria vipindi na kila rafiki aliyenitafuta sikumjibu vizuri mpaka walipoamua kuja nyumbani na kuniona nimebadilika yaani kwa wiki lile nimeshaanza kukonda.

Hakuna aliyejua nini kinaendelea na hata mpenzi wangu naye hakujua ni nini kinaendelea na baada ya kuona maswali kutoka kwa rafiki yamezidi nikaamua kuondoka zangu na kurudi mbeya.

Huku nako baba na mama na wengine wakawa wananiuliza kwa nini nimerudi mapema na kama haitoshi wakaanza kuhisi kama nina umwa vile na mama akawa akizidi kunisihi juu ya ukimwi na kuwa mwangalifu wa maisha yangu na mienendo yangu... Nikaona na nyumbani sasa hakufai.

Nikaanza kujiona kama vile dunia inaanza kunipa kisogo na kama haitoshi kila nikifikiria plan zangu na hata ndoto zangu na nikiona wenzangu wanavyofurahi mimi nikaona sina jipya zaidi ya kufa tuu.

Nikarudi chuo na kuonana na rafiki yangu aitwaye Fred na nikawa sina namna zaidi ya kumsimulia kwani nilishajiona kama ni mfu.Fred akaniambia ni suala dogo sana kwani bado sina uhakika natakiwa nipime ili nijue kuliko kuendele akukaa na mawazo.

Kumbe Fred bila kunishirikisha akaenda kwa dokta mmoja na kumwambia wanipime na hata kama nina maambukizi nisiambiwe kwa muda ule kwani tayari nilishakuwa katika hali mbaya ningeweza kujiua au kufanya lolote lile.

Siku chache baadae nikaenda kupima na dokta akasema, " Fred hata kama uliniambia nikimkuta na maambukizi rafiki yako nisiseme, lakini kiukweli ni kwamba hana maambukizi yoyote"

Niliruka kwa furaha na kurudi chuoni kuendelea na masomo huku nikimshukuru Mungu kwa kuniepusha na janga lile.Sasa nimeokoka na yule mpenzi wangu sasa ni rafiki na tunaishi nae kama ndugu.

Nimejifunza kuwa sio vizuri kung'ang'ania mambo pale binti anaposema haitaji kuwa na mtu ni vyma kuelewa kuliko kutumia njia ambazo zinaweza kukupa wakati mgumu zaidi ya huu nilioupitia mimi.

Kama imekupa kitu share nami nitakuombea kamwe usipatwe na mikasa kama hii

Amen



16 people reached

You Might Also Like

0 comments: