Maskini ya mungu
12:00:00
Unknown
0 Comments
12:00:00 Unknown 0 Comments
Facebook ilivyonikosesha raha
Huwa sio kawaida yangu kumwamini mara moja rafiki yoyote yule kwa njia ya mtandano, lakini nilishaangaa na kamwe siji amini ni kitu gani kili nisibu mpaka nikajikuta natumbukia katikaq janga hili.
Ni ngumu kuisimulia kutokana na maumivu yake lakini sina jinsi nitasimulia hata kama najua haitakuwa suluhu ya mimi kupata ahueni na kulifuta kichwani mwangu.
Ilikuwa ni ijumaa moja majira ya saa nne kasoro za asubuhi miaka kama miwili iliyopita nikiwa katika harakati za kukimbizana na majukumu yangu ya kazi nilipokea notification kuwa kuna mtu ameni POKE
Ok, mimi kwa uelewa wangu mdogo nikagundua kuwa poke ni sawa na kumtekenya mtu hivyo haraka nikaona nimwangalie mhusika. Kweli nikapelekwa mpaka kwenye akaunti ya aliye ni-poke na jina moja la mwanzo lilisomeka COLETHA.
Haraka nikaanza kumchunguza na nikagundua ni binti mmoja ambaye hakika ana uzuri wa kupindukia. Unajua tena mwanaume ukishaona binti mrembo, hips hizo, mara selfie kibao na mtoto ana ule vuto wa kitanzania, huwa hakuna unjanja zaidi ya kubonyeza ADD FRIEND.
Huwezi amini haikuchukua hata dakika binti akawa kanikubali na baada ya hapo mazungumzo ya inbox yakaanza kupamba moto. Kuna wakati hata kama unakiburi ni lazima ukubali kuwa kuna watu wana lugha taamu zenye kukufanya hata akikosa kukujibu text kwa sekunde kadhaa lazima moyo ukupasuke na ukiipokea text yake basi lazima upoteze usikivu.
Tulichati sana siku hiyo na nakumbuka ikafikia wakati hata niliporudi nyumbani kila mtu aligundua nilikuwa busy sana siku hiyo na simu tofauti ya hapo awali.
Mawasiliano yetu yaliendelea na nakumbuka wiki ya pili yake yaani jumatatu alinitumia text kuwa alitaka kuniona na kuwa sasa ananipa apointment ya mimi na yeye kukutana jumamosi ya week hiyo.
Kwa picha alizokuwa akinitumia na jinsi alivyonipagawisha kwa text zaidi ya wiki ya kwanza ile tuliyofahamiana naye yaani ijumaa nikawa situlii kumwomba Mungu angalau siku zisonge mbele fasta niweze kwenda kukutana nae.
Jumamosi ilivyofika nikaamka mapema na kuwahi ofisini ili nimalize majukumu yangu mapema na niweze kwenda kwa binti Coletha.
NIliwasili mapema kabla yake eneo la miadi na nilipofika pale mhudumu alinifuata na kuniambia kama mie ni mgeni wa Coletha na nikamkubalia kwa kutikisa kichwa na baada ya hapo akanichukua mpaka alipokuwepo Coletha.
Ile naufungua mlango niweze kumwona yule binti moyo wangu ulinipasuka na kujikuta.............................................................
Nitaendelea kesho mida kama hiii, unaruhusiwa kutembeleawww.karibumbeya.com

Fuledi Mwagito
Nakushukuru kwa kunipa nafasi hii adimu sana ya kufurahi, kuelimika na kubadilishana mawazo. Nitafurahi sana kama utaniachia comment hapo chini ili nijue kama habari,ucheshi, simulizi na vioja vioja hivi vimekupa siku yako kuwa BOMBA. Kumbuka nawe waweza share nami chochote ulichonacho kwa kunicheki kupitia whatsapp kwa namba 0713317171 au kupitia comment. Asante.
0 comments: