Mke gaidi kuliko wote Tanzania
Jamaa mmoja alianza kupatwa na hofu kuwa mkewe hana tena mapenzi ya dhati zaidi ya kupenda pesa na mali zake.
Basi jamaa akatumia triki na kujifanya anaumwa na kukaa nyumbani kwa wiki zima na ilipofika weekend jamaa akajifanya homa imezidi zaidi.
Jumapili mchana mama akiwa katoka kanisani na mzee yupo pale chumani akaanza kulalalamika kama mtoa roho anamfuata vile na kisha kweli akakata roho.
Mke akataka kupiga kelele ila akajishtukia na kukaa kimya kwanza, wakati huo mme kaimisha pumzi na anamchungulia mke anafanya nini.
Mke akaanza kupekua kabatini akachukua kadi za magari, nyumba na documents zote za muhimu na kuzificha.
Akaenda sebuleni na kuhamisha baadhi ya vitu muhimu na kuvificha chumbani , akamalizia kupika chakula akala akaoga.
baada ya hapo akaanza kupiga kelel ili watu waje, baadhi ya ndugu walipofika na watu wengine mme nae akaamka na kuwapa watu mkanda mzima.. Mpaka mida hii mke kasharudi kwao huko sigimbi
Mbaya sana
0 comments: