Mme wangu anataka niache kazi nibaki nyumbani
Swali kutoka kwa rafiki wa Tabasamu na Fuledi na mteja wa Karibu Mbeya
Mimi ni mwanamke wa miaka 28, nimeolewa na nimebahatika kuwa na mtoto mmoja.
Ndoa yangu ilikuwa na furaha sana ila imegeuka na kuwa tatizo kwani mme ana wivu kiasi cha kwamba anataka aniachishe kazi nikae nyumbani.
Pia hataki niwe na simu wala kuwasiliana na watu nikae ndani tuu nilee mtoto.
Jamani naombeni ushauri wenu nifanye nini?
Nimechanganyikiwa na nahitaji msada wa mawazo
0 comments: