Pete ya diamond yazua balaaaa jijini mbeya

16:27:00 Unknown 0 Comments



Binti mmoja ambaye aliolewa na kijana mmoja wa makamo na ambaye alikuwa na utajiri mwingi sana,  alikuwa anategemea kupata zawadi kutoka kwa mmewe kwani alikuwa anakaribia kuadhimisha  siku yake ya kusherehekea miaka yake ya kuzaliwa.

Kwa muda mrefu alikuwa akitamani pete moja ya almasi iliyokuwa katika showroom moja ya duka moja maarufu sana la kuuzia vitu vya thamani .Binti aliamini mmewe angeweza kuinunua kwani kwa utajiri wake ilikuwa ni fedha kidogo sana. Yeye aliitamani zawadi hiyo ya pete tu na sio nyingine kutoka kwa mmewe kipenzi.

Siku ya birthday ikawa inakaribia na yule binti akawa anasubiri kila dalili za kuipata ile zawadi, na hatimaye siku ikafika. Asubuhi ile yule mme akamwita mkewe chumbani mwao na akamwambia jinsi alivyokuwa na bahati kwa kuwa na mke mzuri na mwema kama yule na jinsi alivyokuwa akimpenda kwa dhati.
Baada ya maneno yale mme akachukua box dogo lililopambwa vizuri na kumpa mkewe .Mkewe akiwa na hamu ya kujua nini kipo mle ndani akaifungua bila kuchelewa na kukuta BIBLIA iliyofungwa vizuri ya yenye kava zuri la ngozi nje yake na lenye  jina lake lilioandikwa kwa dhahabu.

 Yule mke kwa hasira akapiga kelele na kumwambia, “yaani pamoja na hela zote ulizonazo,  uliona BIBLIA hii ndio zawadi ya kunipa mimi katika siku muhimu kama hii???” kisha kwa hasira akachukua vilivyo vake na kuamua kuondoka pale nyumbani na kwenda kuanza Maisha ake akiwa na mwane.
Miaka mingi ikapita na yule mke akawa kajiimarisha ana nyumba yake nzuri na biashara zake na akiishi na mme mpya na familia yake wakati yule mme wake wa zamani alikuwa keshazeeka sana. Siku moja Yule mke akaamua apange kwenda kumtembelea  mme wake wa zamani kwani hawajawasiliana nae kwa kipindi kirefu sana tangu aondoke.

Hata kabla ya siku ya kwenda akapokea ujumbe kuwa mme wake wa zamani amekufa kwa ajali mbaya ya gari na kwa kuwa walikuwa wameoana na wana mtoto mmoja mme aliandika urithi wote uende kwa yeye na mtoto wao. Hivyo mama akaamua awahi kwenda ili akachukue mali hizo.

Alipowasili katika nyumba yao ya zamani, ghafla huzuni na machozi yakaanza kumdondoka akakumbuka Maisha yao na kuamua kuzunguka vyumbani kuangalia vitu muhimu na kuiona ile BIBLIA bado mpya kama alivyoiacha miaka mingi iliyopita.

Huku machozi yakizidi kumtoka akaanza kuifungua ile BIBLIA kila ukurasa na kuona mmewe aliupigia mstari  huu Matt 7:11, Ambao ulisomeka  “Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?”

Akiwa anaendelea kusoma kabahasha kadogo kakaanguka na alivyofungua alilia kwa sauti kuona ni Pete ya almasi kama ile aliyoipenda ikiwa imeandikwa jina lake na maneno kwenye bahasha NAKUPENDA MKE WNGU KIPENZI.

Ni mara ngapi tunakosa Baraka za MUNGU kwa sababu zinakuja tofauti na sisi tulivyotaka?

 Funzo

Usiharibu kile ulichonancho sasa kwa kile unachokitaka
Kumbuka ulichonacho sasa pia ni moja kati ya vitu ulivyoviomba na kuvitarajia

Daima pokea vitu kwa kusema asante hata kama ni vidogo, huwezi jua nini kipo au kitakuja kupitia hivyo


11 people reached
Karibu Mbeya shared a link.
Posted by Fred Kihwele · 42 minutes ago
CHUO CHA DIGITAL MEDIA COLLEGE OF TANZANIA (DMCT) KINATANGAZA KOZI ZA COMPUTER (COMPUTER APPLICATIONS COURSE).
1. PROGRAMS UTAKAZOSOMA:-
1. Microsoft Word. 2. Microsoft Excel.
3. Microsoft Publisher. 4. Microsoft Power Point.
5. Microsoft A... See More
9 people reached
Like ·  · 
Facebook ilivyonikosesha raha 9

Ilikoishia jana

Au ana ajenda ya muhimu na maisha yangu na wenzangu? ndio hapa nilipo anza kufikiria kama kuna mtu nilishamkosea au kumfanya aumie na labda anataka kulipa kisasi.
... See More
Photo: Facebook ilivyonikosesha raha 9

Ilikoishia jana

Au ana ajenda ya muhimu na maisha yangu na wenzangu? ndio hapa nilipo anza kufikiria kama kuna mtu nilishamkosea au kumfanya aumie na labda anataka kulipa kisasi.

Nikiwa katika dimbwi hilo la mawazo nikapokea ujumbe ulionishtua zaidi kupitia namba yangu ya simu ukisema, "............................

Endelea

Nikiwa katika dimbwi hilo la mawazo nikapokea ujumbe ulionishtua zaidi kupitia namba yangu ya simu ukisema,

" Fred, sasa ni muda ambao unatakiwa kuujua ukweli kuhusu maisha yako na kutoka katika kifungo chako. Nenda nyumbani kwako na chini ya kitanda chako cha kulala utaona kitu"

Niliondoka eneo hilo haraka na kwenda mpaka nyumbani na niliingia moja kwa moja mpaka chumbani na kukutana na kitu cha ajabu sana chini ya godoro.

Huwezi amani niliiona sanda ambayo inaonesha kuwa ilitumika na kama haitoshi ilikuwa na maneno fulani yenye lugha iliyoandikwa kwa kiarabu.

Nilifunika haraka na kwa utaratibu ili mke wangu mama segito asigundue kitu na kiukweli nguvu ziliniisha na ni kwa mara ya kwanza nilijikuta nikichukua biblia na kusoma baadhi ya vifungu ingawa hofu ilinitanda zaidi na kuondoka mara moja.

" Pale nyumbani naishi mimi na mke wangu na mwanetu mmoja tuu, sasa ni nani anaweza kufanya mambo yale bila ya mimi kufahamu? au mke wangu kaanza kufanya mambo ya kishirikina?" Nilihoji wakati huo nikipiga kiroba cha nne bar moja maarufu jirani na nyumbani ambako niliamua kwenda kwa muda.

NIlirudi nyumbani kwangu nikiwa nimelewa sana na huwezi amini mke wangu alishangaa sana kwani ilishapita miaka kama miwili tangu niachane na kunywa kilevi cha aian yoyote ile.

Usiku wa siku hiyo haukuwa mfupi kwani kila nilipotaka kupata usingizi uliochanganyika na viloba bado nilishindwa nikikumbuka sanda na mauzauza niliyokutana nayo kwa siku kadhaa zilizopita.

Asubuhi niliamka na kumtegea mke akiwa bafuni na kuichukua sanda ile na kutokomea kwa ally ambaye alinitafsiria maneno yale ambayo yote kwa pamoja yalisomeka "UMASKINI, UMASKINI, UMASKINI"

Swali langu kuu likawa, je umaskini huo ni wa nini na kwa nani? ally akanijibu kwa kifupi tuu kuwa kaka hii kitu imenuiwa kwako hivyo unatakiwa kufanya mapema kuitoa au kuna kubwa lakujia.

Nitaanza kwa nani kuuliza juu ya hilo, na je nimuulizeje mama segito ili swali langu lisiweze kumfanya aumie na kusononeka kama yeye sio mhusika mkuu? nilijiuliza swali hili na kisha nikaondoka pale kwa ally na kurudi kwangu.

Nilimkuta mama segito akiwa kapika chakula na ananisubiri ili tule pamoja. kwa uchovu nikakaa kwenye kochi na kumwomba nisile muda huo jambo lililomshangaza sana mama segito.

Ulipita muda wote tukiwa kimya na kisha nikaona nivunje ukimya na kumwambia, " mama segito mke wangu, naomba nik..................................................

Nitaendelea kesho mida kama hiii, unaruhusiwa kutembelea www.karibumbeya.com kwani ndio mdhamini wangu

http://karibumbeya.com/ads/facebook-ilivyonikosesha-raha-sehemu-ya-9/
482 people reached
35 people reached
Like ·  · 

You Might Also Like

0 comments: