BAADHI YA MWASWALI KWENYE INTERVIEW NA JINSI YA KUYAJIBU

10:30:00 Unknown 0 Comments


1. Hawa referees kwenye CV yako, yupi kati yao
alikuwa wa kwanza kupanda ndege na alilipa sh
ngapi?


2. Hii CV yako kwanini huku i-print kwenye manila
paper?


3. Ni tusi gani ambalo ukitukana unajisikia ahueni,
baada ya kuambiwa umekosa nafasi ya kazi
uliyoiomba?


4. Tunaweza kupata uhakika gani kuwa hauta
mtamani secretary wa bosi


5. Hichi Chumba Kinajaa Lita Ngapi za Maji?


6. Vipi shwari, una fegi hapo?


7. Unahisi muda huu tunapoongea simu ya raisi
wa nchi ina salio kiasi gani?


8. Robin Van persie ni Mgogo au Mhehe?


9. Ubongo Wako Una GB ngapi?


10. Kwa nini lile sanamu la posta mbona haliendi
vitani?


UKIJIBU HAYA UKAKOSA KAZI UJUE UNA MKOSI
KULIKO SHETANI


Karibu Mbeya shared a link.
Posted by Fred Kihwele · 22 hours ago
Advertising Mbeya, ni jarida linalomilikiwa na kampuni ya Jukwaa Huru Media, likiwa ni jarida mahususi la matangazo kwa biashara zilizopo katika mkoa wa Mbeya
258 people reached

Facebook ilivyonikosesha raha 12

Ilikoishia jana

Kakaaa, Hata kabla ya kumaliza kusema neno kaka vizuri simu ilikatwa na hapo sasa hasira ikanipanda na kusema sasa naenda kuchukua ile sanda chini ya kitanda na kwenda kumpelekea kaka na ku... See More
Photo: Facebook ilivyonikosesha raha 12

Ilikoishia jana

Kakaaa, Hata kabla ya kumaliza kusema neno kaka vizuri simu ilikatwa na hapo sasa hasira ikanipanda na kusema sasa naenda kuchukua ile sanda chini ya kitanda na kwenda kumpelekea kaka na kuwaambia ukweli.

Niliingia chumbani kwa hasira na nilipofunua kile kitanda nilichokisusa kutokana na kuona ile sanda nilishtuka kuona.............................

Endelea

Niliingia chumbani kwa hasira na nilipofunua kile klitanda nilichokisusa kutokana na kuona ile sanda nilishtuka kuona ile sanda imetoweka.

Hapa sasa suala la ushahidi likawa halipo na wazo la haraka likanijia kuwa niende mpaka nyumbani kwa shemeji yangu ili niweze jadiliana nae kwa undani.

Huwezi amini nilipofika pale nilitimuliwa kama mbwa tena yule mbwa koko. Sikutaka kubishana hivyo nikarudi mpaka kwa ally nikakutana nae na kumpa maendeleo yangu na nini kinaendelea.

Ally akanipa nguvu kwa ushauri wake na kudai nimsubiri kidogo ajiandae na anisindikize mpaka hospitali ili tukaone hali ya mama segito.

Tuliondoka pale baada kama ya nusu saa na kuelekea hospitali ambako tulikataliwa kuingia kwa madai mgonjwa hataki mtu aingie ndani anahitaji kupumzika.

Kauli hii ilinishangaza sana lakini kwa kuwa najali na uhuru wa nafsi ya mama segito nikaona ni vyema tuondoke na ally  akanishauri kuwa nisipanic ila niwe mpole mambo yote yataisha.

Tukiwa njiani ally akaniomba nimsindikize mjini kwani alikuwa na ahadi ya kuonana na dada mmoja hivyo nimpe kampani kwa kuwa nae huko.

Tulifika eneo la tukio na dakika mbili tatu kuna gari moja likapaki pale bustanini tulikokuwa tumekaa na akashuka dada mmoja niliyemtambua kabisa kuwa ni coletha.

Nilishtuka na kumvuta haraka ally mpaka chooni bila ya coletha kutuona na kumwambia kaka huyo unayetaka kukaa nae hapo ni hatari kaka, lakini ally alikuwa mbishi na hata nilipojaribu kumlazimisha anielewe niliishia kupokea vibao vya mashavuni kuwa ninataka kumwingilia uhuru wake.

Aliondoka na kuniacha nikiwa nimeinama pale na taratibu niliondoka zangu kupitia mlango wa nyuma na kutokomea.

Kwa kuwa hali ilikuwa sasa ni moto nikaona niende mpaka kijijini kwa mama mkwe kilomita kama 20 tu kutoka mbeya mjini. Nilifanikiwa kufika huko baada ya kukodi bodaboda.

Ile naingia mlangoni kwa mama mkwe nilishtushwa na ..................

Nitaendelea kesho mida kama hiii, unaruhusiwa kutembelea www.karibumbeya.com kwani ndio mdhamini wangu

Soma visa vilivyopita kupitia link http://karibumbeya.com/ad-category/stories/
140 people reached

You Might Also Like

0 comments: