Binti aniponza, ameniingizia fedha kwenye simu yangu kumbe fedha chafu..... hali mbaya.. naomba msaada wenu

12:56:00 Unknown 0 Comments





Haya masuala ya kutafuta kazi yana shida sana, hebu fikiria mtu tangu nihitimu chuo mwaka 2011 yaani nipo tu nahangaika na nikibahatika kajikazi basi ni ka mkataba wa siku chache kisha narudi kuhangaika  na kusaka ajira.

Hakuna kibanda cha wauza magazeti nisichokijua au kibanda cha shoe shine wasionijua maana nikiamka kazi ya kwanza ni kwenda kwenye magazeti kuona kuna nini siku hiyo na baada ya hapo nitapiga story mbili tatu na jamaa wa shoe shine kisha nirudi nyumbani.

Huko nyumbani kama nina kifurushi cha internet basi nitaendelea kutuma maombi ya kazi kupitia mtandao kwa nguvu na kama sina basi nitasubiri wapangaji pale nyumbani warudi nidoee vifurushi vyao kwa bidii zote na namshukuru Mungu kwani  nyumba nikaayo ni nyumba ya familia ingawa familia inaishi kijijini hivyo wao wananitumia vifurushi vya unga na maharage mpaka nakoma.

Nimekuwa nikitafuta kazi kwa taabu na nakumbuka kuna siku stress za kupata kazi zilinijaa na kujikuta natuma maombi ya kazi ambayo muda wa kuomba uliishapita miezi saba iliyopita na niligutuka baada ya asubuhi kupewa email isemayo kuwa

 "Pole, kwa sasa nafasi hii ilijazwa miezi saba iliyopita tutakufahamisha ikitokea nafasi nyingine, Asante"

Nilijisikia aibu sana na kujiona kama kichaa ila kwa sasa nikaamua nione kama ni ajali kazini. Nikaona ili kuwa makini basi niandae barua moja ya kuombea kazi ili niwe naituma kila kazi nikiona na kuhariri tu aina ya kazi na anuani ya barua hiyo iendako ili niambatanishe na cv kunifanya niwe makini zaidi na kuweza kutumia muda mwingi kuifahamu kazi kuepuka kukosea.

Kuna siku moja tena mida ya saa nne asubuhi nafungua email nilikutana na majibu ya maombi ya kazi fulani yakanipa kichaa kwani yaliandikwa hivi: 

" Mr Dan, Utasemaje umeichunguza kampuni yetu na kuona ina rekodi nzuri za ufanisi ambao unachangia kukua hivyo ungependa kuwa mmoja wetu?

 Hii ni kampuni mpya sasa inaweza kuwa na historia gani?

 Acha kukopi barua na kutuma bila kujua undani wa kampuni unayotaka kuomba huu ni ukichaa na utapeli

Na kama unataka kupata kazi nzuri anza kujifunza namna ya uombaji wa kazi ulio sahihi na sio ubabaishaji"

Hii ikanikumbusha ile barua niliyowahi kuandia na kusema "My name is Dan a Tanzaniana boy aged 25" na majibu yakaja "Dear Dan, we need to employ a young man and not a boy and remeber this isn not a nursury school" kidogo niwatukane kihehe nikaachana nao.

Aiseee, ila majibu ya leo yakanifanya nikakumbuka kuwa mimi nilifoward tu ile barua na  cv bila kuiangalia vyema ile kampuni na niwakati huu nikakumbuka kuwa nina 10,000 kwenye mpesa nikaona niende nikaitoe na kupunguza ukichaa wangu na mikosi kwa kupata bia tatu ili nije kulala maana sasa stress zimezidi na badala ya majibu kuja mazuri naona sasa watu wanahisi mimi kichaa bila kujua ni stress za kutopata kazi.

Nilishangaa kuona nimefika kibanda cha m-pesa bila kujua nimefikaje kwa haraka hivyo  yaani jinsi mawazo yalivyoniandama kwa wakati ule. 

Nikiwa najiandaa kutoa hela akaja dada mmoja aliyeonekana kuwa mstarabu sana kwa mavazi na mwonekano wake na kuniambia 

"samahani kaka, naomba nimbeep mtu kwenye namba yako na kisha atakutumia fedha kwenye namba yako ya voda na kisha unisaidie kuitoa kwani nimeibiwa simu na anahitaji kunisaidia tafadhali"

Nikamwambia haina neno na akachukua namba hiyo na kuibeep na jamaa mmoja akampigia wakaongea na kisha dakika chache ikaingia milioni moja nikaitoa na dada yule akataka anipe fedha nikagoma ila akanilazimisha na kunipa elfu hamsini.

Nikaahirisha  kutoa fedha pale na kuondoka kwenda kwa mama Salome bar moja niliyokuwa nikipenda kwenda nikiwa na vijihela ili kuyatafakari maisha kwa ufasaha na kupata ujasiri lakini safari hii nilikuwa nikienda kutuliza pressure ya ile email ya asubuhi.

"Karibu Dan"

 Ilikuwa ni sauti ya Salome akinikaribisha pale bar na moja kwa moja akaniletea chupa ya ndovu mezani akaifungua na kunikaribisha. nikamuuliza vipi mama hayupo leo?

" ndio namsaidia, mimi leo nipo off sijaenda kazini."

Nikamuuliza umepata kazi lini salome? 

"kuna rafiki yangu mmoja aitwaye Fuledi alinipigia na kuniambia kuna nafasi kazini kwao hivyo nimepata zali la kazi bila hata interview na nina zaidi ya miezi miwili sasa"  alinijibu huku akivuta kiti na kukaa

Sikusema kitu nikainyanyua chupa ile ya bia na kuigigida mpaka ikaisha na kumlipa fedha na kutafuta bar nyingine nikaona huyu nae ananipa maamuvu yaani kazi bila interview?  

Nikafika mafichoni bar na kuanza moja moja mpaka kichwa kikapata moto na sikujua niliondokaje pale maana nilikuja kujikuta nimelala chumbani na ni siku ya pili saa saba ya mchana. Nikachukua simu yangu nakuona kuna zaidi ya missed calls 72  zote kutoka na simu ya mezani.

Nikiwa nawaza kama nina salio nipige mara ile namba ikaanza kuita tena nikaipokea na mazungumzo yakawa hivyo

Mimi: Hallo nani anaongea?

Simu: Mimi naitwa bwana majuto ni inspekta wa jeshi la polisi nadhani naongea na bwana dan?

(huku shuzi ya hofu ikinitoka)

Mimi: Ndio, nikusaidie nini?

Simu: Tunakuomba mara moja hapa kituo cha polisi cha kati kuna mahojiano kidogo na wewe.

Mimi: Sawa sawa naja.

simu: Jitahidi ufanye hima 

(alisisitiza afande)

Unaambiwa kitu cha kwanza nikaanza kufikiria ni nani nimezinguana nae jana yake au pombe zilinifanya nitende jambo gani?Niliendelea kufikiri huku nikielekea pale polisi nasikupata jibu sahihi mpaka nafika pale polisi.

Nikajitambulisha na kupelekwa kwenye chumba kimoja na kuanza kuhojiwa juu ya fedha nilizotumiwa milioni moja jana yake. Nikatoa maelezo jinsi ilivyokuwa lakini sikueleweka nikaambiwa kuwa nitahitaji kusaidia polisi.

Nikafikiri kusaidia polisi labda ni kuvaa zile sare nami nianze kazi iwe ndio ajira lakini wapi bwana nikaambiwa vua mkanda viatu weka simu hapa na vinginevyo na kuingizwa ndani uchunguzi ukiendelea.

Siku ya pili wapangaji baada ya kuona sionekani nyumbani wala sipatikani kwenye simu wakaamua kwenda kutoa taarifa kituo cha kati na kwa bahati wakaja kituo cha kati na kuambiwa nipo pale na wakaonana na mimi na kutoa taarifa nyumbani kijijini ambako wazazi wakaja siku ya pili yake.

Kesi ile iliendelea huku nikiwa nakabilia na kesi ya kumkata mtu mkono kumnyang'anya simu, kumwimbia laptop, kuhamisha fedha za benki kupitia simu hiyo na kumbaka mkewe mbele yake.

Nikaona dalili za kutoka gerezani na kurudi uraiani kuendelea na kusaka ajira zikiwa zinafifia kabisaa. Niwakati huu ambapo sasa kesi imepamba moto wakaongezeka watuhumiwa wengine wanne nikaona sio mbaya kilio cha wengi huwa sherehe lakini maumivu ya lupango ayajuaye ni mimi.

Kuna siku mahakamani nilishtushwa kuona na yule dada aliyeniomba nimtolee zile pesa kaongezwa katika kundi la wale watuhumiwa wapya nikahisi kuwa naweza sasa kuokoka ila bado hofu ilitanda sana juu ya hatma ya hukumu yetu.

Wiki tatu baadae ikwa siku ya hukumu ambapo watuhumiwa wenzangu walikutwa na hatia na kupewa adhabu za vifungo na mimi nikapewa adhabu ya viboko sita kwa kutumia simu vibaya kuingiza fedha nisizojua zimetoka wapia.

Akaletwa dada mmoja anipige viboko tulipotoka mahakamani nikawa namwonea aibu akanizaba kibao niweke matako sawa ili viboko vikae sawa kabala ya kushtuka muda huu bibi niliyekaa nae kanisani akaizaba kibao kumbe nililala wakati mahubiri yanaendelea na nilikuwa naota ndoto.

Nimeondoka kimya kimya na kwa jinsi nilivyokuwa nasisitiza familia iwe makini na ibada naona hata soo kurudi nyumbani ngoja niende zangu kwa Gracia Cosmas nikapokee cake ya bure.... nawe kama untaka fuata link hii
http://karibumbeya.com/ads/pata-cake-ya-upatanisho-ama-msamaha-bureeee/ 


Posted by Fred Kihwele · 1 hr · 
Pata cake ya upatanisho ama msamaha bureeee
Kutoka Gracious house of cakes... katika msimu huu wa wapendanao kama umekosana na mwenza wako ama ndugu yako ama rafiki ama mzazi wako.. ama mwanaoo tunaomba kukupatanisha nae..tunatoa keki...
KARIBUMBEYA.COM
184 people reached




You Might Also Like

0 comments: