MAKUBWA... Binti afungiwa ndani na kupigwa/kubakwa kwa miaka mitano bila msaada
Kila siku ilikuwa ni kipigo kutoka kwa mme wangu na kupewa maneno ya kejeli eti, " wewe ni mama wa nyumbani tu pamoja na elimu yako ya kidato cha nne huna lolote"Nililia sana tena kwa uchungu huku nikisali ili siku moja niwe na hela za kumsaidia mama yangu aliyekuwa kwa wakati huo akiugua bila ya msaada kisa mme wangu hataki kunipa fedha ya kumwokoa mama yangu.
Lakini pia kama mke nilihitaji kumsaidia mme wangu kwenye majukumu angalau nami niweze kuzalisha kipato cha familia lakini alinikataza na kuendeleza ukatili wake dhidi yangu kama vile mimi nilikuwa pale nyumbani kwa kazi ya kumstarehesha usiku akija kalewa na kulea mtoto na kazi za nyumbani.
Siku moja majira ya saa saba usiku alirudi akiwa kalewa sana nikajaribu kumtayarishia chakula kwani alikuwa akilalamika njaa hivyo nikawa nampashia supu yake.
Alinifuata jikoni akilalamika nachelewa na kabla ya kumjibu alinirushia ile sufuria yenye supu ya moto na kuniunguza tumboni.
Nililalamika kwa kulia usiku ule bila ya msaada zaidi ya huduma ya kwanza niliyojipa mwenyewe bila hata ya huruma, nililia usiku ule na kumuuliza Mungu ni kwanini baba yangu alikufa mapema kwani ni kifo chake kilichonifanya niishie kidato cha nne ili niweze kumwokoa mama yangu amabye naye bila juhudi zangu za siri muda huu angekuwa ni marehemu kutokana na homa yake.
Asubuhi mme wangu yeye alivyoamka akaondoka na kuniacha sina hata senti ya kwenda kutibiwa zaidi ya kuacha elfu mbili ya mboga na kisha kwenda aakuajuako yeye. Nilijiuliza hivi ni kwa nini haya yananitokea mimi? lakini jibu sikupata zaidi ya kulia na wakati huu machozi yaliisha hivyo nililia mkavu..
Nilibahatika kuwa na jirani aliyenipenda na kunionea huruma sana na nakumbuka alianza kuyafahamu maisha yangu kwa undani mwaka mmoja uliopita baada kipigo kikali kutoka kwa mme wangu kilichosababisha mimba kutoka hivyo asubuhi hii ilinibidi nimfuate niombe fedha na kwenda kutibiwa maana tumbo lilikuwa linawaka moto kwa maumivu ya kuungua..
Jioni yake mme wangu alirudi akiwa kalewa na wakati huo mimi nilishawapigia simu wazazi wangu baada ya kukaa siku nzima na kufikiri jinsi nilivyoweza kuvumilia maisha ndoa hiyo kwa miaka mitano ambayo hakukua wa furaha zaidi ya majonzi na vilio kila siku.
Pili nikashukuru kwa kuwa mwanetu alikuwa yuko mkoani kwa babu zake akisoma shule moja ya kulala ya wanawake, hivyo tamati ya mahusiano yetu ilikuwa ni usiku ule na baadhi ya ndugu zake walishaafiki pia suala hilo ingawa kwa huzuni sana na wengine wakitaka nibaki.
Nilimwambia, " baba saila naomba tuongee kidogo." Kwa dharau aliniangalia na kuniambia una nini cha kuongea na mimi "you cheap woman?"
Hakika niliumizwa na neno hilo ingawa baada ya mimi kukaa kimya kwa dakika chache naye kugundua kuwa nilikuwa nimefunga mizigo yangu akaanza kunipiga wakati huu sikungoja nikaliwahi begi dogo nikaukimbilia mlango na kutokomea gizani.
Nilitembea usiku ule na kufika katika bar moja ya usiku na kukaa na walinzi nikijifanya msafiri na asubuhi nikaaanza kufanya utaratibu wa kutafuta nyumba bila ya kuwa na senti mkononi na wajua mbeya ilivyo sasa vyumba juu na maisha sio kama yale ya miaka miwili iliyopita hata kama kuna unafuu kidogo ukilinganisha na mikoa mingine.
Baada ya kuhangaika siku nzima nilibahatika kupata nyumba moja ya mzee mmoja maeneo ya mbalizi ambayo chumba kimoja bei yake ilikuwa ni elfu thelathini na tano kwa mwezi na kwa kuwa sikuwa na hela nikamwomba anisaidie nianze kukaa na ndani ya miezi mitatu nitampa naye akakubali kutokana na hadithi yangu ya maisha..
Nikatandika chini kitenge changu na kulala kabisa nikiwa sitaki tena kuwasiliana na mme wangu hivyo nikabadili namba ya simu na kuweka laini mpya na sasa nikawa na maisha mapya nikiwaza nitakulaje na kuishi vipi.
Wakati huu sikuwa na uso wa upole zaidi ya kuwa na uso mokomavu usiohofia chochote katika maisha ya kuamini kuwa sasa ni wakati wa kuiambia dunia mwanamke anatakiwa kuwa shujaa na kujikomboa yeye na wanamzunguka na kuupinga ukatili huu niliofanyiwa ambao ndo chanzo cha wanawake wengi kufa wakiwa maskini au kuamua kuishi maisha ya kujinyanyasa,
Nilijaribu siku ya pili kwenda kwa dada mmoja ambaye niliwahi fahamiana naye akanikopesha 50,000 ambayo nikanunulia chakula na jiko dogo na hivyo maisha kuanza rasmi
Maisha ya kulala chini pale yalikuwa magumu licha ya wapangaji wenzangu wa kike kunicheka ila nikajipa uso mkavu na kumwomba Mungu aangaze njia zangu.
Niliamka asubuhi na kwenda maeneo waishio watu wenye hela zao na kuomba kuwasaidia kazi kwa malipo kidogo ambayo yalinifanya niweze kujimudu japo kwa kiasi kidogo sana ila nilikubaliana na hali hiyo kwa muda huo.
Nakumbuka ilikuwa ni jumanne moja baada ya mwezi mmoja kupita nilikuwa nyumbani ambapo nilipigiwa simu na mdogo wangu wa mwisho aliyepo kijijini kuwa amenitumia vyakula na fedha kidogo kupitia gari moja hivyo niende kuchukua jioni hiyo pale stand kuu ya mabasi mbeya.
Nilifurahi sana na kufikiri nitaondokaje kwenda kule kwani nilikuwa na akiba ya mia tano na basi kwenda kule ni mia tano hivyo kama vingechelewa ningeshindwa kurudi nyumbani, na akiba hiyo nilikuwa nikitegemea kuitumia jumatano kwenda sehemu amabko nilifanya kazi sasa niliahidiwa kwenda kuchukua ujira wangu.
Wazo la haraka likaja kuwa nitembee kwenda mjini na wakati wa kurudi nipande gari ili ile mia tano itumike nauli ya kurudia mbalizi kama gari lisipoonekana.
Baada ya saa moja na nusu la kutembea hatimaye nikafika stand na kusubiri gari ambalo halikutokea na nikiwa pale kuna msafiri mmoja niliyefahamiana naye alinikaribisha soda ambayo sikuinywa na kuibadili fedha ili inisaidie na kuwa na elfu moja na mia mbili mfukoni.
Nikapanda daladala na kuondoka kwani basi liliharibika na kesho yake lingeingia nikaona niondoke nije kesho yake, nikiwa ndani ya daladala baada ya kutembea kidogo kuna kaka mmoja akawa anataka kushuka kwenye daladala na kumbe waleti kaisahau dukani....makubwa
Baada ya ugomvi na konda wa kulipana nauli nikaona nimlipie na akanishukuru na kuomba namba yangu nami kumpa yangu akanibeep kisha kashuka.
Siku ya pili nikauchukua mzigo na baada ya miezi miwili mambo yakawa magumu zaidi na kipindi hicho chote hakuna aliyejua niko wapi hasa ndugu na mme wangu yule.
Siku mmoja asubuhi baada yakuamka nikiwa sina kitu cha kula na jana yake nililala mtupu na hali yangu ni mbaya nikaona nimpigie yule kaka wa daladala niliyemlipia miezi kadha iliyopita na akanielekeza aliko na nikaamua kutembea tena kutoka mbalizi mpaka kule aliko.
Nikafika pale baada ya safari ndefu na kumsimulia maisha yangu na mapito yake, kaka yule akasema naye ana wakati mgumu ila antanipa simu moja nzuri na kama nitaweza kuuza na kuja kumpa fedha yake nikichukua gawio la juu basi tutaendelea hivyo.
Nikaichukua na kwenda mtaani na kuiuza kwa gharama ya shilingi laki moja na nusu na kupata elfu hamsini yangu na baadae nikamlipa akaniamini na kisha kunipa mbili mara tatu mara nne na kisha mia na wakati huo nami nikawa nimetafuta chumba cha biashara na kuanza kuuza simu zile..
Hivi sasa nina duka kubwa la simu na ninauza jumla na reja reja nina, nyumba yangu binafsi na nina usafiri wangu, nimeweza kumlipia mwanagu feddha kwani mme wangu sasa kaishiwa na kila siku ananitafuta nirudiane naye............
Nimemjibu zaidi ya mara kadhaa " Past cant create future, your my past and i cant hold you now" Ni kiingereza nilichojifunza baada ya kujiendeleza na sasa ninasoma diploma ya biashara katika chuo fulani hapa Mbeya na naishukuru Smart Ideas Communications wamiliki wa www.tabasamunafuledi.com kwa kunipa nguvu na ushauri wa maisha yangu mpaka leo
Ninaishi upya nikiwa na maisha mazuri na namshukuru Mungu kwa kila hatua yangu na kila nikikimbuka maisha ya nyuma siachi kumwambia Mungu wewe waweza na ninnamini nawe uta-comment Mungu waweza pia.
Like Tabasamu na Fuledi
Karibu Mbeya shared a link.
Travel Deal
0 comments: