MAMBO 8 AMBAYO HUWEZI KUFUNDISHWA SHULENI
09:09:00
Unknown
0 Comments
09:09:00 Unknown 0 Comments
1. Maisha hayako fair. Yazoee. Unaweza kufanya kazi sana ila ukakosea kidogo tu usifanikiwe lakini mwingine ukaona hafanyi sana ila anafanikiwa. Usinung'unike, hayo ndiyo maisha.
2. Hutakaa upate kazi ya mshahara wa kukutosheleza mara tu baada ya kuhitimu elimu yako. Anza na kilichopo.
3. Kama unadhani walimu au malekchara hawako fair, subiri ukutane na maboss kwenye kazi halafu tafakari upya.
4. Ukikosea wewe usilaumu wengine. Sijui wazazi, sijui ndugu, sijui waalimu. Ni maisha yako. Jisimamie. Pambana.
5. Watu unaokutana nao wanajua vitu ambavyo wewe hujui. Heshimu watu. Jifunze. Kaa na watu uvae viatu. Usijione graduate ukakute mzee wa darasa la nne mlinzi getini ukaanza dharau. Utapotea.
6. Shuleni unaweza kuwa wa mwisho lakini maisha hayaamuliwi hivyo peke yake. Bado una nafasi.
7. Maisha hayagawanywi kwa mihula (semesters). Jipangie mihula ya maisha mwenyewe, kuwa na sheria na mipango ya maisha yako na itekeleze. Hakuna atakayekupangia wala kukuhimiza kufanikiwa.
8. Unayoyaona kwenye TV ni maigizo, sio maisha halisi. Hata habari wakati mwingine huwa ni za kupikwa, sio uhalisia. Amka! Kwenye maisha ya kawaida watu wanafanya kazi na sio mapenzi muda wote kama tamthilia za Kimexico au Kifilipino.
Facebook ilivyonikosesha raha 12
Ilikoishia jana
Kakaaa, Hata kabla ya kumaliza kusema neno kaka vizuri simu ilikatwa na hapo sasa hasira ikanipanda na kusema sasa naenda kuchukua ile sanda chini ya kitanda na kwenda kumpelekea kaka na ku... See More
Ilikoishia jana
Kakaaa, Hata kabla ya kumaliza kusema neno kaka vizuri simu ilikatwa na hapo sasa hasira ikanipanda na kusema sasa naenda kuchukua ile sanda chini ya kitanda na kwenda kumpelekea kaka na ku... See More
87 people reached
Fuledi Mwagito
Nakushukuru kwa kunipa nafasi hii adimu sana ya kufurahi, kuelimika na kubadilishana mawazo. Nitafurahi sana kama utaniachia comment hapo chini ili nijue kama habari,ucheshi, simulizi na vioja vioja hivi vimekupa siku yako kuwa BOMBA. Kumbuka nawe waweza share nami chochote ulichonacho kwa kunicheki kupitia whatsapp kwa namba 0713317171 au kupitia comment. Asante.
0 comments: