MAMBO YA KUFANYA UKIKUTANA NA EX WAKO

19:54:00 Unknown 0 Comments

1. KUWA MUWAZI kama upo tayari kuongea na ex wako mkikutana, akuulizapo swali lolote mjibu inavyotakiwa kwa majibu mafupi yasiyo ya kubabaisha yenye ukweli mtupu. Kama ni ndiyo 'ndiyo' na kama ni hapana 'hapana' itakufanya kujenga utu wako na kukupa kujiamini. 

2. USIJITONGOZESHE kama umeshaachana na mpenzi wako mpya kwa sababu ya huyo mpenzi wako wa zamani usifanye mambo ya kujitongozesha kama vile kukaa naye karibu kumchekea chekea au kumtega kwa namna yeyote ile kama ikitokea bado unampenda muache yeye akuanze na umsumbue katika kumjibu kwa sababu kama mlishaachana huna hakika lile kosa halitajirudia mkirudiana.

3. KUWA NA MAWAZO CHANYA wengi wanapokuwa pamoja na wapenzi wao waliopita hufikiria negative hujiuliza anawaza nini? Ananiona mbaya? Vipi kama anakuja kunionesha mpenzi wake mpya? Haya ni maswali machache yanayowapitia wengi vichwani mwao. Lakini kama ukiwa na mawazo chanaya unaweza kujiamini na uwezo hata wa kumface huyo mpenzi wako aliyepita kwa hiyo uwapo na ex wako fikiria mawazo chanya.

4.RELAX muda mwingi watu mnapokutana na wapenzi wenu waliopita huwa mnapanic kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kutulia na kuvuta hewa nyingi ndani na kutoa nje hii hujenga kujiamini na kuondoa hofu iliyojengeka usoni mwako

5. USIONESHE KUKOSA FURAHA KATIKA PENZI LAKO LA SASA
usimpe nafasi x wako kujiona yeye ni muhimu sana katika maisha yako yaani ajione yeye alikuwa ni furaha yako ya pekee hata kama huyu wa sasa hana tofauti na yeye lakini jitahidi kujiweka sawa na kumuonehsa kuwa hakuna tatizo huyu wa zamani ili kujenga kujiamini kwako kila mnapozungumzia habari za mahusiano.

Facebook ilivyonikosesha raha 11

Ilikoishia jana

Nilipofika sebuleni hata kabla sijafanya lolote kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya mke wangu na ukanifanya niishiwe nguvu kabisa kwani simu nilikuwa nayo.

Ujumbe huo ulisema...........................................................

Endelea

Ujumbe huo ulisema, " My dear ule muda ndio huu sasa amka na hakikisha hakuoni baba segito na fanya kama nilivyokuelekeza"

Ujumbe huu ulinichanganya zaidi na kunifanya nitoke nje bila kujua wapi nilitaka kuelekea. Nikajiuliza, je hii ni meseji kutoka kwa nani na anataka kumpeleka wapi mke wangu usiku huu?

Nilikaa pale sebuleni kwa muda mrefu sana huku nikiwaza na kujipa majibu ambayo hata hivyo sikuridhishwa nayo na kusubiri kukuche niende kumcheki mama segito.

Asubuhi nikiwa njiani niliijaribu ile namba huku nikihofia kusikia mambo ya ajabu lakini namba ile haikuwa hewani na hata nilipojaribu kuiangalia kama imesajiliwa haikuwa imesajiliwa.

Nilifika pale hospitali kwa kuchelewa kidogo na moja kwa moja nikaingia chumba alicholazwa mke wangu mama segito.

Nilipatwa na mshangao pale mke wangu aliponiona na kukimbilia kwa daktari wa zamu aliyekuwa pale huku akiniita eti mimi freemason nataka kumuua.

Kiuweli nilishikwa na butwaa kwani sikuruhusiwa tena kuingia mle na daktari akaniahakikishia itakuwa ni mshtuko wa jana yake hivyo bado anahofu na hajitambui.

Wakati natoka pale ili nirudi nyumbani pale mlangoni nikapishana na shemeji yangu ambaye ni kaka wa mke wangu na baada ya kusalimiana nae nikaona nimwache aingie peke yake kwenda kumcheki dada yae na mimi nipitie sehemu nipate angalau kifungua kinywa.

Nilikaa pale kwa zaidi ya saa moja na kwenda nyumbani na nilipofika pale nikashangaa baada ya kuonana na binti wa kazi akiwa peke yake bila mwanangu segito na kuniambia shangazi yake ambaye ni mke wa kaka wa mama segito kaja kumchukua.

Wakati nikiendelea kushangaa hayo mara simu yangu ikapigwa...................................................endelea kwa kufuata link hii

http://karibumbeya.com/ads/facebook-ilivyonikosesha-raha-11/

Photo: Facebook ilivyonikosesha raha 11

You Might Also Like

0 comments: