SABABU 3 KUU KWANINI WANAUME HAWATAKI KUOA

09:39:00 Unknown 0 Comments


Dunia imechange sana...Zamani Mwanaume kufika miaka 30 hajaoa ilikuwa hatari,mwiko kwanza maana wazazi na ukoo wote watakukalia kooni..Ila siku hizi,aaah,watu hawana habari,wanatafuta watoto tu kwa kuzalisha Wanawake wa watu halafu basi...Hawataki kabisa Commitment.

Inaonekana kama ni Lifestyle ambayo ilianza mdogo mdogo,ikapenetrate,na ni kama inaanza kukubalika maana ongezeko la Wanadafada kuzaa tu bila mpangilio,bila ndoa linakuwa kubwa sana,na kwao inakuwa Simple tu,yaani Freshhh...

Kwa kutambua hili,Wadada hawana habari...Wanasema kuolewa ni utumwa,heri wazae.....Na Wanaume nao wanasema kuoa mh mh,bora wapate mtoto walee,ila kuweka mtu ndani ah ah,kimeo.

Feeling zote 2 zimegongana,na zimeshabihiana halafu zikakubaliana,bila kuwa na majadiliano yoyote...Imetokea tu...

Kila jambo lina Origin...Kuna chanzo...Kwanini hali hii itokee siku hizi tu,ni utandawazi...Ni mabadiliko ya Tabia nchi...Ni nini haswa???

Lazima kuna jambo...

Source iliyosababisha inaonekana ni Wanaume....Wanaume wanaonekana hawapendi kuoa siku hizi,lakini kwanini wasioe...Why siku hizi na Sio zamani ambapo ilikuwa ni fahari kwa mwanaume kuoa...Miaka 20 mtu ameoa na Watoto juu...Ila siku hizi walaaaa...

Hata Wanaume hawakupenda,ila kuna sababu zimesababisha wasipende kuoa....Kuoa ni a very nice Feeling lakini kuna vitu Wanaume hawataki na ndo maana hawaoi....

Leo tuangalie SABABU 3 ambazo zinawafanya wanaume WAPOTEZE HAMU YA KUOA

1.1961 REASON...ITS ALL ABOUT UHURU
Tanzania ilipata uhuru mwaka 1961!
Hamna kitu Wanaume wanapenda kama UHURU
If una boyfriend,na unafanya mambo ya kumnyima uhuru,asilimia za huyo jamaa kukuoa ni 0.01%,Trust me!

Kama the best u can give ur man is Harassment....Questions kibaooooooo....Kumpangia ratiba zako ili yeye afit aache mambo yake,na kila siku unataka priority,SAHAU NDOA!
Ukikutana nae tu umekimbilia simu,huyu nani kakutext,mara huyu si nlishakukataza kuchat nae..Khaa!!

Uliza walioolewa walifaulu vipi huu mtihani,huu ni kama Mtihani wa Hesabu kwa Mwanafunzi wa Form 4,ukifaulu huu,umejiwekea hazina,trust me! Mpe mwanaume uhuru kwanza then ndo uongee mambo mengine,hapo mtasikilizana na hata ratiba zako zitafit kwenye uhuru wake,Dont try to put urself as the Most Important,ul loose! Akisema anaenda kuwatch mpira we unamwambia arudi home mwangalie movie,what the heck?Why movie na sio Football anayopenda???Sawa kuwatch movie sio dhambi lakini kwanini ugonganishe ratiba na unajua anapenda mpira?Hapa unampa definition kwamba unakuwa dominant na hakuna kitu kibaya na sumu kama wewe kujaribu kuwa Dominant,unajifanya Transformer..Dont be this kind of a Girl,He will end up being a Boyfriend,and He will never move a step ahead,akimove ujue Kibuti!

2.WANAWAKE MIMI-TYPE
Aina ya wanawake wanaojifikiria wao tu...Baby naomba mtaji wa Maembe..Baby naomba mtaji wa Mabungo...Baby nataka kuanzisha biashara ya Nguo na Vipodozi....Why cant you say baby,kutegemea mshahara sio vizuri kwanini TUSIANZISHE BIASHARA ambayo ITATUINGIZIA KIPATO EXTRA....Unaona utofauti????Collective statements..onyesha kwamba na yeye ni Inclusive.Sio MIMI this MIMI that....Be the kind of a Woman who gives an idea...Make sure he understands it...And ensure he takes it further and Control its implementation

Tangu uanze uhusiano wako na huyo Mwanaume umewahi kumshauri kitu gani ambacho siku akitaka kukumwaga atasema dah This girl did this Let me be considerate,Kipo kweli,halafu unataka ndoa????Sio idea za kununua Soksi na Boxer,Idea constructive ambazo zilichange maisha yake...HAKUNA! Sasa nani akuoe??

3. MWANAMKE DIVIDER
Aina hii ya Wanawake ni wale ambao wanaingia kwenye Maisha ya Mwanaume fulani halafu wanataka wawe kama MD hivi...Wamemkuta jamaa ana Marafiki zake,Mabesti kweli,wametoka mbali na huyo Mwanaume hujui wamemtoa wapi,wamemsaidiaje hadi hapo alipo....anaanza kutoa Opinions kuhusu hao watu...Fulani achana nae namuona kama hana lolote....Hivi Fulani anakusaidia nn...Halafu flani simpendi anaongea kweli...Hapo jua ushachemka....

Hamna vita ngumu kama vita ya kumchagulia Boy wako Marafiki na kujifanya HR una-screen uliowakuta eti wewe huwapendi...Huwezi shinda hiyo Vita I guarantee you,na ukiona umeishinda jua kuna kimeo mbele

Ukishinda hiyo vita na uhusiano wako utakuwa chali,unless huyo Mwanaume awe Bushoke type ambaye hana msimamo lakini siku zote ukipigana na Mashemeji ambao ni Close friends wa Jamaa YOU WILL LOOSE

When it comes to Men,Marafiki are more than Parents.They know kila kitu hadi ambavyo wazazi wake hawajui,na si ajabu hata uwepo wako kwenye maisha yake walichangia mawazo na kukuscreen kabla,na kumshauri akuchukue,lazima aliask opinion...Sasa umeingia unajifanya HR,wanaku-Ulimboka fasta utashangaa.

You Might Also Like

0 comments: