SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU LANGO LA MOTONI CHAPTER 21

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 21
Ilipoishia
Bila hata ya kupepesa macho mama zombo alichukua bahasha ile na kuichoma moto na kisha akarudi kuandaa chakula cha jioni bila hata ya kumshirikisha mmewe ambaye muda huo alikuwa katulia ila ana mzinga wa pombe kali mezani na hakutaka kabisa kutoka nje ya nyumba yake siku hiyo, " nani ayarudie maisha yale... thubutu yake" alijisemesha mama mzombo huku akimalizia kupika chakula cha usiku.
Ben alikuwa kashakunywa bia ya tatu na picha ya samira ikiwa mezani kwake, kila mara aliiangalia na kujipiga kifua na saa nyingine alisimama na kutoka nje billa kujua nini angefanya.
Endelea
Akiwa pale ghafla akaingia mwalimu jack na kumfanya ben aachane na kuiangalia picha hiyo na kumsalimia kisha wakaomgea kwa muda.
Maongezi yao yalichukua muda na kisha wakaachana na muda mfupi baaadae ben alikuwa njiani akielekea nyumbani kwake.
Siku ya pili yake asubuhi gari la ben lilipaki nyumbani kwa mwalimu jack na mazungumzo yalikuwa marefu sana kwani ben alitaka kujua wapi waliko aunt amina na samira lakini mwalimu jack aligoma.
Ben akatoka na kwenda nje kwenye gari na aliporudi alikuwa naa bahasha ya mkononi na baada ya kumpa mwalimu jack muda huo huo akaingia ndani nakuja na karatasi yenye namba ya aunt amina na uelekeo walioelkea na kumwambia kuwa kamwe asimtaje kuwa alimpa habari hiyo.
Gari liliendeshwa kwa kasi sana na majira ya moja kasoro jioni ya siku hiyo alikuwa kawasili mji wa akina aunt samira na kwa kuwa ilikuwa ni usiku akaona ni bora atafute nyumba ya kulala wageni ili siku ya pili yake aendelee kuwasaka kwani sasa alitaka kumwambia ukweli samira juu ya hisia za mapenzi juu yake na kuwa anataka wawe kitu kimoja.
Baada ya kupata chumba akaamua aingie upande wa bar ili ajipatie vinywaji huku akijaribu kufahamiana na marafiki. Aliingia na kukaa meza moja aliyokuwa kakaa mrembo mmoja na kuagiza kinywaji chake huku akiwa busy na simu yake akiwatumia watu meseji.
Alikaa pale kwa mudda na kuitoa picha ya samira na kuiangalia, jambo hilo likamfanya binti alikuwa kakaa meza ya jirani aichungulie na haraka kajinyanyua na kwenda nje na kumpigia mtu.
" Khadija niambie wangu!!, umesharudi??"
" ndio na nipo hapa hotelini ila kuna mpya muddy, wewe uko wapi?"
" Nipo mtaa wa pili hapa nilikuja kula, leo sikutaka kula hapo hotelini nikaona nile cha mama ntilie hapa"
" Ok, basi fanya haraka uje kuna issue sitaki tujadili kwenye simu kuna kitu hapa"
" Ok, khadija nakujaa nipe dakika kama nne"
" Roger that", alihitimisha khadija na kurudi haraka kwenye meza yake na kumwonaa ben akiwa anaendelean kunywa bia yake huku kaishika picha mkononi.
Dakika chache baadae muddy alifika hotelini pale na kumpgia simu khadija atoke nje. " muddy kuna jamaa yuko ndani hapo sura yake ngeni ila kaishika picha ya samira sijui ana lengo gani"
" kakaa wapi"
" meza ya karibu na mlango wa kutokea bustanini"
" ok, wewe ulifanikiwa kwa mzee zombo"
" ndio ila sasa hatoki ndani na ile bahasha nafikiri mkewe hajampa au mzee katia kichwa ngumu maana hakuna lolote mpaka sasa"
" ok kesho tutafanya zoezi lingine ila sasa ngoja tudeal na huyu jamaa"
Ben alikaa pale kwa muda huku akiwa anakunywa pombe bila break ilipofika mida ya saa tano na madakika ben alikuwa tayari kashakunywa vya kutosha na muda huo alipigiwa simu na kumfanya atoke nje.
Akiwa pale nje anataka kupokea simu alishtushwa na kishindo cha mtu aliyemrukia na kumpulizia kitu usoni na mara moja akapotelewa na fahamu.Akachukuliwa usiku huo huo mpaka sehemu moja nje ya mji ambako muddy aliweka kambi yake na kumweka ben katika chumba kimoja chenye giza nene huku akiwa kafungwa.
Mama zombo aliamka kwa kuchelewa sana siku hii na alipoichukua simu yake akagundua kuwa alichelewa apointment hivyo akajiandaa haraka na kuondoka. Nusu saa baadae aliingia hotel moja na moja kwa moja akaingia chumba namba 209 na kukutana na Grey.
Grey na mama zombo wamekuwa na mahusiano ya siri kwa muda mrefu hasa baada ya mzee zombo kuanza kuchanganyikiwa na mabinti wa dogo hasa baada ya kupata ubilionea wa ukubwani na kusahamu majukumu yake ya kifamilia na kumfanya mkewe ajikute akiangukia mikononi mwa grey ambaye alikuwa akija nyumbani kwake kumpaka rangi kucha zake.
Walikaa pale ndani kwa muda wa masaa mawili bili ya kujua kuwa alikuwa akifuatiliwa na watu na muda mfupi baadae aliondoka na kuanza kuelekea sokoni kama kiteteo cha safari yake. Akiwa anajiandaa kuingia barabara ya sokoni kuna gari lilimsimamisha kwa kuikata barabara na kumwamuru mama ashuke na alikuwa ni binti wa siku ile pale sokoni aliyempa ile bahasha.
Mama zombo alichukuliwa na kuwekwa kwenye gari jingine na gari lake likawekwa pembeni ya barabara na kufungwa kisha nae akafungwa kitambaa cheusi machoni na wakaondoka kwenda kusikojulikana.
Majira ya saa kumi na mbili kasoro mzee zombo alionekana pale nyumbani akihaha kila chumba mara kupiga simu bila ya mkewe kuonekana. Ilipotimia saa.......
KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia WHATSAP nipigie 0713317171 na kwa wale waliolipia chapter namba 22, 23 na 24 mmetumiwa
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

0 comments: