SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU LANGO LA MOTONI CHAPTER 22

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 22
Ilipoishia
Mama zombo alichukuliwa na kuwekwa kwenye gari jingine na gari lake likawekwa pembeni ya barabara na kufungwa kisha nae akafungwa kitambaa cheusi machoni na wakaondoka kwenda kusikojulikana.
Majira ya saa kumi na mbili kasoro mzee zombo alionekana pale nyumbani akihaha kila chumba mara kupiga simu bila ya mkewe kuonekana. Ilipotimia saa.......
Endelea
Majira ya saa kumi na mbili kasoro mzee zombo alionekana pale nyumbani akihaha kila chumba mara kupiga simu bila ya mkewe kuonekana. Ilipotimia saa moja na nusu kijana mmoja wa mzee zombo alimpigia simu mzee zombo.
" mkuu, habari za jioni"
" Unataka kuzija zikusaidie nini wewe, hebu niambie nini kimekufanya unipigie simu muda huu" alifoka mzee kombo ambeye kwa siku kadhaa amekuwa katika hofu inayoambatana na kunyimwa uhuru wake wa awali.
"Samahani mkuu, gari la mama nimeliona limepaki hapa nji ya kuingilia sokoni kwa muda mrefu sana, sijui limesahaulika"
" ok, asante kwa taarifa, nakuomba ukae hapo uliangalie na unipe taarifa ya nini kinaendelea"
"Sawa mkuu" alimaliza kuongea na kukaa chini huku akijaribu kufikiri ni nini kimemsibu mzee zombo mpaka akawa mpole kiasi hicho. Aliendelea kutafakari kwa dakika kadhaa kabla ya kushtuka kuona mama zombo akija na kisha akaliwasha gari na kuondoka kwa mwendo wa ajabu.
Nusu saa baadae mama zombo aliwasili nyumbani kwake na hakuwa na dalili zozote ile za hofu na moja kwa moja aliingia chumbani na kumshuhudia mzee zombo akiwa kafura kwa hasira na mkononi akiwaa na chupa ya bia.
" wewe ulikuwa wapi mmpaka uliache gari pale sokoni kwa muda wote huo?"
" Mme wangu si nilikuomba jana kuwa leo nitaenda salon ka wasusi wa kimasai pale karibu na sokoni? au umesahau?" mama zombo aliutumiaa mwanya huo kumdanganya mmewe kwani alikumbuka kuwa jana yake usiku alikuwa kalewa sana na pombe kutokana na mawazo yanayomkabili.
"ooooooh, am sorry my wifelicious nilisahau wangu, nisamehe" aliongea mzee zombo huku akimfuata na kumkumbatia mkewe ambaye yeye muda huo alikuwa akicheka kicheko kikubwa baada ya kusikia neno wifelicious.
Ben alikuwa bado yupo katika kile chumba cha giza bila ya kuonana na mtu yoyote zaidi ya kusikia sauti ya mziki kutoka katika radio aliyokuwa kawekewa pale ambayo pia alishindwa kuifikia kutokana na kufungwa na pia bado alikuwa na hofu.
Dakika chache baadae chumba kile kilifunguliwa na muddy akiwa na khadija waliingia na kuanza kuhojiana na ben bila hata ya kuwaona kutokana na giza lililokifunika chumba hicho.
" hallo tunaomba utuambie wewe na yule binti aliyekuwa kwenye picha yako mnamahusiano gani naye?" Alihoji muddy kwa sauti ya ukali
" Mimi naitwa BENITO SONGOMBO maarufu kwa jina la ben ni mfanyabiashara na ni mtu niliyewasaidia samira na aunt amina hapo awali. Nimepotezana nuriuao na sasa nilikuja huku kuwatafuta kwa lengo zuri"
"kwa sasa hutaruhusiwa kuonana nao wala kujua popote pale walipo na unapewa masaa machache baada ya kuachiwa hapa uwe umetoweka katika mji huu, na chochote utakachojaribu kukifanya tena au kujribu ili kukutana na watu hawa utaumia"
Alipomaliza kuongea maneno hayo akamfungua na kumfunga kitambaa cheusi na kumtoa hapo na waakampeleka na kumtupa nje jirani ya hoteli ile na kisha wakatokomea kusikojulikana.
Mlinzi wa hotel hiyo alisikia sauti ya ben akiomba msaada na kwenda kumsaidia, wakati huo ilishatimia saa nne kasoro ya usiku na akafanikiwa kulichukua gari lake na kuanza safari ya kuondoka muda huo huo kurudi kwake mji jirani na hapo.
Saa tano kasoro ya usiku mama zombo alikuwa yuko bafuni kwake kafungulia maji huku yeye akiwa kaegama ukutani akifikiri jambo kwa kina sana na kujikuta akitamka kwa sauti.
" Duh, mambo juu ya mambo, nikisema niwaibie huo ufunguo wa chumba cha siri cha mzee zombo na kuwapa haya mafaili na mzee kombo akinishika nitaachika, na nikisema nisiwape ndani ya siku mbili wamedai watanifanya kitu kibaya, sasa hapa sijui nafanyeje mbona nahisi kufa kufa!!!, ila piga ua mimi bado ni mtoto wa mjini tutapelekeshana tu" almaliza kuongea mama zombo na kuanza kuoga.
Saa saba kasoro dakika 20 za usiku simu iliita........................ ..............
KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia WHATSAP nipigie 0713317171 na kwa wale waliolipia chapter namba 22, 23 na 24 mmetumiwa
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

0 comments: