HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Sehemu ya 4
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Sehemu ya 4
ILIPOISHIA JANA
Sauti niliyoisikia ilikuwa ya yule dada ambaye mara kwa mara tumekuwa tukiwasiliana naye bila kumjua jina lake. Akasema, sapraiiiz hata nimeku-miss nikaona nikupigie simu nikusalimu sina mengi nitakutafuta usiku kwenye simu yako ya mkononi kuna kitu nyeti nataka tujadili......... hakuongea zaidi akakata simu.
Niliishiwa nguvu na kuanguka chini......................... .............................. ......
Soma mwendelezo wake
BAADA ya kuzinduka nikajikuta nipo hospitali nikiwa nimezungukwa na ndugu na marafiki. Sikuamini nilichokiona nikafikiri nipo ndotoni.
Mke wangu akanihoji, " nini kilikukuta mme wangu? Maana nilipigiwa simu kuwa umeanguka ghafla na umeletwa hospitali na pia vipimo vinaonyesha ulipatwa na mshtuko mme wangu, Ni mshtuko gani mme wangu?"
Ingawa nilikuwa nimeshaanza kupata nguvu, kutokana na lile swali nikajifanya sina hata nguvu ya kulijibu swali maana ingenipa mshtuko wa pili hata kabla ya kutoa maelezo yake. Jioni yake nikaruhusiwa kutoka na kurejea nyumbani.
Zilipita takribani wiki tano nikiwa nimeirushia chooni ile laini tena choo cha shimo ili nisiweze kuiona tena.
Hata kama nipatwa na wasi wasi baada ya kukumbuka enzi za udogo wetu tuliwahi mchukia paka wetu kisha tukamshika na kumtupa katika choo cha shimo ili asiwe taabu tena kwa kunya kitandani na kwenye unga.
Lakini maajabu yake baada ya kumtupa na kuridhika kuwa yuko shimoni muda wa chakula alikuja akiwa na kinyesi yaani wote tuliduwaa na kunifanya kuwachukia kabisa paka.
Lakini kwa hili niliamini kuwa ni suluhu na hata yule mhudumu wa ofisi nimwambia asipokee siku yoyote ya kunitaka mimi private zaidi ya kuwambia wanitafute bila kuwapa namba yangu na zile za kiofisi ajibu.
Nilichukua likizo ya wiki mbili pale ofisini na kumwambia mke wangu twende nje ya mji tukapumzike na nikatumia mwanya huu kumkumbusha kuwa nilitakiwa kufanya hivyo kwa ushauri wa daktari hasa baada ya lile la shinikizo kuwa nilizidisha kazi mno.
Niliondoka na familia yangu kwenda matema nje kidogo na mji wa Mbeya huku nikiamini sasa lile tatizo limeisha.
Kweli zilipita siku tatu nikiwa pale kwa furaha na familia yangu nikiwa na marafiki wapya na simu nyingi nilizopigiwa zilikuwa ni za ndugu jamaa na marafiki.
Ijuma mmoja usiku wa saa nne nikiwa nacheza na mwanangu huku napata mvinyo wangu mara simu ikaita kuangalia ilikuwa ni namba ngeni.
Nilipotaka kupokea tu ikakata na kwa kuwa sikuwa na muda wa maongezi na ilikuwa ni usiku nikaachana nayo.
Jumapili usiku nikiwa na mke wangu tumelala pale hotelini, simu ilipigwa tena na wakati huu iliita sana na mtu wa kwanza kuisikia alikuwa mke wangu.
Akaichukua simu na kunipatia, si wajua tena hawa ndugu zetu walivyo aleji na simu wakijua ni michepuko.
Basi mimi nikaichukua ile simu na kuipokea kwa loudspeaker nikijiamini kuwa sina mchepuko.Ila kwa bahati mbaya mpigaji alisikika hewani ila hakuongea neno nikakata simu na kulala.
Jumatatu mchana nikiwa nimekaa pembezone mwa ziwa napunga upepo nilipokea sms iliyosema "Nitakupigia usiku" kutoka kwenye namba ile ile ya jana yake usiku.
Nikataka kupata uhakika wa kuwa ni nani huyo ambaye hawezi kuongea mchana mpaka usiku. Nikaupiga ile namba ila haikupokelewa basi sikuitilia maanani.
Nikaendea kupunga upepo pale na si wajua tena mandhari ya matema ilivyoyakuvutia? Zilipita dakika 20 nikapokea sms kutoka katika namba ile ile ikisema, " wee endelea kupunga upepo tu, nimeshakuambia nitakupigia. Huelewi nini hapo?"
Nilinyanyuka haraka na kuelekea usawa wa ziwa bila kujua naelekea wapi? Mara ghafla nikashtishwa ba sauti ya mwanangu akisema baba na mimi nije kuogelea?
Ile nageuka tu nilichokiona.................. .................... Fuatilia kisa hiki kesho mida kama hii
NAKUTAKIA WEEKEND NJEMA
Ile nageuka tu nilichokiona kilinifanya nibadilishishe uamuzi wa kuelekea ziwani kwani alikuwa mke wangu akiwa na mwanetu mdogo.
Akaniita na kuniuliza, " mbona umenyanyuka haraka na kuelekea ziwani?"
"Nimepata mzuka wa kwenda kuchezea maji mama watoto" nikamjibu huku nikichezea maji ingawa kichwani mwangu akili iliniruka wakati huo.Basi nikageuza na kuelekea upande aliokuwepo.
Ilipofika saa tatu usiku huku kichwa changu kikiwa na mawazo tele juu ya simu itakayopigwa na hamu ya kula ikiwa imenitoka na baadhi ya vyakula vikinikodoea macho nilijiuliza.
Mimi wa kunywa bia moja saa zima? Kweli mawazo yamenishika.
Muda wote nilikuwa nikiitazama simu ili kuona nini kitajiri.
Muda wote nilikuwa nikiitazama simu ili kuona nini kitajiri.
Muda ulizidi kwenda na ile bia ikanizia na hatimaye kuyafumba macho yangu kwa usingizi mzito.
Asubuhi nililipoamka nikakuta missed call zaidi ya 10 na meseji moja kutoka kwenye ile namba.
Kwa kweli nilitamani nisingeamka na kuelendea na usingizi ulionifariji sana.
Wazo likanijia kichwani "haya mambo nimshirikishe mke wangu?"
Nikaona nijikaze kiume na kutoka kwenda bafuni kuoga bila kuifungua ile meseji.
Nikaona nijikaze kiume na kutoka kwenda bafuni kuoga bila kuifungua ile meseji.
Bafuni nilikaa zaidi saa moja nikiitafakari ile meseji itakuwa ina nitaka nini mimi?
Niliporudi toka bafuni nikaitazama ile simu juu ya kitanda ila wakati huu nikaifungua chupa yangu ya pombe kali aina ya grants na kuigigida ili kujiongezea ujasiri.
Nikaitazama ile simu ambayo ilikuwa muda huo kiganjani kwangu kisha nikaufungua ule ujumbe.
Jumbe uliandikwa hivi, " acha kuendekeza pombe wewe wanaume, pombe sio chai ambayo utakunywa na maandazi ili kutatua matatizo yako kuwa wanaume wewe!!"
Duuh!!! Hakuishia hapo mstari ulionichosha zaidi ni huu uliosema hivi, " nitakupigia baadae sasa leo zima simu uone!"
Dakaika kama tatu hivi wakati na itafakari hiyo sms nilisikia kelele toka nje. Nilipotoka nje nilimwona mke wangu alikuwa akiniita huku akilia kwa sauti ya kuchanganyikiwa.
Mtoto wetu alidumbukia kwenye maji na kwa bahati nzuri aliweza kuokoka baada ya mramaria mwema kumwokoa.Hivyo basi tukaelekea hospitali kupata matibabu zaidi.
Ilipofila mida ya saa kumi jioni tukiendelea kumwangalia mwanetu nilipokea ujumbe mwingine.
Kwa kuwa nikikuwa na stress za mwanangu niliufungua ule ujumbe bila kufohia na kuusoma.
Ujumbe ule lisema, " pole baba na mjukuu, manaendeleaje mbona simu yako haipokelewi?"
Duuuuuh, nilishusha pumzi ndefu baada ya kungundua ujumbe ule ulikuwa wa mama.Nilipomaliza kuusoma ule ujumbe nikairudisha ile simu na kuelekea wodini kumwangalia mtoto na kumwambia mke wangu juu ya ujumbe ule.
Tukaruhusiwa muda mfupi baadae na kuelekea hotelini ambako tulipofika hotelini mhudumu wa hotel aliniita na kuniambia kuwa nina ujumbe wangu.
Ujumbe huo ulitoka kwenye namba ilele na baada ya kuzisoma zile namba nikagundua ni namba ile ile ambayo hunipigia
Ujumbe ule ulisema hivi, .............................. .......................
Itaendelea kesho muda kama huu
Share kama umeipenda
soma kupitia whatsapp 0713317171
soma kupitia whatsapp 0713317171
0 comments: