LANGO LA MOTONI Sura ya 8

07:46:00 Unknown 0 Comments



SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

Mtunzi: Fred Kihwele 0713317171

Sura ya  8

Ilipoishia

Ulikuwa umepita mwezi mmoja tangu mzee zombo afanikiwe kuteketeza nyumba ya aunt amina ambaye ni dada yake wa damu ili tu kuhakikisha anatumia nafasi hiyo kupoteza kabisa utambulisho wa samira na kwa habari alizokuwa nazo ilikuwa ni kwamba samira alikufa katika moto huo mkubwa ulioteketeza kila kitu.

Endelea

Mzee zombo alikuwa akisherehekea ushindi  wa kumtoa duniani   samira na watu walikuwa wakinywa kwa furaha na  katikati ya tafrija hiyo mara gari la polisi likaizingira nyumba hiyo.

Polisi walishuka kwa mwendo wa haraka na kulizingira eneo hilo kwa kubana kila upenyo na ndipo mkuu wao akingia ndani na kumwita mzee zombo. Wakati huo mzee zombo yeye wala hakuwa hata na dalili ya hofu zaidi ya kutabasamu.

"karibuni wakuu, polisi ni sehemu ya usalama na najua mpaka muda hu nipo chini ya ulinzi yani kila idara iko salama"


"Ndugu hatujaja kwa utani hapa, uko chini ya ulinzi na tunakuhitaki uje kituo cha kati hapa kwani kuna maelezo tunayahitaji kutoka kwako" alitoa amri hiyo kamanda ambaye hata kwa sura yake kamwe usingelimwingia kwa neno lolote.

" tuliza munkari kamanda, kwani kuna nini la haraka hivyo ambalo sitakiwi kupata hata dondoo kabla ya kwenda huko kituoni? hebu tukae chemba tuongee sie watu wazima bwana" aliongea maneno hayo bilionea wa ukubwani mze zombo huku akiacha amri ya kupewa vinywaji wale polisi wengine waliokuwepo pale ndani nae akaingia chemba na kamanda mkuu.

" sikia mzee zombo, kijana wako mmoja alionekana  katika tukio la moto lililotokea hivi karibuni na kuiteketeza nyumba, hivyo unahitajika kituoni kwa ajili ya malelezo"

" ha ha ha kumbe ndio hilo tuu kamanda? kwani nani mwingine anajua suala hili?"

" Limenifikia mimi pale na upelelezi wa kwanza umeonesha ni nyie mnaohusika kwani inasemekana pia hamna maelewano mazuri na nduguyo"


" hatuishi vizuri na nani? labda wao hawaishi vizuri na mimi, mimi ni mtu wa watu bwana na kama hauamini kuwa mimi ni mtu wa watu basi leo nitakuonesha kuwa mimi ni mtu wa watu" aliongea mzee zombo huku akiingia katika chumba kimoja na aliporudi alirudi akiwa na bahasha ya kaki iliyoonekana kuwa nzito.

" sasa kamanda, naomba ni kukabidhi hii bahasha na kila kitu ili hii kitu ishie si unajua tena masuala ya heshima maana ni watu tu wanataka kunichafua na si unajua nataka kugombea ubunge?"

" hilo nalielewa  mzee mwenzangu hebu niachie mimi na kwa advertise utaona nikitoka hapo nje, kwanza ngoja niumalizie huu mvinyo kabla sijatoka" aliongea kamanda huyo huku akiificha vyema bahasha ile na kisha akaunyanyua mvinyo uliokuwa kwenye chupa akaugigida na kutoka nje kwa haraka


" haya afande tangulieni nitawakuta kituoni kuna jambo la kiitelejensia nataka kulishughulikia" alimaiza kamanda huyo akiwaacha wale vijana wakiondoka na yeye akarudi ndani na kuendelea kupata mvinyo katika chumba hicho walichokuwa wamekaa wawili tuu.

" sasa kamanda mimi nitaomba sana nikutumie kuanzia sasa, maana kuna watu wananipiga vita sana hivyo nitaomba msaada wako?

"hiyo haina shida mzee zombo wewe muda wowote ukiwa na jambo nishtue" alimaliza maneno hayo kamanda  na wakaendelea na maongezi kwa muda na kisha wakaangana.


***
Ijumaa tarehe 26.07.2002

"Mama ulisema utanisimulia mkasa mmoja na nisiumie na mkasa huo, kwani unahusu maisha yangu, sasa nimekuwa mkubwa nina miaka 15 na leo ndio siku yangu ya kuzaliwa naomba unisimulie"

"Ni hadithi ndefu sana mwanangu na sikupenda uifahamu ila nafikiri ni vyema uifahamu na  naamini pia haitakufanya upoteze mapenzi yako kwangu"


"mama unajua wanitisha sana? niambie basi tafadhali mama yangu"


" silikiliza mwanangu Salha, Kama ujuavyo kuwa mimi kazi yangu ni muuguzi mkunga, miaka kumi na tano iliyopita nikiwa kazini alikuja mama mmoja ambaye alikuwa kazidiwa na uchungu na uchungu huo ulitokana na mshtuko alioupata.

Alipokelewa na mimi nikawa msaidizi wake pale na akajifungua mtoto kabla ya muda wake na mtoto huyo alizaliwa akiwa na miezi saba. Ikabidi abaki pale hospitali hata baada ya mama yake kuruhusiwa ili aweze kuhudumiwa na mitambo maalumu ya kulelea watoto wa namna hiyo.


Kila siku asubuhi, mchana na jioni mama yule alikuja kumtembelea mwanae akiwa na baba na mtoto wao mwingine wa kike. Mama yule pamoja na familia yake walikuwa wazuri na walipendana sana.

Siku moja majira ya asubuhi alikuja kama kawaida na alipotoka muda mfupi baadae taarifa zilizagaa na kusemekana kuwa baba na mama wa mtoto yule walikufa walipokuwa wakitoka kumpeleka mtoto wao shuleni baada ya kutoka pale hospitali.

Basi baba na mama yule walizikwa na baada ya hapo familia yao ikaingia katika mgogoro mkubwa sana.Na kwa kuwa mimi nilikuwa nikimsimamia mtoto yule pale hospitali, basi alipofikia muda wa kutoka kwenye zile mashine nilimpeleka kituo chakulelea watoto na baada ya kuanza kutembea niliamua kumchukua na kukaa nae kwa siri kwani sikutaka ndugu zake wajue baada ya kupata kisa cha kumficha mtoto wa yule mama aliyebaki hai na ndugu walikuwa hawajui lolote juu ya mtoto aliyeachwa hospitali.

Mtoto huyu nikamtunza kwa mapenzi ya dhati na mpaka hivi leo ni binti mkubwa na anayesoma kidato cha tatu na jina lake anaitwa SALHA yaani wewe mwanangu. Kwa hiyo ukweli ni kwamba wewe ndio mtoto yule niliyekuwa nikimtunza pale hospitali."


Salha alipatwa mshtuko na ku...

KIsa hiki kitaendelea kesho jioni na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia whatsapp wasiliana nasi kwa whatsapp namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini


KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

You Might Also Like

0 comments: