LANGO LA MOTONI CHAPTER 11

08:20:00 Unknown 0 Comments




SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 11

Ilipoishia


Samira alimshukuru sana  na wakaachana na ben kwa miadi ya kuwa aende mpaka hostel akaweke mizigo yake sawa ili dereva aende kumchukua na kumpeleka hoteli mpya.


Samira alifika mpaka pale hostel na kabla ya kuufungua mlango wake akaona aende pale alikojificha usiku kwani kumbukumbu ilimrudia na kukumbuka kila kilichofanyika pale jana yake usiku na wale watu waliokuwa dirishani kwake.

Alipolikaribia dirisha lake kwa chini samira aliona.......................


Endelea


Alipolikaribia dirisha lake kwa chini samira aliona kuna pakiti ya sigara iliyotumika na kilichimfanya asimame na kuokota ilikuwa ni business card moja iliyokuwa na jina la  h zombo ambaye alionesha kuwa ni mmiliki wa kampuni moja ya usindikaji vyakula na matunda.

Kilichomshutua zaidi ni nyuma ya  business card hiyo kuwa na jina lake na la aunt amina. Moyo ulimruka na ghafla jasho la uoga likaanza kumtoka bila hta ya kutarajia akajikuta akitamka " Mungu wangu, ina maana watu hawa bado wananitafuta mimi na aunt amina, na je huyu mzee kombo ni nani?" 

Hata kabla ya kujipa jibu akasikia muungurumo wa gari likija alipochungulia akaona ni dereva aliyetumwa na Ben, akaificha ile business card na kisha kaingia kuchukua mizigo na kuondoka kuelekea hoteli.

Hoteli hiyo ilikuwa nzuri na aliufurahia ulinzi wa eneo hilo na kwa hakika akijesemesha " Asante Mungu naamini kwa muda hapa nitakuwa salama na naomba umrejeshe salama aunt amina na hakika tuweke mikononi mwako ili tuwe salama"

Kwa upande mwingine mapambano huko mtaani yalipamba moto sana kwani samira alipotea kutoka mikononi mwa vijana wa mzee zombo. Walijaribu kufuatilia kila kona lakini hawakupata dalili yoyote juu ya wapi aliko samira ikabidi wampigie simu bosi wao.

" Pumbavu sana nyie yaani mnakuwa kwama landline crocodilelicious, yaani katoto kadogo kanwashinda... Sasa nasema nitamtuma mtu aje awalete hapa muone moto au mpaka jioni mnipe jibu zuri"

Kijana aliyekuwa anapiga simu akajikuta akishindwa kuvumilia na kucheka na kumuuliza, "mzee kwani hiyo landline crocodilelicious ni nini?"

" acha ujinga, hilo swali muulize baba yako ambaye hakukupeleka high education institute of centre, hapo nimekutukana sana kwa kiingereza, haya sina muda wa kuongea na mapuuzi sasa nasema rudini kazini"

Kijana yule aliishiwa nguvu na kujikuta akikaa chini na kucheka hasa akikumbuka kiingereza cha mzee zombo ambaye hakuwa na historia ya kuhudhuria shule kama alivyokuwa akijitamba na maneno ya kiingereza kisichoeleweka na muda mfupi baadae waliondoka eneo hilo kuendelea kumsaka samira.


Siku hiyo samira aliwahi kuamka na tayari alikuwa ameshajiandaa akimsubiri Ben ili waende airport kumpokea aunt amina ambaye akikuwa akirudi siku hiyo. Ben alifika pale hotelini akiwa analalamika njaa hivyo akaona ni boda aagize chakula kwa kuwa muda ulikuwa bado unaruhusu hivyo wakajumuika pamoja na samira.

Muda mfupi baadae ben na samira walikuwa sehemu ya kupokelea wageni pale airport. Samira alikuwa kavaa sketi yake fupi na top moja iliyomfanya aonekane vizuri hasa chuchu zake zilizokuwa zimechomoza pale kifuani mithili ya vichuguu uchungu viwili huku sketi ikiuacha mguu wake uliojazia nao upate kuonekana kiurahisi.

Lakini hips, nywele ndefu za kimanga na jicho la samira ndio vitu vilivyowafanya baadhi ya wanaume wakware wenye nia binafsi na samira wamkodolee macho huku wengine nao wakimchukia ben kwa kuwa karibu na binti huyu ingawa nae ben mara moja au tatu alidakwa na jicho la samira akiwa anamkodolea macho na akapotezea kwa kumsifia au kumfariji juu ya aunt amina.

Aunt amina aliwasili pale baada ya ndege yake kushuka samira alipong'aza aunt amina alirukwa na furaha na kujikuta akimkumbatia na kulia kwa furaha na hakuamini kama kweli alikuwa kapona na anaona tena.Walingia garini na ben akawachukua moja kwa moja mpaka moshono na kwenda kupaki mtaa wa ichenga na kisha wakashuka garini.

Aunt amina alisita kungia ndani na akajikuta akitokwa na machozi na .................


KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini



KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki


You Might Also Like

0 comments: