LANGO LA MOTONI CHAPTER 10
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
Mtunzi: Fred Kihwele 0713317171
CHAPTER 10
Ilipoishia
"Ok, basi mie nakuacha nafikiri zile hela bado unazo hivyo hakuna shida upande wako, nitakucheki kwa simu mida mida" Alihitimisha Ben na kisha wakaachana na samira yeye akaingia hostel.
Wakati anakaribia mlango wa hostel samira kuna kitu kilimfanya asite kuingia na kuamua kurudi nyuma na kujibana sehemu kwani muda huo giza lilikuwa limeanza kuwa la kumfanya mtu asione vyema.
Akajisogeza hatua kama nne na ku...................
Endelea
Akajisogeza hatua kama nne na kukijibanja pembeni ya ukuta wa hostel hiyo, sehemu ambapo hakuna mtu ambaye angefanikiwa kumwona kwa urahisi ingawa yeye aliweza kuona na kusikia vyema kila kilichoendelea.
" Oya huyu mtoto inaonekana hayupo na kama haitoshi muda huu bado kweupe kweupe na kuna wapangaji wengine wanaweza kuja na kuharibu deal, kama vipi wewe zima simu ili boss asitupate muda huu na ikifika mida ya saa sita tuje tufanye kazi hawa ngedere wakiwa wamelala"
Alimaliza kuongea mtu mmoja ambaye kwa mbali alionesha kama alikuwa akitaka kurudi lango kuu kutokea dirishani mwa chumba cha kulala samira alipokuwa kasimama huku mwenzie akimfuata taratibu.
Hazikupita hata sekunde kadhaa, samira alishtuka kuona akiwa kashikwa na mtu aliyembana kwa kitambaaa fulani kwenye mdomo wake na pia kilichoifunika pua yake jambo lililomfanya alishindwe kupiga kelele hata ile ya kurusha mguu na hatimaye taratibu alijikuta akiishiwa nguvu na kupoteza fahamu.
Saa tano na dakika 45 za asubuhi mlango wa chumba uligongwa na kisha dada mmoja aliingia na kukaa kitanda alichokuwa kalala samira ambaye nae ndio alikuwa akianza kurudiwa na fahamu.
" Umeamkaje dada?"
"salama kiasi kwani nipo wapi hapa na nimekujaje hapa?" Alihoji samira ambaye kwa uchovu alikuwa akijiweka sawa pale kitandani.
" Dada, hii inaitwa PLEASE REST IN PEACE GUEST HOUSE," aliongea dada huyo ingawa ilimbidi atulie kuongea baada ya samira kushtuka kulisikia jina hilo.
"Rest in peace!!!!!! yani kama ile ya R.I.P? oooh maskini mimi!!!, MUNGU wangu kwani nini tena?"
"samahani dada, sio rest in peace kama maana ya ile ya kumwambia marehemu hapana,hii ni maana nyingine" aliongea dada huyo huku akimsaidia kumpa tishu ya kufutia machozi samira na kisha akaendelea kuongea
" jana nilikuwa zamu ya usiku ambayo huishia asubuhi ya leo saa mbili, na wakati nikiwa mapokezi nilisikia kishindo hapo nje na nilipoenda haraka nikaona ukiwa umeanguka pale sakafuni.
Ulikuwa haujielewi na kama umelewa vile maana hukuweza kuongea wala kusema lolote. Nikakupekua na kuona mfukoni una shilingi laki 2 na simu yako, vyote nikakuwekea na kuamua kukupa chumba ili upumzike kwani nilihisi utakuwa uliwekewa madawa ya kulevya ili wakuibie na sasa ulifanikiwa kufika mpaka hapa na unahitaji msaada"
Wakati wote huo samira alikuwa kashikwa na bumbuazi iliyomfanya hata yale machozi yakauke na sasa akabaki kushangaa kwani kumbukumbu pia zilianza kumrejea na akakumbuka kuwa jana yake hakuwa na fedha nyingi hivyo bali alikuwa na shilingi elfu kumi na mbili na tena hakuwa ametembea nayo.
Mawazo yakaanza kumrudia tena na wakati huu akafikiria suala la mtu kumwekea fedha na kumpeleka katika hoteli hiyo ambayo hajawai kuisikia na haraka akamuuliza yule dada,
" Samahani dada kwani mtaa huu unaitwaje? na je ni mbali sana na stand kuu?"
" hapana ni umbali mdogo kwani unapanda daladala moja tuu au hata kwa bodaboda ni shilingi elfu tatu tuu."
" ok, asante naomba simu na hela" Samira alimwomba dada huyo na kisha akapokea fedha hizo na baada ya kumlipa akaondoka haraka na kuchukua bodaboda mpaka stand kuu.
Alipofika stand kuu akaenda moja kwa moja kwenye kibanda kimoja cha simu na kuweka zile fedha kwenye simu yake na baada ya hapo akampigia simu Ben na baada ya ben kumwambia sehemu aliyoko. Samira alichukua tena bodaboda na kumfuata.
Walionana na baada ya kumsimulia ben, ben akamhakikishia usalama na kumwambia sasa atahakikisha anamwamisha pale na kupeleka hoteli nyingine ambako atalala kwa siku mbili na siku ya tatu yake wakishampokea aunt amina basi watahama eneo hilo na kwenda kuishi kule Moshono ambako hakuna atakayepajua.
Na kuhusu suala la pesa ile laki mbili ben akamwambia umefanya vyema kuiweka kwenye simu ili tusubiri tuone kama kuna mtu atapatikana ili tumchukulie hatua za kisheria, maana nafikiri kuna kitu kinasukwa na hatujui ni nani maana unakutana na mambo makubwa sana dada samira.
Samira alimshukuru sana na wakaachana na ben kwa miadi ya kuwa aende mpaka hostel akaweke mizigo yake sawa ili dereva aende kumchukua na kumpeleka hoteli mpya.
Samira alifika mpaka pale hostel na kabla ya kuufungua mlango wake akaona aende pale alikojificha usiku kwani kumbukumbu ilimrudia na kukumbuka kila kilichofanyika pale jana yake usiku na wale watu waliokuwa dirishani kwake.
Alipolikaribia dirisha lake kwa chini samira aliona.......................
KIsa hiki kitaendelea JUMATATU na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia whatsapp wasiliana nasi kwa whatsapp namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini
KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki
0 comments: