Amini usiamini MUNGU yupo anatenda miujiza,

18:24:00 Unknown 0 Comments




Fuledi amini usiamini MUNGU yupo anatenda miujiza,

Miezi kadhaa iliyopita ilinibidi niondoke na kwenda mjini kujitafutia riziki kwani pale nyumbani mambo yalizidi kuwa magumu na mama yangu mzee anayehitaji msaada wetu kifedha na mme aliyenizalisha wanangu wawili alitutelekezea mwaka mmoja uliopita na kukimbilia inasemekana south Africa.

Nikiwa mjini ambako nilipata kazi ya uhudumu wa nyumba ya kulala wageni na wanangu nikiwa nimemwachia mama na dada yangu mdogo, nilpigiwa simu yakunitaka nirudi nyumbani mara mmoja.

Kama ujuavyo kama mama sikuwa na cha kupoteza muda nikaondoka baada ya kuomba ruhusa na kwenda zangu kijijini.

Nilifika kijijini na kushuhudia kwa mwanangu ameukwa kwa zaidi ya wiki ugonjwa wa kuharisha na imefikia kipindi ndio anaanza kuharisha damu.

Sikuwa na hela lakini ujasiri ukanijia na kwenda duka moja la rafiki yangu nikakopahelana kumpeleka yule mwanangu hospitali na kuanza matibabu.

Hali ikazidi kuwa mbaya madaktari wakajitahidi lakini matumaini ya kupona yakaanza kunipotea.

Nikiwa kitandani pale huku nalia mwanangu mdogo wa mwisho akasema,"mama dada atapona tu kwa jina la yesu na wewe kabla ya kulala leo usiku sema atapona"

Sikuwahi kuwa na tabisa za kusali usiku au asubuhi au nikiwa na tatizo lolote lile, basi nikamsikiliza na kuendelea kuumia kwa chini chini pale kuhusu hali ya mwanangu

Usiku ule nikiwa pale hospital kabla ya kulala nikaifungua biblia ambayo aliniletea mwanangu na kusoma maneno haya,"Nikipatwa na mashambulizi ya magonjwa yaletwao na yule mwovu naiita jina la Jehova Rafa yaani Mungu mponyaji."

Hakika sio mimi tu mpaka madaktari walishangazwa baada ya kuamka asubuhi na kuona mwanangu kaanza kufungua macho na kaweza kula na siku mbili baadae tukaruhusiwa kutoka pale na mpaka leo mwanangu ni mzima wa afya tele..

Kweli kumtegemea MUNGU ni zaidi ya kilakitu hapa duniani

You Might Also Like

0 comments: