Baba mwenye nyumba ananiharibia ndoa
Kwa bahati mbaya nimefukuzwa kazi na maisha
yameanza kuwa magumu sana kwangu na familia
yangu.
Hali hii ikapelekea hata kulipa pango iwe tatizo na
hivi karibuni nilikutana na baba mwenye nyumba
akaniambia sasa nisilipe ila nikiwa na kazi
nitaanza kumpa kwani sasa kanisamehe.
Na wiki jana kamwajiri mke wangu katika duka
lake kubwa la kuuzia madawa ya binadamu.
Mbaya zaidi ni kwamba mtaani kuna tetesi kuwa
mke wangu anatembea na baba mwenye nyumba
akiwa kazini.
Na baada ya uchunguzi nimebaini
kuna ukweli.
Naombeni mnishauri nini nifanye maana
nashindwa kuamini kama mke wangu ambaye
nimezaa nae watoto wawili anaweza nisaliti kwa
changamoto hizi....
0 comments: